Nchi za kibeberu na vibaraka wao wana tabia ya kuwazushia viongozi wanamapinduzi ubaya waonekane wabaya kama shetani.
Walipofanikiwa kumpindua Kwame Nkurumah wa Ghana walimzushia uongo mwingi hadi ikawa kisiasa ghana huwezi kufanikiwa kwa kuunga mkono siasa na sera za Nkrumah. Kutokana na propaganda za magharibi ikawa kama aibu mtu kuunga mkuno sera za ukombozi afrika na uchumi wa kijamaa. Waghana hadi leo hawampi nkurumah anayeheshimika Afrika nzima heshima anayostahili. Uwanja wa ndege wa kimataifa accra hadi leo unabeba jina la kotoko mtu aliyempindua Nkrumah.
Hata nchini guenea ni hivi karibuni tu kumeanza wimbi kuwaelimisha vijana na taifa Sekou Toure alikua kiongozi wa namna gani kwa waguenea na Afrika. Huyu naye alikua mwanamapinduzi ila ubeberu wamemchafua ili waguenea wasifuate mawazo yake.
Kwa nchi yetu ni tofauti kutokana na umoja na mwamko mzuri wa kisiasa wa wananchi. Licha ya kazi kubwa ya wapinga maendeleo wakiongozwa na ubeberu wameshindwa kumchafua Nyerere. Watanzania wanamkumbuka na kutaka dira yake ifuatwe. Hakuna mwanasiasa anaweza kufanikiwa tanzania kwa kumchafua Nyerere.
Tuliona baadhi ya viongozi wa Chadema wakitumika kuchafua jina na heshima ya nyerere hadi bungeni mmojawapo akiwa antipass lissu. Baada ya kuona wanajichafua kwa kujaribu kumchafua Nyerere wakageuza mbinu. Sasa wanajidai kumnukulu kila wakati nyerere ila kwa kupotosha kauli zake.
Magufuli amelinganishwa na nyerere kwa kutetea kwa nguvu maslahi ya umma kwenye uongozi wake. Tangu aitwe na mola wake tumeshuhudia furaha kwa wapinga maendeleo. Wamediriki hadi kumsifia mama kama mwokozi wa taifa dhidi ya uongozi uliyopita wa Magufuli. Juzi tu tumemsikia askofu mmoja akimtaka mama kutibu majeraha taifa.
Wanamapinduzi tunajua wenye majeraha ya magufuli ni fisadi na wazembe. Wale waliyojaribu kuiba mali au mashirika ya umma, wale waliyokua wamejimilikisha kinyemela mali za chama chao cha CCM, wale waliyokua wanashirikiana na barrick kuona madini ya nchi yanaibiwa makontena na makontena kwa kupewa ujira.
Sasa anatokea askofu eti mama ponya majeraha. Majeraha ya fisadi. Ina maana awarejeshe kwenye kudhulumu umma.
Tunamtahadharisha mama awe macho kukumbatiwa na watu waovu ambao wanategemea kuibia umma na kujitajirisha binafsi huku umma wa wananchi ukiendelea kufukarika.
Ni jambo la kutia moyo kuona jinsi wananchi wa tanzania wanavyomkumbuka magufuli. Ni hatari kwa kiongozi yeyote kutaka kufuata sera za kuwanufaisha wachache kwa gharama ya umma. Kimsingi CCM ni chama cha kulinda na kuendeleza maslahi ya umma. Wakifanya tofauti watapigwa chini.
Nikisikia mtu anamlinganisha Jiwe na Nyerere,napata kichefuchefu,nataka kutapika,Kitu limeongoza kwa miaka mitano,lakini,limeua,limebagua watu kikabila,limeharibu biashara za watu,
Kitu lilifikia kutoa hotuba kwenye vyombo vya umma kwa kutumia lugha ya kabila lake!!!!?kisukuma!!
Sasa hebu fikiria lingeongoza kwa miaka 10 ingekuwaje.
Without fear of contradiction,Jiwe alikuwa shetani,tatizo,kikwazo na bahati mbaya sana kwa nchi yetu,kwa muda aliokuwepo ameharibu nchi kabisa.
Nyie mnaomlinganisha na Nyerere,Nyerere alikuwa Mwalimu tu,lakini alikuwa na uwezo wa kuchambua mambo ya Dunia kwa ufasaha,alizimidu Lugha za kimataifa na kiswahili vzr.
Lile jiwe lenu,na PHD yake ya kimagumashi,hata kiswahili lilikuwa haliwezi kuongea vzr,Kizungu ndio kabisaa,
Wazungu mnawaita mabeberu lakini ndio wanaowaingizia pesa nyingi kupitia utalii.
Raisi wa Kenya,amealikwa Whitehouse US,jiwe angeweza kwenda kuongea na Raisi wa Dunia?!!yeye alikuwa anaweza kufokea mawaziri wake basi.
We are better off without that kind of personality