Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Cheti fekiDhalim hana uwezo wa kutoa laana kwani yeye mwenyewe alikuwa laana.
Ukiandika kwa uchache hivi ninakusoma; ukiandika gazeti sisomi.Sasa kama huyasomi inanihusu nini? Unapata faida gani kunijibu ili kuniambia tuu kuwa haunisomi? Mimi nilijua hausomi chochote ninachoandika. Kwa kweli nilifurahi kwa sababu nilijua utaniweka katika "ignore list" yako nisikuchoshe. Lakini sishangai, maana uko hapa unamtetea Lissu lakini hautaki kukubali kuwa unakipenda chama chake. Au na wewe ni follower wa Lissu, sio chama chake?
Btw naandika maneno mengi kwa sababu najua wengi ni wavivu wa kusoma.
Amandla...
Kwa vile sikuandikii wewe bora uni "ignore" kabisa. Nitaendelea kuandika ninavyotaka na sio unavyotaka.Ukiandika kwa uchache hivi ninakusoma; ukiandika gazeti sisomi.
Kama unataka kujuwa mimi ni" follower" wa nani, jibu ni rahisi sana. Ni mfuasi wa TANZANIAmchana na usiku na siku zote za uhai wangu.
Kiongoz au chama chochote kikionyesha kuwa na maslahi kwa Tanzania, sina haya/aibu yoyote kukiunga mkono; kama nilivyo kuwa na matarajio na Bwana Mbowe wakati fulani kabla hajatekwa na ulaghai wa Samia. Sasa hivi matumaini yapo kwa CHADEMA, Lissu na viongozi wenzake. Lakini na wao wakionyesha dalili za kutetereka, hasa kuungana na kuikwamisha nchi, tutawaponda mawe vile vile kama wasaliti wa nchi yetu wengine wote.
Ile PhD ya kudesa iliyomtoa roho Ben Saanane siyo?Cheti feki
Majibishano na mimi kama unavyo fanya hapa ni kuniandikia mimi, na hilo ndilo nililo maanisha nilipo andika kuwa "sisomi gazeti". Sina sababu ya kukuweka kwenye "ignore list"; na wala sina kizuizi cha kutojibu hoja zako kama zipo, unapoziweka humu.Kwa vile sikuandikii wewe bora uni "ignore" kabisa. Nitaendelea kuandika ninavyotaka na sio unavyotaka.
Mtu uliyemtaka ndio ameshinda. Na kokote atakakokipeleka chama chenu ni juu yenu. Mbowe hahusiki.
FAFO.
Amandla...
Ni jambo jema kama ni hivyo. Kwa vile wewe ndie uliingiza suala la kutosoma nilichoandika bado naamini itakurahisishia kama utaniweka katika "ignore list" yako. Lakini ni uamuzi wako. Siwezi kukulazimisha.Majibishano na mimi kama unavyo fanya hapa ni kuniandikia mimi, na hilo ndilo nililo maanisha nilipo andika kuwa "sisomi gazeti". Sina sababu ya kukuweka kwenye "ignore list"; na wala sina kizuizi cha kutojibu hoja zako kama zipo, unapoziweka humu.
Sawa.Hakuna mahali popote nilipo kuzuia kuandika unavyotaka; kama wewe usivyo kuwa na uwezo wa kunizuia nisiyatolee maoni maandishi yako.
Kwa vile inaelekea umekuwa unanifuatilia kwa muda mrefu, nipe mfano wa mahali nilipomuombea Lissu ashindwe na CDM isambaratike. Mimi nilisema hafai lakini pamoja na hayo nikasema bora ashinde maana angeshindwa asingekubali matokeo na hivyo kuzidisha mpasuko katika chama chake.Sasa unasubiri huyo aliyeshinda kwa demokrasia uliyokuwa ukiiimba ashindwe na chama kisambaratikeili upate nafasi ya kuja hapa kutueleza ulivyojuwa hayo yote yangetokea hata kabla ya "demokrasia"!
Uchaguzi umepita na uongozi wa juu wote wa CDM ni Team Lissu. Mbowe anahusika vipi katika muelekeo wa sasa wa CDM? Demokrasia ilifanyika pale alipoweza kugombea, kushindwa na kukubali matokeo. Sasa hii inahusika vipi na uendeshaji wa sasa wa CDM? Au hamuamini kuwa kweli mlishinda na mmeshika hatamu?"...Mbowe hahusiki"? Wewe sasa umekuwa msemaji wa Mbowe wakati kote umejitangaza kuwa ulicho kuwa ukipigania ni "demokrasi"?
Sasa wewe hilo la Tundu Lissu "asingekubali matokeo" umelitoa wapi; wewe mwenyewe hata hapa unaonyesha ni kiasi gani unavyo subiri CHADEMA chini ya Tundu Lissu isambaratike; halafu nataka nikupe mfano wa maneno uliyo andika kuhusu hili kuonyesha ushahidi?Mimi nilisema hafai lakini pamoja na hayo nikasema bora ashinde maana angeshindwa asingekubali matokeo na hivyo kuzidisha mpasuko katika chama chake.
Una maana Wenje naye ni timu Lissu, na yule mama wa BAWACHA aliyetangaza kumuunga mkono Mbowe, pia ni timu Lissu?Uchaguzi umepita na uongozi wa juu wote wa CDM ni Team Lissu
Lissu hakuwahi kusema kuwa atakubali matokeo ya uchaguzi. Kabla ya uchaguzi mkaanza kupenyeza taarifa za watu kuhongwa na watu wa Mbowe ( kumbe walikuwa wanalipwa posho zao). Usiku wa kabla ya uchaguzi Lema akatoa taarifa kuwa kuna wapiga kura wao ambao wananyimwa vitambulisho. Waandishi wa habari walipoenda katika kituo husika wakakuta watu wanaendelea kupewa vitambulisho na hamna aliyenyimwa. Zote hizo zilikuwa ni kutayarisha uwanja kwa ajili ya kupinga matokeo kwa sababu waliisha jiaminisha kuwa Mbowe ni king'ang'anizi na atafanya kila namna abakie madarakani.Sasa wewe hilo la Tundu Lissu "asingekubali matokeo" umelitoa wapi; wewe mwenyewe hata hapa unaonyesha ni kiasi gani unavyo subiri CHADEMA chini ya Tundu Lissu isambaratike; halafu nataka nikupe mfano wa maneno uliyo andika kuhusu hili kuonyesha ushahidi?
Uongozi wa juu ni Mwenyekiti, naMakamu Wenyeviti. Katibu Mkuu na wenzake ni watendaji na wanatekeleza maagizo ya viongozi wa juu. Kamati Kuu sio uongozi wa juu. Humo utawakuta sio tu hao uliowataja bali watu kama Boni Yai, Sugu, Sharifa na Freeman Aikaeli Mbowe. Hawa hawahusiki katika uendeshaji wa siku kwa siku wa chama. Kama hata hilo hauelewi basi iko namna.Una maana Wenje naye ni timu Lissu, na yule mama wa BAWACHA aliyetangaza kumuunga mkono Mbowe, pia ni timu Lissu?
Naona hata subira tu ya kuiona CHADEMA ikisambaratika imekuwa ngumu kwenu?
Wewe inaonekana unayasema yote haya kwa sababu ulikuwa ni sehemu ya wahusika wa karibu katika mchakato huo, mimi sijui; kwa sababu sipo huko ulipokuwa wewe. Ila niliwahi kumsikia Mbowe akijigamba kuwa hana shaka na ushindi kwa sababu pesa ya kutosha ipo, na watu wa kumwezesha kufanya hivyo anao! Sasa maana ya majingambo hayo kabla ya uchaguzi mimi siijui.Lissu hakuwahi kusema kuwa atakubali matokeo ya uchaguzi. Kabla ya uchaguzi mkaanza kupenyeza taarifa za watu kuhongwa na watu wa Mbowe ( kumbe walikuwa wanalipwa posho zao). Usiku wa kabla ya uchaguzi Lema akatoa taarifa kuwa kuna wapiga kura wao ambao wananyimwa vitambulisho. Waandishi wa habari walipoenda katika kituo husika wakakuta watu wanaendelea kupewa vitambulisho na hamna aliyenyimwa. Zote hizo zilikuwa ni kutayarisha uwanja kwa ajili ya kupinga matokeo kwa sababu waliisha jiaminisha kuwa Mbowe ni king'ang'anizi na atafanya kila namna abakie madarakani.
Tuache kudanganyana, hauna ushahidi wowote wa Fundi Utumbo akiombea CDM isambaratike.
Sasa sikuelewi. Hawa hawakuchaguliwa kidemokrasia kama ulivyo taka wewe. Tatizo lipo wapi?Uongozi wa juu ni Mwenyekiti, naMakamu Wenyeviti.
Umewahi kumsikia mgombea yeyote akiingia katika mpambano na kusema kuwa anategemea kushindwa. Hata Heche alitangaza wazi kuwa wanaenda kumshinda Mbowe ingawa wanamheshimu. Hizo pesa ni kweli zilikuwepo na ndio maana alitoa milioni 250 kuwezesha mkutano ufanyike. Watu alikuwa nao ndio maana Bawacha walimchagua Sharifa pamoja na Lissu kumfanyie kampeni mshindani wake. Uo ndio ukweli wenyewe kama ulivyo ukweli kuwa Mbowe alishindwa kutetea nafasi yake.Wewe inaonekana unayasema yote haya kwa sababu ulikuwa ni sehemu ya wahusika wa karibu katika mchakato huo, mimi sijui; kwa sababu sipo huko ulipokuwa wewe. Ila niliwahi kumsikia Mbowe akijigamba kuwa hana shaka na ushindi kwa sababu pesa ya kutosha ipo, na watu wa kumwezesha kufanya hivyo anao! Sasa maana ya majingambo hayo kabla ya uchaguzi mimi siijui.
Unaposema nitakubali tu matokeo kama nitashinda. Hapo ni kuweka njia ya kuyabatilisha kama akishindwa.Sijui kama ulitarajia Tundu Lissu akubali matokeo hata kama ni matokeo batili!
Sasa sikuelewi. Hawa hawakuchaguliwa kidemokrasia kama ulivyo taka wewe. Tatizo lipo wapi?