Mpambano mkali kituo cha Polisi Nzega stendi kati ya Abiria na Polisi

Mpambano mkali kituo cha Polisi Nzega stendi kati ya Abiria na Polisi

Bus kwenda 80 au 85 ni ku over speed? Agizeni basi Buses zenye speed limit ya 50km ph
Kwa hiyo kwenye kibao cha 50 wewe ukienda 85 au 85 siooverspeed?

Aliyeuroga watanzania yapaswa apewe tuzo ya Nobel!
 
  • Thanks
Reactions: ALT
Wanabodi

Natumai mungu ni mwema kwa kila mmoja kwa kupata zawadi ya uhai.

Muhtasari wa habari.

Moja kwa moja kwenye mada. Mnamo tarehe 5/10/2021 nikiwa natoka Arusha kuelekea mwanza na basi la kiazi kitamu ulizuka msuguano mkali kituoni cha polisi Nzega stendi.

Polisi walimshusha dereva kwenye gari kimya kimya wakampandisha kwenye difender hadi kituo cha Polisi central. Abiria baada ya kutomuona dreva, tukaenda kituoni kuhoji, askari wa zamu anasema dereva kasnikwa, kapelekwa central, moto ukawaka, abiria tunamtaka dereva.

Habari kamili.

Safari kutoka arusha ilianza saa 11:57 alfajiri stendi ya mabasi ya kwenda mikoani. Gari baada ya kukaguliwa lilitoka. Baada ya masaa matatu, tulifika stendi ya babati mkoani manyara, trafiki polisi walikagua gari tena, wakakumbusha abiria kufunga mkanda, kama baada ya dakika 20 tangu kutoka stendi ya babati gari likaanza kutoa harufu kana kwamba matairi yanaungua kumbe ni clutch plate inaungua na imeisha. Gari likasimama likashindwa kwenda, abiria tusijue hili wala lile safari imesimama, konda akasema abiria tunaomba mvumilie, dreva ameenda kuchukua maziwa, kumbe ni fiksi, abiria wakamwambiia usitufanye watoto wadogo, gari ni mbovu, clutch plate iimeungua, gia haziingi, hakuna maziwa wala nini. Dereva akomba radhi akasema gari limeharibika.

Ilikua karibu saa 3:45 asubuhi, wakajaribu kutengeneza hadi saa tano kamili, gari likawashinda. Wakapiga simu, fundi akatokea Kateshi, akafika saa sita kasoro kama dakika 5 akiwa na clutch plate mpya. Utengenezaji ukaanza rasmi, baada ya masaa 3, karibia saa 9 na nusu mchana, gari likatengamaa.

Safari ikaanza, kwakweli tulikua tumechelewa sana, kwa wastani safari ya Arusha-Mwanza ni kwamba ukitoka saa 12 alfariji ukichelewa njiani basi saa 12 jioni unakua umefika mwanza.

Dreva alijitahidi kupiga gia, tuliingia mkoa wa Tabora, wilaya ya Nzega, Nzega stendi saa mbili kama na robo usiku. Wakati tunaelekea stendi tuliipita gari ya polisi, Toyota Hilux double cabin, kumbe ilikua ni gari yya RPC. RPC akapiga simu gari ishikwe stendi hapo Nzega kwasababu dereva yuko na mwendo mkali, kaipita gari yake wakati yeye RPC yuko kwenye themanini akutegemea apitwe na basi.

Bana kumbe dere alipoingia stendi, wakashuka kama kuchimba dawa, trafiki polisi wa zamu/sajenti, akamshika, akamuweka chini ya ulinzi, patrol defenda ikafika, ikamchukua mpaka central ya Tabora usiku huo. Abiria tulitangaziwa, chimbeni dawa jamani, chukueni chakula, tukitoka hapa hatusimami popote. ilipopita nusu saa safari haianzi, ndipo abiria mmoja akasema, wakati ameenda haja, ameona dereva kapakiwa kwenye difenda, abiria tukachachamaa.

TUKAENDA WOTE KITUO CHA POLISI HAPO STENDI

Sajenti, dereva yuko wapi? Ameshikwa kwa amri ya RPC na kapelekwa central. Abirira wakamuuliza, tunaendeleaje na safari? Akajibu, dereva mwingine yupo, awapeleke. Abiria wakahoji, dereva mwingine yuko wapi? Na, kwanini umchukkue dereva bila kututaarifu? Inakuaje unafanya kazi katika hali ya ajabu namna hii? Aaaya , tupe dereva uyo wa pili atupeleke. Afande kimya. Abiria, sisi tumetoka Chuga na dereva mmoja na huyo pekee ndiye tunaye.

Kama hoja ni overspeed, mbona gari nyingi zina-overspeed? Abiria wanamhoji sajenti, sajenti kimya. Abiria na connection zetu tuakapiga simu usalama wa taifa, kwa IGP na media kadhaa na kwa RTO mkoa wa Tabora. RTO akaja, alipofika, akakutana na wananchi wenye hasira na waliochoka na safari, baada ya kubanwa kwelikweli, ikabidi awe mpole. Akaomba apige simu awasilaine na wakubwa wake, mwishowe aksema, dereva anakuja. Abiria wakafurahi.

Yapata saa sita na dakika tano usiku, dereva akaletwa na difenda, dereva akitabasamu baada ya airia kumtoa ndani huko ambako alikua ameishawekwa. Safari ikaendelea. Wazee wa PGO ziro Abiria 3

MAFUNZO MAKUU KATIKA SAFARI HIZI ZA MIKOANI NNILIYOJIFUNZA

1. Polisi/wazee wa PGO bado wao hawafanyi kazi kwa weledi, wanachukua sana rushwa, magari flani yanazuiwa na magari flani hayazuiwi.

2. Polisi ndio chanzo cha ajali. Arusha wameruhusu gari itoke stendi wakati ina dereva mmoja peke yake, kitu hiki ni kinyume na sheria, inakuaje Tabora ndio wagundue?

3. Wamiliki wa mabasi, baadhi yenu, hakikisheni mnafanyia service vyombo vyenu. Haiwezekani kama hili la liazi kitamu clutch plate iungue namna ile bila kufahamika, tumetoka tabora saa 6 usiku, kufika shinyanga, gari likapiga pancha, tukapoteza muda tena.

4. Raia, simamia sheria, polisi ni waoga sana mkishindana nao kwa hoja na mkiwa na umoja, lolote lile linawezekana.

MWISHO KABISA

Mungu ni mwema, safari ilimalizika saa 9:45 alfajiri tarehe 6/10/2021 kila abiria akiwa salama salmini.

View attachment 1967536
.


View attachment 1967534
Poleni sana ndugu ALT ,na kongole nyingi zikufikie wewe kwa kuuleta huu uzi hapa na kuwa "expose" hawa wazee wa PGO.
Mungu akubariki sana.
 
  • Thanks
Reactions: ALT
Umeleta ushabiki sana kwenye hii habari sijaona kosa la polisi. Kosa lipo kwenye bus bovu ,mwendo mkali. Hivi mfano hilo basi lingewamwaga si mngelalamikia polisi hawakulizuia Nzega stend. Pia mwenye basi ana makosa safari ndefu inahitaji dereva wawili.

Yaani hapo ni faini juu ya faini
Lakini polisi walitakiwa kuwataarifu abiria kuwa dereva amekamatwa kwa makosa ya barabarani hapo ndio shida ilipoanzia
 
Pumba na upupu mtupu, najua ni umbumbumbu unakusumbua tuu... Ni hivi huyo askari alitakiwa aingie ndani ya Bus na baada ya kuwasalimia na kuwapa pole abiria awajulishe kosa la dereva na kifungu husika na adhabu stahiki. Makosa ya overspeed mengi ni faini na faini ina muda wa kuilipa. Baada ya dereva kuandikiwa makosa yake na faini anaruhusiwa na safari ili abiria karibia 65 waweze kufika makwao. Hicho kilichofanyika siyo ukamataji ni utekaji, kama ilivyo kawaida yao. Hivi ingekuwa huyo abiria mmoja asingeona dereva akitekwa si ina maana wangekaa hapo mpaka asubuhi??
niulize, hapo kwenye kulipa faini. Hivi Ni lazima kulipishwa faini ama askari ana option ya kuamua asiandike faini na kukupeleka mahakamani!?
 
Kumbe ndo maana mwenyekigoda yupo jela daah ufisadi mkubwa
ohh masikini yani mtu ukiwa na gari wewe ni fisadi 🤣 🤣 🤣

Haya mawazo ya kifukara ndiyo yanakufanya unatukanana na makondakta wa daladala kila kukicha.
 
😂😂😂😂si ndo mawazo yako hayo
ohh masikini yani mtu ukiwa na gari wewe ni fisadi 🤣 🤣 🤣

Haya mawazo ya kifukara ndiyo yanakufanya unatukanana na makondakta wa daladala kila kukicha.
 
Back
Top Bottom