Uchaguzi 2020 Mpaka sasa nafikiria Gwajima atakavyomshukia Halima kama mwewe baada ya kuitwa Mrembo

Uchaguzi 2020 Mpaka sasa nafikiria Gwajima atakavyomshukia Halima kama mwewe baada ya kuitwa Mrembo

Wana JF kama kuna siku naingojea kwa hamu kubwa na ambayo namuomba mwenyezi Mungu anijalie nikutwe na afya njema na niwe sehemu ya mkutano huo wa ufunguzi wa kampeni za askofu Gwajima au niwe sehemu ambayo nitaweza kuona mubashara.

Hii shauku imesababishwa na Halima James Mdee kumuita ASKOFU Gwajima mrembo.

Mpaka sasa nafikilia Gwajima atakavyomshukia Halima kama mwewe anavyoshukia kifaranga cha kuku.

Mimi nadhani CCM hakika walifanya utafiti mkubwa kumchagua gwajima jimbo la Kawe, nasikio la kufa halisikii dawa, maana Mdee naona kachokoza nyuki yeye mwenyewe.

Clip ya mgombea wa CHADEMA H. Mdee inasambaa u-tube kwa kasi akimuita Gwajima mrembo na kumfundisha swaga za kitaa.

Mwe mwe mwe...... halima huyu huyu ninaemjua au ametoa wapi huo ujasiri wana JF?

Nawaomba wana JF tupashane siku na tarehe ya ufunguzi wa kampeni wa askofu Gwajima najua itakuwa burudani kama ya SIMBA DAY au ya WANANCHI Dar young Africa, nchi itasimama.

Halimaaa nasikia bishop saivi anakusanya data zako zote tangia ukiwa mtoto.

Usilalamike maana umeanza mwenyewe yangu macho.
Halima ataenda kusimamia zile cruiser zake alizomkabidhi kaka yake kule arusha ziko tatu. Au na yeye aolewe na Esther bulaya kama atashinda ubunge kule bunda.
 
Atajuta kuzaliwa ngoja Baba mchungaji amwage cheche.
 
Halima ataenda kusimamia zile cruiser zake alizomkabidhi kaka yake kule arusha ziko tatu. Au na yeye aolewe na Esther bulaya kama atashinda ubunge kule bunda.
Huyo Gwajima aliewatukana waislam hana chake Kawe

Sent from my Infinix X573 using JamiiForums mobile app
 
Mengine sijui ila nilichokiona kwako ni uandishi mbovu..... majina ya watu na ya Mwenyezi Mungu tunayaanzia na herufi kubwa. Plus kuchanganya L na R. Jitahidi, ni vitu vidogo vidogo kama hivi hutenganisha wale waliokuwa serious kumsikiliza mwalimu na wale waliopita shule kukua. Ni mtizamo wangu tu
"Hata wa la saba wanatosha!"
Usimlaumu sana huyo.
Alishindwa za Bashite wanaetoka kijiji kimoja ataweza za sauti ya zege aliyemkuta kitaa?
 
Gwajima kawe hatoboi,,na asipokuwa makini atapoteza wafuasi kanisani atachuja kabisa
 
Akiingia kwenye gemu ya siasa full kashfa matusi sijui Kanisani atakuwa anahubiri nini
 
Mimi katika hili nina mtizamo kuwa Mch. Gwajima hatakuwa na muda wa kurudisha personal attacks kwa mshindani wake ambaye tayari ameshaonyesha hofu kubwa na ya wazi kabisa. Ninaamini atajikita zaidi kwenye ilani ya uchaguzi ya chama chake. Kuna watu watatu tu ambao ni vigumu mno kwa wao kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu na anayeongoza kwenye kundi hilo ni Mch. Gwajima. Inawezekana kwa mgombea mwingine yeyote yule kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu, ila si Gwajima. Kwa Gwajima uwezeakano huo haupo!
Gwajima yupo too weak kwenye kujikita kwenye hoja,mara nyingi anapenda ligi za Personal,angalia alivyofanya kwa Pengo angalia alivyofanya kwa Makonda,video ya Ngono ndio imemtuliza Gwajima.Nina uhakika ile clip itajirudia tena huko Kawe
 
Shida Kuna watu wanasema wanasiasa au wanafuagilia siasa kumbe hakina kitu.

CDM Wana Kanda kumi ukifiatilia kwa karibu utaona Sasa wanapita Kanda moja moja, na viongozi wa Kanda husika ndio waandaji wa kampeni za eneo lao. Hivyo huwezi kumuona sugu Mwanza, au Msigwa utawaona kwenye Kanda zao. Lakini pia wenyewe ni wagombea na Kuna mapingamizi mengi lazima wapambanie hayo mapingamizi kwanza.
 
Gwajima hana ujanja kwa halima, tena asipokaa sawa atapekekwa jando nyingine.
 
Gwajima yupo too weak kwenye kujikita kwenye hoja,mara nyingi anapenda ligi za Personal,angalia alivyofanya kwa Pengo angalia alivyofanya kwa Makonda,video ya Ngono ndio imemtuliza Gwajima.Nina uhakika ile clip itajirudia tena huko Kawe
Analysis yako ni sahihi ila bado hatujawahi kumshuhida hata siku moja, akiwa amesimama kwenye jukwaa la ki-Siasa na hivyo kwenye Siasa bado hajaonyesha kama yuko hivyo. Still, strength ya Gwajima haipo kwenye hoja kwamba ana maneno mazuri muno ya kuwafurahisha watu pindi anaposimama kwenye jukwaa, hapana. Strenghth yake iko kwenye social-ties, na hapa ndipo unapokuja lutofauti wa umaarafrufu wake ukimlinganisha na wanasiasa maarufu. Mwanasiasa maarufu ni yule anayejulikana na karibia kila mtu ndani na nje ya eneo lake la kupigiwa kura, na possibly anaweza hata akawa pia ana uwezo wa kuongea maneno ya kuwafurahisha sana wapiga kura wake. Tofauti na mtu mwenye strong social ties, yeye anapendwa na watu wote ndani ya eneo analoweza kupigiwa kura, si kwa maneno yake mazuri bali kwa matendo yake ya nyuma ambayo hayakuwa na mlengo au uhusiano wowote na kisiasa, na ambayo hatimaye yamepelekea akawa na rekodi nzuri sana ya mahusiano na watu walioko kwenye eneo lake naye.
Hii sifa niliyoitaja hapa mwisho ndiyo sifa pekee na mama ambayo huwa mara nyingi kama siyo zote, mtu akiwa nayo basi huwa inapelekea mtu huyo anachaguliwa kuwa Mbunge kwa mara ya kwanza
 
tunaandikaga Mungu na sio mungu umekosea pia na hapo
Uwnaweza dhani unajua kumbe na wewe hujui kuwa hujui, Mungu/God, na mungu,god ni maneno mawili tofauti, na yanatumika kwa usahihi kulingana na mwandishi husika, tunaandikaga? ndo nini?
 
Back
Top Bottom