Kumlinganisha Nyerere na Magufuli, ni sawa na kulinganisha mlima Everest na tuta la viazi. Labda humfahamu Nyerere. Tafuta CV yake uisome.
Magufuli na Nyerere wanafanana kwenye mambo mawili tu - wote ni binadamu, na wote wamefariki, japo hisia ya vifo vyao kwa umma zilikuwa tofauti sana. Wakati Mwalimu, kifo chake kilileta simanzi kwa kila mtu, kifo cha Magufuli, kwa baadhi kiiwapa unafuu. Waliobambikiwa kesi za uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na madawa ya kulevua, waliweza kuachiwa. Waliokuwa na hofu ya kutekwa, kuuawa au kupotezwa, wana uhakika wa usalama wao kwa kiasi kikubwa, wasiojulikana hawasikiki sana kama wakati wa utawala wa Magufuli. Wafanyabiashara walioamua kuhama Tanzania kutokana na kunyamg'anywa pesa zao halali na Magufuli, wameanza kurudi na kufanya uwekezaji.
Ukiwatazama hawa wawili:
Mmoja ni tunda la Roho Mtakatifa maana ndani yake kulikuwa na Roho wa Mungu.
Mmoja alikuwa wakala wa shetani. Ndani yake iliishi Roho ya uharibifu, roho ya shetani ambayo kazi kubwa ilikiwa ni kuwatesa, kuwaua, kuwapoteza na kuwahadaa Watanzania kwa namna ya ajabu, sawa na alivyo ibilisi ambaye ni mfalme wa hila na uwongo.