Mpaka sasa mitandao ya kijamii imekusaidiaje katika harakati za kupambana na umasikini?

Mpaka sasa mitandao ya kijamii imekusaidiaje katika harakati za kupambana na umasikini?

Mkuu kwema? Pole na uchovu wa safari ya kuperuzi JF.

View attachment 2528237

Boss, ebu tuongee kidogo kuhusu hii mitandao ya kijamii mpaka leo imekusaidia chochote ?

Au unaonaga mauzauza tu 😅?

Graduate uliyehitimu chuo na hauna Ajira, vipi hii mitandao ya kijamii unaichukuliaje?

Ni sehemu ya kupotezea muda na mawazo baada ya kutemmbea sana kusambaza CV?

Mwanachuo ambaye bado upo hapo chuoni unasoma, hii mitandao ya kijamii kwako unaionaje? Je unaiona kama huyo graduate hapo juu anavyoiona au unalo jicho la tofauti?

Mfanya Biashara vipi kuhusu wewe mtazamo wako kuhusu mitandao ya kijamii ukoje?

Ni baadhi ya maswali tu ambayo yanaweza saidia katika kufanya tathmini fupi juu ya mtazamo wako kuhusu mitandao ya kijamii.

Sasa naomba nikupe siri hii wewe mkuu unayesoma hii post,

Mitandao ya kijamii ni Dili ambalo Ukiweza kufahamu njia sahihi ya kuitumia unaweza hifadhi vyeti vyako kwenye makabati na badala ya wewe kutafuta kazi, waajiri watakutafuta wewe wakupe kazi.

Soma kwa kutafakari na ruhusu akili yako kuelewa hayo maneno hapo juu.

Kabla ya kuingia mtandaoni jiulize nini utaenda kufanya mtandaoni.

Ebu Fikiria, unaweka bando lako, unafungua Facebook, Instagram au Jamii Forum halafu unaingia kutazama tu vitu mpaka bando linakata.

Halafu unatafuta tena pesa unaweka bando lingine kurudi kufanya vilevile ulivyo fanya mwanzo.

Na katika harakati zako zote hizo kukimbia kimbia Instagram mara Facebook, hujakaa Sawa upo Twitter na kabla ya kutulia unakumbuka nyuzi za MMU unarudi Jf.

Hakuna hata Mia unaingiza, na hakuna mtu yoyote unaye gusa maisha yake huko mtandaoni.

Kiufupi unaishi ndani ya MATRIX (Gereza huru) pasipo kujua.

Ebu jaribu kutafakari muenendo wako mtandaoni halafu kaa ujiulize naweza kufanya nini na bando langu na kufikia malengo yangu katika maisha kwa kutumia mtandao.

Unataka connection? Kujenga ujuzi? Kujenga biashara yako kuwafikia watu wengi? Kuongeza maarifa yako?

Aisee hii mitandao ya kijamii imejaa majibu yote hayo.

Amka, halafu Usione uvivu kutafuta watu wanaoweza kukusaidia kufikia hayo malengo yako mtandaoni.

Ni hayo tu mkuu.

Imeandaliwa na Mr. Purpose 0752026992.

Tuambie namna gani mitandao ya kijamii imekunufaisha au kukupotezea muda. Andika tujifunze zaidi.
Imenisaidia kupata hili andiko lako
 
Nimekuwa admin wa ma group 3 ya ngono, mawili ya kubet na moja la vichekesho.
 
Huwa nakufuatilia sana mkuu kuanzia LinkedIn hadi Instagram.

Unafanya kazi kubwa sana na ni mfano mzuri wa kuigwa.

Ukiwa na malengo thabiti na nia ya kweli hakuna kitu utashindwa kukipata mtandao.

Muhimu tu uelewa kwanini unafanya.

Be blessed brother Kelvin.
Nifuatilie na mimi naitwa "Bill Kiwia"
 
Ni ngumu sana kupambana na umasikini nipo zangu napambana na utajiri nzega
 
Ni ngumu sana kupambana na umasikini nipo zangu napambana na utajiri nzega
Mkuu umeniacha njia panda.

Unapambana na utajiri kwa lengo la kuuondoa au Unapambana kuupata?
 
Nimekuwa admin wa ma group 3 ya ngono, mawili ya kubet na moja la vichekesho.
Mkuu naomba kujua muamko wa watu ukoje katika makundi hayo na njia gani unatumia kupiga pesa kupitia makundi hayo?

Hii inaweza kuwa fursa. Tuelimishe mkuu.
 
Back
Top Bottom