Mpasuko mkubwa kwenye Baraza la Mawaziri kisa kuuzwa kwa Bandari

Nimejifunza kitu kipya kwa hili: barazd la mawaziri halikushirikishwa kwenye uamuzi. Swali linakuja: kwanini? Kwanini huu mkataba umefanywa kwa siri namna hii? Umekuja na points muhimu sana mkuu:.
Huu ndiyo ukweli na ndiyo maana wameweka mgomo baridi hutawaona kwenye majukwaa wakishabikia wizi wa nchi yao
 
Hili sasa ndilo ombi letu wabaki papo hapo wasikubali kugeuka jiwe
 
Tutafika tu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kwetu hatuna chembe ya khofu kwa hilo
 
Tafuta kazi nyingine, hii haitokusaidia
 
Kuna umafia wa kutisha unaendelea
 
Kwa hoja yako hii ina maana lawama zote kuhusiana na mkataba wa uporaji bandari za Tanganyika, zinatakiwa kumwangukia Samia kwa sababu ndiye mwenye maamuzi ya mwisho juu ya jambo lolote liwe jema au baya.

Kwa hiyo kwenye mkataba huu wa hovyo wa bandari, unataka kusema wa kulaumiwa ni Rais Samia.
 
Kwenye uovu, ni vigumu sana watu wote mkubaliane. Lazima wengine dhamira zao zitakataa, hata kama watalazimishwa na mazingira yao ya kazi.
Kabisa kushindana na Muumba lazima baadhi wajitenge kwa khofu ya Mungu
 
Matumizi mabaya ya neno 'Mpasuko' ukihusiana na waCCM. Wote wanaimba wimbo mmoja wakisindikizwa na wapiga makofi na vigelegele(machawa)
[emoji2] [emoji3] [emoji1] [emoji16] [emoji1787] [emoji23] [emoji2] [emoji3] [emoji1] [emoji16]
 
Unajuaje kama hawautetei huo mkataba?, umeshawahi kukaa nao ukawahoji mmoja mmoja?, ndio umbea wenyewe na upotoshaji ambayo ni sifa ya huu uzi.
Njia rahisi ni kubeza kifungu kwa kifungu siyo kupindua mada na kuwa ya mleta mada wa kuhojiwa.

Labda turudi kwenye misingi ya uchambuzi hatuwezi kwenda kienyeji enyeji tu
 
Mtumwa mtumwa tu kazoea kutumikia! hata akikaa kwenye viti vya wa falme anajiona hatoshi kwa kuwa nafsini kwake kuna utumwa! hivyo humpa kifaacho bwana wake na yeye kuendelea kula makombo yatokayo kwa bwana wake!
 
Huna akili, hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza unga mkono Ccm, lakini pamoja na hilo hatutaki habari za kuungaunga JF.
Habari za kuungwa ungwa ndo zikoje eti ndugu Dr Matola PhD?
Kwanza Mama Samia kutokwenda Urusi binafsi nimefurahi, Rais wetu hawezi kukutana na muuwaji, Kwahiyo kumpeleka Pm ni sahihi kabisa.
Unajua umeandika nini hapo☝️☝️☝️?

Labda hujui, nitakuambia..

Kwamba kitendo cha kutuma mwakilishi tu maana yake Madam President Samia Suluhu Hassan is there sitting with whom you call, the killer !

Au hujui maana ya "to represent?". Aaah, ndiyo maana unarusha matusi hovyo ndugu yangu Dr Matola PhD..!
Kwa bahati Mbaya wengi hamjui majukumu ya makamu wa Rais basi tuwasamehe bure tu.
Nadhani badala ya "KUTUSAMEHE" kwa kutojua kwetu, na nadhani muungwana huwajulisha wasiojua ili nao wajue anachojua yeye

Kwa hiyo, hebu tuambie ni yepi kweli majukumu ya VP maana tunayoyajua sisi pengine si hayo ambayo wewe mwenzetu unayajua. Pls, share with us...!
Hakuna jambo lolote kubwa kwenye nchi lisilopita kwenye baraza la mawaziri.
Una uhakika?

Let's assume, Yes...... Hakuna.

Lakini ujue kuwa kwa mfumo wa kikatiba na kiutawala wa nchi yetu, cabinet haiwezi kumzuia Rais a.k.a Mungu mtu kufanya lolote bila kujali hiyo the so called cabinet inaridhia ama la..!!

Hapa nina maana kuwa assumption ya mleta hoja iko sahihi na wewe unnecessarily and ignorantly unajaribu kupambana na reality...!
Ni mtu asiyekuwa na akili tu ndio hajui nguvu za Mwenyekiti wa Ccm kwenye vikao vyao, Mwenyekiti wa Ccm angekuwa hana "VETO" basi Lowasa angekuwa Rais wa Tanzania.
Hili bila shaka ni la kwenu huko CCM. It's irrelevant here..
Na hili ndilo tatizo kubwa la nchi hii. Na ndiyo chanzo cha matatizo yote ya nchi hii likiwemo hili tunaloendelea nalo sasa la DP WORLD na bandari zetu..

Kwa hiyo, si jambo la kujivunia ama kujitapa nalo. Huu ni ugonjwa hatari. Unapaswa kutafutiwa tiba ya kikatiba haraka ili kuwezesha principle ya checks & balance of powers kufanya kazi sawasawa..!
Kama Ccm wanaweza kumfukuza uanachama mtoto wa Karume hakuna mtu mwingine yeyote wa kuleta fyokofyoko kwenye vikao vya chama.
Hii maana yake nini kwani?

Is it relevant with what we have on the table..?
 
VP Dr Mpango yupo kimya kabisa katika hili..
Ila Mzee wa kushupaza shingo PM kama kawa ngoma yoyote ya serikali yee anaicheza tu.
 
Mwarabu ana teknolojia ambayo sisi hatuna. Kumbuka bandari sita za China zimemkodisha.

Siasa nyingi za kijinga ndio sifa ya utanzania wa leo hii, hakuna mantiki zaidi ya kudharau ambacho mtu hana uelewa nacho.
Mwarabu hajawahi kumiliki tekinolojia mwenzetu kama ni ngumbalu ni vyema ukatujuza tushushe darasa hili kwa kina zaidi.

Pia ujue watendaji karibu wote wa ngazi za juu ni waingereza na mikopo kaichukua Benki za Marekani na wala hatumii hela yake.

Kwa kifupi tu, mwarabu anatumika kama ule wakati wa utumwa.

Hii mikataba tuliyoisaini anaenda kuikabidhi benki za mabeberu ambao wanampa mikopo ya riba kubwa sasa hivi ni 10.8% hailipiki.

Baadaye akishindwa mabenki ya mabeberu yanauza hii mikataba kwa wawekezaji wengine sisi hatuna chochote tunapata.

Angalia NBC ilivyobadilisha umiliki na sisi tupo hapo hatujui kinachoendelea. Mkaburu alitumiwa na waingereza kuinunua benki kwa bure maana ile dola 300 Mill tulimrudishia ili atuuzie NMB

Baada ya hapo akaiuza kwa Standard Chartered Bank ya Mwingereza kwa faida ya mara kumi ya aliyoinunulia benki na ukizingatia alirudishiwa kila sumni na hivyo kuichukua bure.


Subiri mziki bado sanaaaaaaa kuna mengi utajifunza na hawa mabeberu

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…