Ikiwa mkataba wako ulipitia kwenye mikono ya kisheria na kutiwa balaka Zote, harafu mteja wako wa nyumba/mpangaji wako aliupitia mkataba akaridhia akiwa na akili timamu akamwaga saini yake kwamba amekubaliana na masharit yaliyowekwa, basi Fata mkondo ule ule wa kisheria hupaswi kutumia nguvu anaweza aka kutengeneza hata kesi, ukivunja kufuri atakuja kudai ametibiwa hata fedha, mshirikishe mwanasheria wako nadhani kwa taaluma zao zipo mbinu huwa wanatumia hata polisi huwa wanashirikishwa kuhamisha,, ingawa unapotaka kumtoa mpangaji wako inabidi umuandalie notes ya miez 3 kabla ya kuhama kwake hapo Kuna kumpatia muda wa yeye kujipanga na kutafuta nyumba nyingine,, sas ukimtoa na ukichukulia hajapata hifadhi unategemea atakwenda wapi? Unaweza kuta kwa muda huu Hana fedha maisha yetu ni siri kubwa,, unaonaje ukibeba utu Bila kujari Sana changamoto zake au changamoto unazopitia? Kitendo cha kutafuta ushauri ni ishara tosha busara unazo,, kama ikikupendeza mbebe kwa utu sisi binadamu hujui kwa sas anapitia changamoto gani, miongoni Mwa matendo ya huruma ni kama maamuzi yako kwa sasa! Inawezekana uliwahi pitia nyumba za kupanga ktk maombi yako kwenye mafanikio uliapa hautokuja kuwafanyia wengine kama ulivyo fanyika kipindi upo nyumba za kupanga,, au na wew ulinyanyasika na wewe unataka kulipa visasi? Naziona busara zako,, ombi langu usitoe au kufanya maamuzi ukiwa na hasira au kushinikizwa ingawa ni haki yako na tupo kwenye mwezi mtukufu na kwaresma beba utu njia ya mafanikio ni ngumu!