Mpangaji agoma kuhama baada ya mkataba kuisha. Nitumie mbinu gani kumtoa kwenye nyumba yangu?

Mpangaji agoma kuhama baada ya mkataba kuisha. Nitumie mbinu gani kumtoa kwenye nyumba yangu?

Nenda kwa mtendaji ukiwa na huo mkataba,,, ukiona hakuna ushirikiano, nenda police,,, wape kitu kidogo like 50k, waje hapo, mvunje nyumba, mtoe vitu vyote vivilvyopo na viandikishwe chini ya uangalizi wa police ! Simple
 
Usimshauri kufanya hivi hapo ndio unazidi kumpoteza.
Baadae kesi huwa inageuka ikifika mahakamani kisha hao watendaji wanakuruka,nilishawahi kukutana na kesi za hivi.
 
Ondoa mabati mpangaji atakimbia mwenyewe.
Huo ushauri mbaya saana. Jirani yangu hapa kala miezi 6 jela baada ya kuezua mabati juu vyumba alivyokuwa kampangisha jamaa na familia yake. Baada ya kuezua mvua ikanyesha siku mbili mfululizo TV, na mali zote za jamaa ziliharibika plus watoto kuugua pneumonia. Mwenye nyumba pamoja na kufungwa miezi sita jela ametakiwa amlipe jamaa fidia ya milioni 4.
 
Wana BODI naomba ushauri. Wapangaji wangu wote naingia nao mkataba wa miezi sita. Ambao ni renewable .Katika mkataba kuna kipengele cha security deposit Sawa na kodi ya mwezi ambayo hutumika kutengeneza nyumba mkataba ukiisha.

Mpangaji wangu mmoja single mother mkataba wake ulikwisha mwezi January mwaka huu lakini amegoma kuhama akidai arudishiwe deposit yake ndio ahame kabla nyumba haijakaguliwa ; lakini amekwisha kaa hiyo nyumba mwaka mmoja na nusu na nyumba inahitajika matengenezo.

Amegoma kuondoka na sasa amefunga nyumba na kuacha vitu vyake ndani na kutoweka na funguo!

Ameisha kaa zaidi ya mwezi bila kulipa kodi na hata bill ya maji hajalipa! Nimekwenda serikali ya mtaa kutoa taarifa nao hawana msaada.

Nitumie mbinu gani kumtoa kwenye nyumba yangu?
Mpe anachotaka Kwa maandishi mbele ya mashahidi ahame
 
Mpe anachotaka Kwa maandishi mbele ya mashahidi ahame
Kwanini nifanye hivyo? Yeye mkataba wake umekwisha hivyo kuendelea kukaa ni trespassing!! Kama ana dai afungue kesi ya madai mahakamani.
 
Mkuu huo ni mtego amekuwekea ukikurupuka tu mkienda mahakamani atakushinda na fidia utamlipa,nimeshawahi kukutana na hizi kesi mara nyingi.
Si kila mahali unataka kutumia nguvu sehemu zingine busara inahitajika.
Hebu nieleze mtego uko wapi na hizo kesi ulizokutana nazo wali Shinda kwa vipi? Busara hutumika kwa wenye busara na sio kwa wahuni!
 
Mwenye nyumba ana kaushamba fulani ivi au kwa kutokuelewa biashara, sasa kulikua na haja gani ya kuweka hio security deposit wakati kodi unalipwa au kama unaona hio kodi haitoshi pamoja na matengenezo basi ungeongeza (jumlisha) hio deposit kwenye kodi wala mpangaji asingejua maana hivo ulivo zitenga inaonekana kama unyonyaji.
 
Wana BODI naomba ushauri. Wapangaji wangu wote naingia nao mkataba wa miezi sita. Ambao ni renewable .

Katika mkataba kuna kipengele cha security deposit Sawa na kodi ya mwezi ambayo hutumika kutengeneza nyumba mkataba ukiisha.

Mpangaji wangu mmoja single mother mkataba wake ulikwisha mwezi January mwaka huu lakini amegoma kuhama akidai arudishiwe deposit yake ndio ahame kabla nyumba haijakaguliwa ; lakini amekwisha kaa hiyo nyumba mwaka mmoja na nusu na nyumba inahitajika matengenezo.

Amegoma kuondoka na sasa amefunga nyumba na kuacha vitu vyake ndani na kutoweka na funguo!

Ameisha kaa zaidi ya mwezi bila kulipa kodi na hata bill ya maji hajalipa! Nimekwenda serikali ya mtaa kutoa taarifa nao hawana msaada.

Nitumie mbinu gani kumtoa kwenye nyumba yangu?
Ndoo maana wajanja wanawekeza kwenye bonds na utt amis ili kuepuka kero ndogondogo kama hizi.
 
Unaweza kutaja au kupiga mahesabu ya uharibifu alioufanya kwenye chumba anachoishi?
Nimekwisha fanya mahesabu na yeye kumjulisha ; in fact gharama za matengenezo ni kubwa kuliko deposit yake! Hivyo anadaiwa pamoja na kodi ya nyumba kwa muda wote anaondelea kukaa na funguo!
 
Anza mjumbe pili kata baraza la ardhi eatakupa go ahead to court huyo ni mvamizi kisheria ila fatal hzi taratibu usipigishane na yy wala usiende polisi
Mimi Nataka atoe vyombo vyake kwenye nyumba yangu hivyo polisi watahusika! Kwanini nisiende polisi ? Una sababu gani kusema hivyo!
 
Pana jamaa mmoja alikua anasumbuliwa sana na wapangaji wake huko Mbeya ni kama walikua wanasimuliana jinsi ya kumiimbia mwenye nyumba baadae mwenye nyumba kipindi cha masika akaamua kutoa bati lote la nyumba yake maana aliwapa barua ya matengenezo muda mrefu na hawakuzingatia yule Mzee alikua mafia sana walipotoka akarudisha bati lingine na maisha yakaendelea..
Adhabu yotehiyo ya nini.

Kuna mzee kopindi cha magu. Aliwaambia wapangaji wanangu hali ni ngumu...kila mmoja wenu azingatie mkataba. Ila kama unatatizo niambie usikae kimya.

Kuna binti alimwambia kama huna ukipata utanipa alikaa bure kwa muda na baasae akampa yule mzee kama milioni kama asante.

Wenye nyumba tuishi kwa upendo.wapangaji wanashukran sana wakitendewa ubinadamu
 
Usimshauri kufanya hivi hapo ndio unazidi kumpoteza.
Baadae kesi huwa inageuka ikifika mahakamani kisha hao watendaji wanakuruka,nilishawahi kukutana na kesi za hivi.
Mtendaji ataruka vipi wakati kutakuwepo na Mjumbe na Polisi?
 
Kama kipengele hicho Kiko kwenye mkataba na kikawa express kwamba hiyo pesa ni non refundable, kinambana mteja.

Cha maana Sasa kafungue shauri, Ili udai Kodi, usumbufu, amri ya vacation.
Wapangaji wengine, kama ilivyo kwa wapangishaji, ni wasumbufu na wakorofi
 
Back
Top Bottom