Mpambano mkali kituo cha Polisi Nzega stendi kati ya Abiria na Polisi

Mpambano mkali kituo cha Polisi Nzega stendi kati ya Abiria na Polisi

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ila kuwa mfuasi wa gaidi kazi sana,wewe umeniita maskini kisa sina gari,nimekuita tajiri unapanic daahπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
acha mawazo ya kifukara bana umeniaibisha mnoo.

usirudie tena kumuita mtu tajiri eti kisa tu ana gari 🀣 🀣 🀣
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ila kuwa mfuasi wa gaidi kazi sana,wewe umeniita maskini kisa sina gari,nimekuita tajiri unapanic daahπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

ohh masikini nikuambia hapa u-quote maandishi yangu niliyosema wewe ni "masikini" nakununulia kanga za chama doti 20.

Narudia tena acha mawazo ya kifukara, usimuite tena mtu tajiri kisa tu ana gari, leo umeniaibisha mnoo 🀣 🀣 🀣
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚kumbe nawe ni wale wale wanunua kanga za chama. Maskini natafuta hela tajiri mwenye gariπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
ohh masikini nikuambia hapa u-quote maandishi yangu niliyosema wewe ni "masikini" nakununulia kanga za chama doti 20.

Narudia tena acha mawazo ya kifukara, usimuite tena mtu tajiri kisa tu ana gari, leo umeniaibisha mnoo 🀣 🀣 🀣
 
Umeleta ushabiki sana kwenye hii habari sijaona kosa la polisi. Kosa lipo kwenye bus bovu ,mwendo mkali. Hivi mfano hilo basi lingewamwaga si mngelalamikia polisi hawakulizuia Nzega stend. Pia mwenye basi ana makosa safari ndefu inahitaji dereva wawili.

Yaani hapo ni faini juu ya faini
Habari haijaandikwa kishabiki, imeandikwa kitaalamu, ila wewe ndo Mshabiki uliyeumia, kwenye Hitimisho mtoa Masa kashauri na kutoa mapendekezo yote...

Hata Kama inauma Vumilia tu.
 
Wanabodi

Natumai mungu ni mwema kwa kila mmoja kwa kupata zawadi ya uhai.

Muhtasari wa habari.

Moja kwa moja kwenye mada. Mnamo tarehe 5/10/2021 nikiwa natoka Arusha kuelekea mwanza na basi la kiazi kitamu ulizuka msuguano mkali kituoni cha polisi Nzega stendi.

Polisi walimshusha dereva kwenye gari kimya kimya wakampandisha kwenye difender hadi kituo cha Polisi central. Abiria baada ya kutomuona dreva, tukaenda kituoni kuhoji, askari wa zamu anasema dereva kasnikwa, kapelekwa central, moto ukawaka, abiria tunamtaka dereva.

Habari kamili.

Safari kutoka arusha ilianza saa 11:57 alfajiri stendi ya mabasi ya kwenda mikoani. Gari baada ya kukaguliwa lilitoka. Baada ya masaa matatu, tulifika stendi ya babati mkoani manyara, trafiki polisi walikagua gari tena, wakakumbusha abiria kufunga mkanda, kama baada ya dakika 20 tangu kutoka stendi ya babati gari likaanza kutoa harufu kana kwamba matairi yanaungua kumbe ni clutch plate inaungua na imeisha. Gari likasimama likashindwa kwenda, abiria tusijue hili wala lile safari imesimama, konda akasema abiria tunaomba mvumilie, dreva ameenda kuchukua maziwa, kumbe ni fiksi, abiria wakamwambiia usitufanye watoto wadogo, gari ni mbovu, clutch plate iimeungua, gia haziingi, hakuna maziwa wala nini. Dereva akomba radhi akasema gari limeharibika.

Ilikua karibu saa 3:45 asubuhi, wakajaribu kutengeneza hadi saa tano kamili, gari likawashinda. Wakapiga simu, fundi akatokea Kateshi, akafika saa sita kasoro kama dakika 5 akiwa na clutch plate mpya. Utengenezaji ukaanza rasmi, baada ya masaa 3, karibia saa 9 na nusu mchana, gari likatengamaa.

Safari ikaanza, kwakweli tulikua tumechelewa sana, kwa wastani safari ya Arusha-Mwanza ni kwamba ukitoka saa 12 alfariji ukichelewa njiani basi saa 12 jioni unakua umefika mwanza.

Dreva alijitahidi kupiga gia, tuliingia mkoa wa Tabora, wilaya ya Nzega, Nzega stendi saa mbili kama na robo usiku. Wakati tunaelekea stendi tuliipita gari ya polisi, Toyota Hilux double cabin, kumbe ilikua ni gari yya RPC. RPC akapiga simu gari ishikwe stendi hapo Nzega kwasababu dereva yuko na mwendo mkali, kaipita gari yake wakati yeye RPC yuko kwenye themanini akutegemea apitwe na basi.

Bana kumbe dere alipoingia stendi, wakashuka kama kuchimba dawa, trafiki polisi wa zamu/sajenti, akamshika, akamuweka chini ya ulinzi, patrol defenda ikafika, ikamchukua mpaka central ya Tabora usiku huo. Abiria tulitangaziwa, chimbeni dawa jamani, chukueni chakula, tukitoka hapa hatusimami popote. ilipopita nusu saa safari haianzi, ndipo abiria mmoja akasema, wakati ameenda haja, ameona dereva kapakiwa kwenye difenda, abiria tukachachamaa.

TUKAENDA WOTE KITUO CHA POLISI HAPO STENDI

Sajenti, dereva yuko wapi? Ameshikwa kwa amri ya RPC na kapelekwa central. Abirira wakamuuliza, tunaendeleaje na safari? Akajibu, dereva mwingine yupo, awapeleke. Abiria wakahoji, dereva mwingine yuko wapi? Na, kwanini umchukkue dereva bila kututaarifu? Inakuaje unafanya kazi katika hali ya ajabu namna hii? Aaaya , tupe dereva uyo wa pili atupeleke. Afande kimya. Abiria, sisi tumetoka Chuga na dereva mmoja na huyo pekee ndiye tunaye.

Kama hoja ni overspeed, mbona gari nyingi zina-overspeed? Abiria wanamhoji sajenti, sajenti kimya. Abiria na connection zetu tuakapiga simu usalama wa taifa, kwa IGP na media kadhaa na kwa RTO mkoa wa Tabora. RTO akaja, alipofika, akakutana na wananchi wenye hasira na waliochoka na safari, baada ya kubanwa kwelikweli, ikabidi awe mpole. Akaomba apige simu awasilaine na wakubwa wake, mwishowe aksema, dereva anakuja. Abiria wakafurahi.

Yapata saa sita na dakika tano usiku, dereva akaletwa na difenda, dereva akitabasamu baada ya airia kumtoa ndani huko ambako alikua ameishawekwa. Safari ikaendelea. Wazee wa PGO ziro Abiria 3

MAFUNZO MAKUU KATIKA SAFARI HIZI ZA MIKOANI NNILIYOJIFUNZA

1. Polisi/wazee wa PGO bado wao hawafanyi kazi kwa weledi, wanachukua sana rushwa, magari flani yanazuiwa na magari flani hayazuiwi.

2. Polisi ndio chanzo cha ajali. Arusha wameruhusu gari itoke stendi wakati ina dereva mmoja peke yake, kitu hiki ni kinyume na sheria, inakuaje Tabora ndio wagundue?

3. Wamiliki wa mabasi, baadhi yenu, hakikisheni mnafanyia service vyombo vyenu. Haiwezekani kama hili la liazi kitamu clutch plate iungue namna ile bila kufahamika, tumetoka tabora saa 6 usiku, kufika shinyanga, gari likapiga pancha, tukapoteza muda tena.

4. Raia, simamia sheria, polisi ni waoga sana mkishindana nao kwa hoja na mkiwa na umoja, lolote lile linawezekana.

MWISHO KABISA

Mungu ni mwema, safari ilimalizika saa 9:45 alfajiri tarehe 6/10/2021 kila abiria akiwa salama salmini.

View attachment 1967536
.


View attachment 1967534
Polisi wana haki ya kutimiza wajibu wao, lakini wakumbuke na usemi wa Samia, sheria na utu. Unamchukua Dereva wa gari lililotoka masafa, abiria waliomo hali zao huna habari! Kama gari ni bovu polisi ina wajibu kumtaka mmliki kuleta au kukodi gari lingine safari iendelee. Kama dereva mnamhitaji , mmiliki alete dereva mwingine. Mbona mnanyang'anya bodaboda funguo na kuendesha pikipiki zao, leseni ya kuendesha mabasi hamna?
 
Haha kumbe ulikuwa kwenye kiazi kitamu mdau mie nilikuwa kwenye Dar lux wale askari wapuuzi sana aiseee hasa yule mzee aliyekuwepo kituoni hajui lolote
Ndio mdau...ile siku sitoisahau maishani kwakweli. DAR LUX / KIAZI KITAMU wakipambania madereva wao ili safari iendelee kwa mujibu wa PGO
 
Umeleta ushabiki sana kwenye hii habari sijaona kosa la polisi. Kosa lipo kwenye bus bovu ,mwendo mkali. Hivi mfano hilo basi lingewamwaga si mngelalamikia polisi hawakulizuia Nzega stend. Pia mwenye basi ana makosa safari ndefu inahitaji dereva wawili.

Yaani hapo ni faini juu ya faini

Unaweza kuwa sahihi kabisa kwa mujibu wa katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa tanzania. Ila, msikilize aliyekuwa amemshika dereva wa gari pale alipomrudisha baada ya raia kumhoji.
 
Siku mpiga mzinga kwa sababu ya oversped na mkakatika vichwa mje tena hapa kuandika gazeti la namna mlivyomshabikia dreva kuwafikisha kuzimu!

Laiti ungekua umeelewa nilichokimaanisha, husinge tamatisha hivi. Anyway, tunategemeana. Bila msuguano hakuna moto.
 
Walipeta kwa sababu ilikuwa usiku na mmeanzisha vurugu. Siku hizi ni sheria, Safari ndefu lazima madereva wawili, full stop!

Binafsi, niliona walitambua kosa kubwa walilofanya arusha, waliruhusuje gari litoke ilihali dereva ni mmoja? Ujue hua wanasaini vile vitabu vyao vya magari kabla hayajatoka. Very simple, ni kwamba walifunika kosa lao la kwanza kwa kufanya kosa la pili. Ndio maana, nimeleta hapa ili tujifunze, iwe case study ili yasitokee mambo haya.
 
Abiria ni watu wanafiki sana likienda kuanguka au kugonga na kusababishia watu ulemavu/kifo utaskia dereva alikua nakimbia sana na polisi walimruhusu
Huo haukua ushindi ila waliacha kwasababu mmeshakua radhi kufa

I second you 100%
 
"Hapa si Polisi usalama wa raia? Tufungulie tuingie tulale humo humo"alisikika jaluo mmoja🀣

Kimsingi sauti hiyohiyo iliskika wakati gari limeharibika babati ikisema " abiria , tusubiri kidogo, kuna mtu ameenda kumchukulia dereva maziwa", kumbe, ilikua fix
 
Mbona naona kama police walikua sahihi?

Walikiri kabisa walikuwa sahihi, na mimi niliona. Sema hatuwezi kutatua kila kitu kwa sheria, hekima ni mhimu. Unamchukua dereva, unawaacha abiria bila kuwataarifu, wana njaa, wamechoka na kibaya zaidi, hao ndio wanakulipa. inabidi ufikirie pande zote, utoe maamuzi sahihi.
 
dereva kiazi,abiria viazi mbatata.

yaani umetafakari ukaona uje na huu ujinga wako hapa!!!
wazee wa PGO hawanaga cha kupoteza mdogo wangu,ni kama mwenye kampuni ya kamari,anakula kwa aliyepoteza na aliyepata.

hivi huyo jamaa yenu angeenda kuwazibua kwenye roli ungekumbuka hata PGO hapa jf kweli!!!

Lichukue kama case study, take it positive, kuna kitu cha kujifunza hapa. Tuvumiliane.
 
Back
Top Bottom