Mpambano mkali kituo cha Polisi Nzega stendi kati ya Abiria na Polisi

Mpambano mkali kituo cha Polisi Nzega stendi kati ya Abiria na Polisi

Umeleta ushabiki sana kwenye hii habari sijaona kosa la polisi. Kosa lipo kwenye bus bovu ,mwendo mkali. Hivi mfano hilo basi lingewamwaga si mngelalamikia polisi hawakulizuia nzega stend. Pia mwenye basi ana makosa safari ndefu inahitaji dereva wawili.

Yaani hapo ni faini juu ya faini
kosa la mwendokasi dereva anaweka lock up au anaandikiwa fine??

Au mwenzetu bado unatembea kwa miguu maswala ya barababarani huyajui 🤣 🤣 🤣
 
Daah mkuu mwambie aliyekuchomekea auchomoe uandike vizuri yaan unakatika katika hadi sio poa
Pumba na upupu mtupu, najua ni umbumbumbu unakusumbua tuu... Ni hivi huyo askari alitakiwa aingie ndani ya Bus na baada ya kuwasalimia na kuwapa pole abiria awajulishe kosa la dereva na kifungu husika na adhabu stahiki. Makosa ya overspeed mengi ni faini na faini ina muda wa kuilipa. Baada ya dereva kuandikiwa makosa yake na faini anaruhusiwa na safari ili abiria karibia 65 waweze kufika makwao. Hicho kilichofanyika siyo ukamataji ni utekaji, kama ilivyo kawaida yao. Hivi ingekuwa huyo abiria mmoja asingeona dereva akitekwa si ina maana wangekaa hapo mpaka asubuhi??
 
Sina gari mkuu ni mwendo wa daladala tu.

Yeah lockup inamhusu na sio mara ya kwanza kwa dereva kuwekwa ndani kisa mwendo kasi. Pitia uzi wa mabasi sijui sauli utaona shuhuda za wananzengo kuhusu polisi na madereva wa mwendo kasi
kosa la mwendokasi dereva anaweka lock up au anaandikiwa fine??

Au mwenzetu bado unatembea kwa miguu maswala ya barababarani huyajui 🤣 🤣 🤣
 
hivi karne hii ya technolojia bado kuna magari ya kuwalaza watu njiani!!!???
 
  • Kicheko
Reactions: ALT
Sina gari mkuu ni mwendo wa daladala tu.

Yeah lockup inamhusu na sio mara ya kwanza kwa dereva kuwekwa ndani kisa mwendo kasi. Pitia uzi wa mabasi sijui sauli utaona shuhuda za wananzengo kuhusu polisi na madereva wa mwendo kasi
aisee tafuta kwanza pesa uwe na gari alafu ndiyo ujue makosa ya fine ni yapi na makosa ya lock up ni yapi.
 
aisee tafuta kwanza pesa uwe na gari alafu ndiyo ujue makosa ya fine ni yapi na makosa ya lock up ni yapi.
Aise hujui chochote alaf unaongea Sana.
Uendeshaji wa Njia ya hatari/overspeed kinyume na K/F 42
Adhabu yake chini ya k/f cha 63(2) (b) adhabu yake ni faini au kifungo kisicho pungua miaka miwili.
Kwahiyo ukiona unapigwa faini na kuachiwa siyo kwamba huwezi kukamatwa na kuwekwa lockup unakamatwa vizuri tu na ndani ya masaa 24 unapelekwa mahakamani na unachezea mvua miaka miwili jela ila kama ushahidi upo na hauna shaka ndani yake.
Sheria hapa Tz zinalegezwa sana zikiamua kukazwa kila mtu ataionja jela mfano kuna wengi sana tunafundishana magari/pikipik bila kibali chochote bila kujua ni kosa kisheria
 
Na zikishaua ndugu zao wanakuja kuilalamikia serikali na polisi hawakudhibiti mwendokasi
Achana nao hao sisi wa Tz huwa ni wanafki sana gari hata ikiwa mwendo mdogo likipata hitilaf likaanguka utaskia alikua anakimbia Sana, lakin akiwa mwendo kasi na mkafika salama anapewa sifa nyingi
 
View attachment 1967569
Wanabodi

Natumai mungu ni mwema kwa kila mmoja kwa kupata zawadi ya uhai.

Muhtasari wa habari.

Moja kwa moja kwenye mada. Mnamo tarehe 5/10/2021 nikiwa natoka Arusha kuelekea mwanza na basi la kiazi kitamu ulizuka msuguano mkali kituoni cha polisi Nzega stendi.

Polisi walimshusha dereva kwenye gari kimya kimya wakampandisha kwenye difender hadi kituo cha Polisi central. Abiria baada ya kutomuona dreva, tukaenda kituoni kuhoji, askari wa zamu anasema dereva kasnikwa, kapelekwa central, moto ukawaka, abiria tunamtaka dereva.

Habari kamili.

Safari kutoka arusha ilianza saa 11:57 alfajiri stendi ya mabasi ya kwenda mikoani. Gari baada ya kukaguliwa lilitoka. Baada ya masaa matatu, tulifika stendi ya babati mkoani manyara, trafiki polisi walikagua gari tena, wakakumbusha abiria kufunga mkanda, kama baada ya dakika 20 tangu kutoka stendi ya babati gari likaanza kutoa harufu kana kwamba matairi yanaungua kumbe ni clutch plate inaungua na imeisha. Gari likasimama likashindwa kwenda, abiria tusijue hili wala lile safari imesimama, konda akasema abiria tunaomba mvumilie, dreva ameenda kuchukua maziwa, kumbe ni fiksi, abiria wakamwambiia usitufanye watoto wadogo, gari ni mbovu, clutch plate iimeungua, gia haziingi, hakuna maziwa wala nini. Dereva akomba radhi akasema gari limeharibika.

Ilikua karibu saa 3:45 asubuhi, wakajaribu kutengeneza hadi saa tano kamili, gari likawashinda. Wakapiga simu, fundi akatokea Kateshi, akafika saa sita kasoro kama dakika 5 akiwa na clutch plate mpya. Utengenezaji ukaanza rasmi, baada ya masaa 3, karibia saa 9 na nusu mchana, gari likatengamaa.

Safari ikaanza, kwakweli tulikua tumechelewa sana, kwa wastani safari ya Arusha-Mwanza ni kwamba ukitoka saa 12 alfariji ukichelewa njiani basi saa 12 jioni unakua umefika mwanza.

Dreva alijitahidi kupiga gia, tuliingia mkoa wa Tabora, wilaya ya Nzega, Nzega stendi saa mbili kama na robo usiku. Wakati tunaelekea stendi tuliipita gari ya polisi, Toyota Hilux double cabin, kumbe ilikua ni gari yya RPC. RPC akapiga simu gari ishikwe stendi hapo Nzega kwasababu dereva yuko na mwendo mkali, kaipita gari yake wakati yeye RPC yuko kwenye themanini akutegemea apitwe na basi.

Bana kumbe dere alipoingia stendi, wakashuka kama kuchimba dawa, trafiki polisi wa zamu/sajenti, akamshika, akamuweka chini ya ulinzi, patrol defenda ikafika, ikamchukua mpaka central ya Tabora usiku huo. Abiria tulitangaziwa, chimbeni dawa jamani, chukueni chakula, tukitoka hapa hatusimami popote. ilipopita nusu saa safari haianzi, ndipo abiria mmoja akasema, wakati ameenda haja, ameona dereva kapakiwa kwenye difenda, abiria tukachachamaa.

TUKAENDA WOTE KITUO CHA POLISI HAPO STENDI

Sajenti, dereva yuko wapi? Ameshikwa kwa amri ya RPC na kapelekwa central. Abirira wakamuuliza, tunaendeleaje na safari? Akajibu, dereva mwingine yupo, awapeleke. Abiria wakahoji, dereva mwingine yuko wapi? Na, kwanini umchukkue dereva bila kututaarifu? Inakuaje unafanya kazi katika hali ya ajabu namna hii? Aaaya , tupe dereva uyo wa pili atupeleke. Afande kimya. Abiria, sisi tumetoka Chuga na dereva mmoja na huyo pekee ndiye tunaye.

Kama hoja ni overspeed, mbona gari nyingi zina-overspeed? Abiria wanamhoji sajenti, sajenti kimya. Abiria na connection zetu tuakapiga simu usalama wa taifa, kwa IGP na media kadhaa na kwa RTO mkoa wa Tabora. RTO akaja, alipofika, akakutana na wananchi wenye hasira na waliochoka na safari, baada ya kubanwa kwelikweli, ikabidi awe mpole. Akaomba apige simu awasilaine na wakubwa wake, mwishowe aksema, dereva anakuja. Abiria wakafurahi.

Yapata saa sita na dakika tano usiku, dereva akaletwa na difenda, dereva akitabasamu baada ya airia kumtoa ndani huko ambako alikua ameishawekwa. Safari ikaendelea. Wazee wa PGO ziro Abiria 3

MAFUNZO MAKUU KATIKA SAFARI HIZI ZA MIKOANI NNILIYOJIFUNZA

1. Polisi/wazee wa PGO bado wao hawafanyi kazi kwa weledi, wanachukua sana rushwa, magari flani yanazuiwa na magari flani hayazuiwi.

2. Polisi ndio chanzo cha ajali. Arusha wameruhusu gari itoke stendi wakati ina dereva mmoja peke yake, kitu hiki ni kinyume na sheria, inakuaje Tabora ndio wagundue?

3. Wamiliki wa mabasi, baadhi yenu, hakikisheni mnafanyia service vyombo vyenu. Haiwezekani kama hili la liazi kitamu clutch plate iungue namna ile bila kufahamika, tumetoka tabora saa 6 usiku, kufika shinyanga, gari likapiga pancha, tukapoteza muda tena.

4. Raia, simamia sheria, polisi ni waoga sana mkishindana nao kwa hoja na mkiwa na umoja, lolote lile linawezekana.

MWISHO KABISA

Mungu ni mwema, safari ilimalizika saa 9:45 alfajiri tarehe 6/10/2021 kila abiria akiwa salama salmini.

View attachment 1967536
View attachment 1967568
.

View attachment 1967534
Huo muda wa saa 9 usiku mliofika........Asubuhi yake dereva huyohuyo anarudi nalo Arusha tena
 
  • Nzuri
Reactions: ALT
aisee tafuta kwanza pesa uwe na gari alafu ndiyo ujue makosa ya fine ni yapi na makosa ya lock up ni yapi.

taja hata moja mkuu.

ndio nyinyi mnaosema anayekanyaga zebra anatakiwa apewe onyo aondoke.
mwendo kasi ni jaribio la kuua kama lilivyo hilo hapo juu.
ni hapa bongo tu sababu ya umasikini,wahuni barabarani wanageuzwa kitega uchumi,mpaka makosa serious namna hiyo unatozwa fine ya elfu 30.

kuachwa uendelee kuendesha gari lako zuri ni sababu uko mwenyewe ndani humo,ukibinuka kafie mbali huko utajijua.
 
Aise hujui chochote alaf unaongea Sana.
Uendeshaji wa Njia ya hatari/overspeed kinyume na K/F 42
Adhabu yake chini ya k/f cha 63(2) (b) adhabu yake ni faini au kifungo kisicho pungua miaka miwili.
Kwahiyo ukiona unapigwa faini na kuachiwa siyo kwamba huwezi kukamatwa na kuwekwa lockup unakamatwa vizuri tu na ndani ya masaa 24 unapelekwa mahakamani na unachezea mvua miaka miwili jela ila kama ushahidi upo na hauna shaka ndani yake.
Sheria hapa Tz zinalegezwa sana zikiamua kukazwa kila mtu ataionja jela kuna wengi sana tunafundishana magari bila kibali chochote bila kujua ni kosa kisheria
Aisee polisi wangekuwa wako sawa wangeendelea kumshikilia dereva,
why wamemuachia dereva kama kweli sheria iliwaelekeza kumuweka lock up dereva na kuwaacha abiria na sintofahamu???

Mnatakiwa mjiongeze msisome traffic acts kama makasuku, huyo mkuu wa polisi aliyetoa order angedhibitishaje kuwa dereva alikua kwenye mwendokasi??
 
taja hata moja mkuu.

ndio nyinyi mnaosema anayekanyaga zebra anatakiwa apewe onyo aondoke.
mwendo kasi ni jaribio la kuua kama lilivyo hilo hapo juu.
ni hapa bongo tu sababu ya umasikini,wahuni barabarani wanageuzwa kitega uchumi,mpaka makosa serious namna hiyo unatozwa fine ya elfu 30.

kuachwa uendelee kuendesha gari lako zuri ni sababu uko mwenyewe ndani humo,ukibinuka kafie mbali huko utajijua.
dereva ameachiwa ameendelea na safari kwasababu hakutakiwa kuwekwa lock up full stop.
 
Aisee polisi wangekuwa wako sawa wangeendelea kumshikilia dereva,
why wamemuachia dereva kama kweli sheria iliwaelekeza kumuweka lock up dereva na kuwaacha abiria na sintofahamu???

Mnatakiwa mjiongeze msisome traffic acts kama makasuku, huyo mkuu wa polisi aliyetoa order angedhibitishaje kuwa dereva alikua kwenye mwendokasi??
Mwendokasi inakutia hatiani hata kwa ushahidi wa kimazingira tu na siyo lazima upigwe tochi za wale trafki ilimrad tu umehatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara na abiria uliowabeba unaweza kukamatwa na kupelekwa mahakamani.
Polisi kumuachia huyo dereva haimaanishi kwamba dereva hakua na kosa isipokua inawezekana busara ilitumika.
Polisi kosa lao ni kuruhusu gari kuondoka Stand Arusha bila kuhakikisha gari ina dereva wawili na ingekua na dereva wawili huyo dereva asingeachiwa na kukamatwa kwake haikua uonevu, ajali zinauwa na zinasababishia watu ulemavu wa Tz tuache kushabikia haya mambo ya hatari gari ikiwa mwendo kasi ni hatari kama ilivyo silaha zingine za mauaji.
 
  • Thanks

eti busara ilitumika 🤣 🤣 🤣

Walivyomkamata na kuwaahc aabiraia na sintofahamu ni nini ilitumika???

Huu ni muda muafaka wa jeshi la polisi kuacha kuajiri failures(division 4 na zero) ili kuepukana na upumbavu kama huu.
 
eti busara ilitumika [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]

Walivyomkamata na kuwaahc aabiraia na sintofahamu ni nini ilitumika???

Huu ni muda muafaka wa jeshi la polisi kuacha kuajiri failures(division 4 na zero) ili kuepukana na upumbavu kama huu.
Sasa usiseme kuwa kosa la overspeed ni faini peke yake alaf unakomaa kabisa kumbe hujui
 
  • Thanks
Reactions: ALT
Back
Top Bottom