Mpangaji agoma kuhama baada ya mkataba kuisha. Nitumie mbinu gani kumtoa kwenye nyumba yangu?

Kama hiyo pesa ipo kwenye mkataba na yeye alisaini ni kweli ako na makosa ila kama ni makubalino ya mdomoni tu hilo litakua ni jambo lingine.

Kama hautaki mambo yawe mengi na wewe ni mfanya biashara unaweza kurudisha hiyo pesa ili uendelee na biashara zako, maana mnapotezeana muda tu hapo.

Vinginevyo nenda kwenye chama cha wapangishaji uone wanakushauri vipi kwa kesi kama hiyo.
 
Wabongo wamezoea kulipa kodi ya miezi sita!! Wale wa kulipa kodi ya mwaka mmoja ni wachache sana.
 
Asante sana umenisaidia kuandika aisee
 
Kwq uelewa wangu mpangaji kama kodi imeisha inatakiwa umpe nosti ya miezi 3 ambayo atakaa free baada ya hapo ndio anatakiwa aondoke hio deposit ya pesa ambayo mnawekeana kama Iko kwenye mkataba na yeye alikubali kuwa na jambo kama Hilo na akasaini huo mkataba basi haki Iko kwako
 
Cha kufanya fanya hivi! Nunua kufuli la elfu hamsini kubwa na imara,kisha nenda kwenye nyumba yako,kwa vile ameweka kufuli lake,we kaongezee la kwako,siku tu akirudi akutane na kufuli lako na itakuwa mwanzo wa kukutafuta. Kuna bwana mmoja nilimpangisha tena malipo ya kawaida kila mwezi, amelipa vizuri kama miezi 4 tu akaanza kukwepa, hajalipa kama miezi miwili, akaondoka,akaacha vitu vyake ndani, nlichokifanya ni kama nilivyoeleza hapo juu! Siku aliporudi akanitafuta nikampa masharti eidha ahame au alipe aendelee kuishi. Akalipa zote akaendelea kuishi kwenye nyumba yangu. SIMPLE LIKE THAT.
 
Hicho kipengele cha security deposit ya mwezi mmoja ni cha kinyonyaji kwa mpangaji. Inaweza kuwa fair endapo kuna kitu tangible mpangaji ameharibu, akikatwa ni sawa, ila kama hakijaharibika kitu, ni rangi na vitu vya kawaida, huo mkataba ni wa kinyonyaji.

Kwa hiyo kodi unayopewa haihusiki na matengenezo ya nyumba yako?
 
Mwite mjumbe na mwenyekiti Kisha andikisha vitu vyake tafuta store yoyote ile yeye ataenda kugomboa vitu vyake huko
 
Sasa hayo ya status yake ya usingle maza vinausiano gani na malalamiko yako?
 
Pana jamaa mmoja alikua anasumbuliwa sana na wapangaji wake huko Mbeya ni kama walikua wanasimuliana jinsi ya kumukimbia mwenye nyumba baadae mwenye nyumba kipindi cha masika akaamua kutoa bati lote la nyumba yake maana aliwapa barua ya matengenezo muda mrefu na hawakuzingatia yule Mzee alikua mafia sana walipotoka akarudisha bati lingine na maisha yakaendelea..
 
Wenye nyumba na madarali ni kama mjomba na shangazi wamepishana jinsia ila kwa vile mjomba ni mama ana tofauti na shangazi.

Wenye nyumba ujumbe kwenu
 
Experience yangu nao especially wale wanaojidai wafanyabiashara ( kwenda Dubai au China ) wanapata changamoto sana za kodi za pango!
"Wanaojidai wafanyabiashara (kwenye Dubai au china" unamaanisha Nini?
 
kwa hayo maelezo yako uliyoyatoa mpangaji hana tatizo ila wewe mwenye nyumba ndio mwenye matatizo,unatumia unyonge wa wapangaji kuwarubuni,unaongelea habari za matengenezo ya nyumba yeye mpangaji inamuhusu nini ikiwa wewe ndio mmiliki.
Kama unakiri kweli alilipia deposit ni sababu ipi inayokufanya usimrudishie pesa yake?si ungemlipa tu pesa yake aende,tamaa yako itakusababishia matatizo makubwa hapo umekutana na mpangaji anayezijua sheria sasa amekuchoka anataka kukupa somo ili ujifunze na kuacha jeuri kwa wapangaji wako.
 
Unaweza kutaja au kupiga mahesabu ya uharibifu alioufanya kwenye chumba anachoishi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…