Mpasuko mkubwa kwenye Baraza la Mawaziri kisa kuuzwa kwa Bandari

Kwa hiyo kama Samia akiwa mwenyekiti wa CCM, na Amiri Jeshi mkuu, ndio atoe bure bandari zetu watanganyika milele kwa waarabu?

Unakurupuka kama mtoto kujibu, wewe ndie unayeshusha hadhi ya hili jukwaa.
😄😄😄
 
Na huyu Tulia alitulizwa na chapaa siyo bwerere anatusaliti na hata jimboni kwake hawataki hata kumsikia.
Honorable Spika alijiondoa the honorability(ni neno) na alijitwaa u FaizaFoxybility, na akawaita Wapiga kura wake ni Wajinga!

Unategemea vipi wapiga kura wake Wamsikilize?

Sasa hizi Nguvu wanazotumia watwana hawa, TuliaFoxy na
20141018_MAP004_0.jpg

vibaraka wa Waarabu na hawa wakoloni mamboleo ni nguvu wanazoweza kuvuliwa, na ikumbukwe, kama ilivyoelezwa kinadharia na kiuhalisia, Watashindwa kwenye sanduku la Kura! Watashindwa kwa kushindwa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT. Watashindwa lwa Usaliti kwa Watanganyika.

Amani ikufikie
 
Kuna viashiria si shwari tena Baraza la Mawaziri;

1) Waziri Mkuu kumwakilisha Rais nchini Urusi taifa tajiri kuliko yote duniani kwa maliasili ni dhahiri Makamu wa Rais ananyanyapaliwa. Wakati wa Magufuli Makamu wa Rais ndiye aliyekuwa ana mwakilisha Rais nje ya nchi na wala siyo Waziri Mkuu.

2) Makamu wa Rais na wengi wa Mawaziri Watanganyika wamejizuia kuutetea wizi wa maliasili za nchi yao na kuonyesha kuna mifarakano na sintofahamu ndani ya Baraza la Mawaziri.

3) Agizo la Rais la kumwelekeza Waziri wa uchukuzi aingie mkataba wa kimataifa haukuonyesha ulitokana na vikao vya baraza la mawaziri. Hii ni ushahidi tosha uamuzi wa kuuza nchi haukuwa wa baraza la mawaziri.

4) Hakuna jitihada zozote zile zilizofanywa na serikali kuambatanisha muhtasari wa Baraza la Mawaziri kulithibitishia bunge uamuzi wa kuuza bandari zetu ulitokana na maamuzi ya vikao vya Baraza la Mawaziri kabla ya Rais kumwagiza Waziri wa Uchukuzi kusaini mkataba wa kuuza nchi yetu pendwa.

Tungependa kukumbusha tu hakuna uwajibikaji wa pamoja kwenye maamuzi yasiyo shirikishi.

5) Kwa vile mkataba wa kuuza nchi ulifanywa bila ya kuzingatia mpango wa miaka 5 ya uendelezaji wa bandari zetu hii ni ushahidi tosha msukumo wa kuuza bandari zetu haukutoka kwa Mamlaka ya bandari zetu. Na ndiyo maana Mtendaji Mkuu wa bandari zetu alitupiwa virago vyake kwa sababu alipinga huu wizi wa mali ya umma.

6) Kuna viashiria uamuzi wa kuuza bandari zetu ulikuwa wa kukurupuka kwa sababu ulifanyika baada ya kupokea mkopo wa benki ya dunia wa dola 420 milioni na hata hizo hela hatujajua kama zingetatua matatizo yetu ya ufanisi, uthibiti wa mapato nk, wao wakaamua kumtajirisha mwekezaji.

7) Wanaoupigia upatu huu wizi wa mali ya umma hawamo kwenye Baraza la Mawaziri ila wanaona huu ni mwanya wa kujenga hoja ya kufikiriwa kujaza nafasi ya mawaziri waliopo ambao wanaonekana hawaafiki nchi yao kuuzwa.

8) Ukimwondoa Waziri wa uchukuzi hakuna Mzanzibara hata mmoja ambaye aliandamana na genge la makada wa CCM ambao walikuwa wanapigia upatu wizi wa mali ya umma. Ni dhahiri hata Wazanzibara hawaafiki na hili.

9) Pamoja na Kikwete kujitokeza hadharani na kudai anamuunga mkono Rais lakini hajawahi kuuteteta huu wizi wa mali ya umma.

10) Makamu wa Rais hajawahi hata mara moja kutetea nchi kuuzwa na hii inaashiria mpasuko mkubwa ndani ya Baraza la Mawaziri na tunabashiri wakati wa Uchaguzi wa 2025 jina lake litakatwa na hatarudi kwenye nafasi yake ya Umakamu wa Urais. Tutafafanua zaidi kwenye hili.
Kweli, kama ambavyo wananchi wamelipokea Mkataba wa DP World kwa kushtukiziwa, inaelekea vivyo hivyo vikao mbalimbali vya maamuzi ndani ya serikali na hata ccm havikushirikishwa. Kabla ya vikao vya hivi karibuni vya ccm hakuna kiongozi wa chama alishapata kuzungumzia mkataba wa bandari licha ya kwamba kelele zilishaanza kupigwa. Siyo kwamba hao viongozi waliamua tu kunyamaza bali walikuwa hawajui chochote. Kwenye mitandao ya kijamii watu walionyesha kushangazwa kuwa kinyume na ilivyozoeleka hata UVCCM kama hawakujitokeza kuunga mkono.

Inaelekea kupitia vikao vya karibuni ccm wamewekana sawa na kukubaliana kunusuru uongozi wao kwa kadhia hii. Walikubaliana kufunika kombe mwanaharamu apite. Vivyo hivyo upo uwezekano mkubwa vikao vya kiserikali navyo havikushirikishwa. Ndiyo maana kinyume na matarajio na taratibu, hata kule bungeni AG hakuchukua nafasi yake kwenye mjadala wa Azimio la Bunge kuridhia mkataba. Badala yake, inaelekea Spika wa Bunge ndiye aliyechukua nafasi ya AG!

Inaelekea ndani ya nchi yetu sasa kuna kikundi cha wahuni wanahaha sana kuona kuwa uchaguzi wa 2025 hausababishi mabadiliko yoyote katika uongozi wa juu wa nchi. Wahuni hawa wanahaha kudumisha 'status quo' kwa maslahi yao binafsi. Ndani ya kikundi hiki wamo mafisadi na wahuni ambao kwa muda mrefu wametumia ccm kama ngazi ya kupandia kupata madaraka na kichaka cha kujificha wakati wakiibia nchi hii na kulinda na kuimarisha ufisadi wao. Bila shaka hawa wahuni ndiyo waliobuni mpango wa Mkataba wa bandari. Upo uwezekano mkubwa kuwa pamoja na uwekezaji wa DPW kwa lengo lililofichwa la mpangi huu ni kuibinafsishia ccm bandari za nchi kwa mgongo wa DP World. Ndiyo kusema kupitia mpango huu ccm itakuwa na "hisa" za siri kwenye buashara ya bandari za nchi ili kuwa na uwezo wa kifedha kununua chaguzi mbalimbali katika nchi hasa nafasi za juu za uongozi.
 
Kama watu wapo serious uchaguzi ujao wabunge wote including wa viti maalum wapigwe chini asichaguliwe hata mmoja
Kwani walichaguliwa?
Si Magu aliwapa ushindi[emoji1787]

Mimi ni die hard fan wa JPM sema mzee kwenye hili alizingua sana.
 
Kuna viashiria si shwari tena Baraza la Mawaziri;

1) Waziri Mkuu kumwakilisha Rais nchini Urusi taifa tajiri kuliko yote duniani kwa maliasili ni dhahiri Makamu wa Rais ananyanyapaliwa. Wakati wa Magufuli Makamu wa Rais ndiye aliyekuwa ana mwakilisha Rais nje ya nchi na wala siyo Waziri Mkuu.

2) Makamu wa Rais na wengi wa Mawaziri Watanganyika wamejizuia kuutetea wizi wa maliasili za nchi yao na kuonyesha kuna mifarakano na sintofahamu ndani ya Baraza la Mawaziri.

3) Agizo la Rais la kumwelekeza Waziri wa uchukuzi aingie mkataba wa kimataifa haukuonyesha ulitokana na vikao vya baraza la mawaziri. Hii ni ushahidi tosha uamuzi wa kuuza nchi haukuwa wa baraza la mawaziri.

4) Hakuna jitihada zozote zile zilizofanywa na serikali kuambatanisha muhtasari wa Baraza la Mawaziri kulithibitishia bunge uamuzi wa kuuza bandari zetu ulitokana na maamuzi ya vikao vya Baraza la Mawaziri kabla ya Rais kumwagiza Waziri wa Uchukuzi kusaini mkataba wa kuuza nchi yetu pendwa.

Tungependa kukumbusha tu hakuna uwajibikaji wa pamoja kwenye maamuzi yasiyo shirikishi.

5) Kwa vile mkataba wa kuuza nchi ulifanywa bila ya kuzingatia mpango wa miaka 5 ya uendelezaji wa bandari zetu hii ni ushahidi tosha msukumo wa kuuza bandari zetu haukutoka kwa Mamlaka ya bandari zetu. Na ndiyo maana Mtendaji Mkuu wa bandari zetu alitupiwa virago vyake kwa sababu alipinga huu wizi wa mali ya umma.

6) Kuna viashiria uamuzi wa kuuza bandari zetu ulikuwa wa kukurupuka kwa sababu ulifanyika baada ya kupokea mkopo wa benki ya dunia wa dola 420 milioni na hata hizo hela hatujajua kama zingetatua matatizo yetu ya ufanisi, uthibiti wa mapato nk, wao wakaamua kumtajirisha mwekezaji.

7) Wanaoupigia upatu huu wizi wa mali ya umma hawamo kwenye Baraza la Mawaziri ila wanaona huu ni mwanya wa kujenga hoja ya kufikiriwa kujaza nafasi ya mawaziri waliopo ambao wanaonekana hawaafiki nchi yao kuuzwa.

8) Ukimwondoa Waziri wa uchukuzi hakuna Mzanzibara hata mmoja ambaye aliandamana na genge la makada wa CCM ambao walikuwa wanapigia upatu wizi wa mali ya umma. Ni dhahiri hata Wazanzibara hawaafiki na hili.

9) Pamoja na Kikwete kujitokeza hadharani na kudai anamuunga mkono Rais lakini hajawahi kuuteteta huu wizi wa mali ya umma.

10) Makamu wa Rais hajawahi hata mara moja kutetea nchi kuuzwa na hii inaashiria mpasuko mkubwa ndani ya Baraza la Mawaziri na tunabashiri wakati wa Uchaguzi wa 2025 jina lake litakatwa na hatarudi kwenye nafasi yake ya Umakamu wa Urais. Tutafafanua zaidi kwenye hili.

Soma number 9 tena na tena.
 
Fitina na majungu ndio lengo la huu uzi. Makamu akienda huko nje mnakuja na uzi wa kumnyanyapaa mkisema kazi yake ni kukata utepe na kuhutubia katika sherehe tu.

Serikali yote ipo kama kitu kimoja, hakuna mgawanyiko kama huu mnaojaribu kuutengeneza vichwani mwenu.

Waambieni hao mafisadi wanaowatumia kuanzisha mada humu jamvini kwamba muda wao umeshamalizika.
Hoja kuu ya huu uzi mbona mawaziri watanganyika hawatetei kuuzwa kwa nchi yao? Jaribu kujikita kwenye mada mdau

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Mawaziri wa CCM tunawajua, wote wanatekeleza maamuzi ya chama [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Huo mpasuko labda upo kwenye sketi
[emoji2] [emoji3] [emoji1] [emoji16] [emoji1787] [emoji23] [emoji2] [emoji3] [emoji1] [emoji16] [emoji1787] [emoji23]
 
Hakuna hoja ya maana, unaposema nchi imeuzwa uweke na ushahidi wa mauziano na makabidhiano wa hiyo bidhaa iitwayo nchi.

Mnapotosha watu kwa kutumwa na kundi fulani la wezi pale bandarini lakini mnasahau namna mnavyowatendea vibaya wafanyabiashara wa kweli wa uagizaji na uuzaji wa bidhaa wanaoitumia bandari yetu.

Nyinyi wengi wenu mnashinda humu JF hivyo hamuwezi mkajua kwa kina kile kilio cha bandari yetu mpaka kufikia kupoteza wateja wanaoamua kwenda Kenya wakikimbia urasimu uliopo mahali pale.

Ipo siku mtakuja kuulipia huu usaliti mnaoifanyia nchi yenu kwa makusudi kabisa.
Kwa hiyo mwarabu ndiyo mwarobaini wa wizi na ubadhirifu jipange upya huko ni mchepuko hauna tija
 
Kuna viashiria si shwari tena Baraza la Mawaziri;

1) Waziri Mkuu kumwakilisha Rais nchini Urusi taifa tajiri kuliko yote duniani kwa maliasili ni dhahiri Makamu wa Rais ananyanyapaliwa. Wakati wa Magufuli Makamu wa Rais ndiye aliyekuwa ana mwakilisha Rais nje ya nchi na wala siyo Waziri Mkuu.

2) Makamu wa Rais na wengi wa Mawaziri Watanganyika wamejizuia kuutetea wizi wa maliasili za nchi yao na kuonyesha kuna mifarakano na sintofahamu ndani ya Baraza la Mawaziri.

3) Agizo la Rais la kumwelekeza Waziri wa uchukuzi aingie mkataba wa kimataifa haukuonyesha ulitokana na vikao vya baraza la mawaziri. Hii ni ushahidi tosha uamuzi wa kuuza nchi haukuwa wa baraza la mawaziri.

4) Hakuna jitihada zozote zile zilizofanywa na serikali kuambatanisha muhtasari wa Baraza la Mawaziri kulithibitishia bunge uamuzi wa kuuza bandari zetu ulitokana na maamuzi ya vikao vya Baraza la Mawaziri kabla ya Rais kumwagiza Waziri wa Uchukuzi kusaini mkataba wa kuuza nchi yetu pendwa.

Tungependa kukumbusha tu hakuna uwajibikaji wa pamoja kwenye maamuzi yasiyo shirikishi.

5) Kwa vile mkataba wa kuuza nchi ulifanywa bila ya kuzingatia mpango wa miaka 5 ya uendelezaji wa bandari zetu hii ni ushahidi tosha msukumo wa kuuza bandari zetu haukutoka kwa Mamlaka ya bandari zetu. Na ndiyo maana Mtendaji Mkuu wa bandari zetu alitupiwa virago vyake kwa sababu alipinga huu wizi wa mali ya umma.

6) Kuna viashiria uamuzi wa kuuza bandari zetu ulikuwa wa kukurupuka kwa sababu ulifanyika baada ya kupokea mkopo wa benki ya dunia wa dola 420 milioni na hata hizo hela hatujajua kama zingetatua matatizo yetu ya ufanisi, uthibiti wa mapato nk, wao wakaamua kumtajirisha mwekezaji.

7) Wanaoupigia upatu huu wizi wa mali ya umma hawamo kwenye Baraza la Mawaziri ila wanaona huu ni mwanya wa kujenga hoja ya kufikiriwa kujaza nafasi ya mawaziri waliopo ambao wanaonekana hawaafiki nchi yao kuuzwa.

8) Ukimwondoa Waziri wa uchukuzi hakuna Mzanzibara hata mmoja ambaye aliandamana na genge la makada wa CCM ambao walikuwa wanapigia upatu wizi wa mali ya umma. Ni dhahiri hata Wazanzibara hawaafiki na hili.

9) Pamoja na Kikwete kujitokeza hadharani na kudai anamuunga mkono Rais lakini hajawahi kuuteteta huu wizi wa mali ya umma.

10) Makamu wa Rais hajawahi hata mara moja kutetea nchi kuuzwa na hii inaashiria mpasuko mkubwa ndani ya Baraza la Mawaziri na tunabashiri wakati wa Uchaguzi wa 2025 jina lake litakatwa na hatarudi kwenye nafasi yake ya Umakamu wa Urais. Tutafafanua zaidi kwenye hili.
Kwenye uovu, ni vigumu sana watu wote mkubaliane. Lazima wengine dhamira zao zitakataa, hata kama watalazimishwa na mazingira yao ya kazi.
 
Matumizi mabaya ya neno 'Mpasuko' ukihusiana na waCCM. Wote wanaimba wimbo mmoja wakisindikizwa na wapiga makofi na vigelegele(machawa)
 
Hiyo aspect zijaizungumzia nimeongelea uongo wako kwamba makamu wa rais ndo pekee humwakilisha rais kwenye mikutano ya kimataifa na kwamba waziri mkuu hajawahi kumwakilisha
Sijasema ni pekee ila kutokana na ukubwa wa matatizo yetu ya kiuchumi alipaswa kuongoza huo msafara badala ya kumwachia waziri mkuu ambaye sina uhakika hata umombo umetua.Tunashida kubwa ya uraro wa mapato na kiwese kimechangia sanaaaaaaa na Makamu wa Rais angelienda huko Putin angelimpa uzito zaidi na hata kutufungulia bomba la uhakika tukaachana na hawa kupe wahindi wanaotumaliza na mafuta hayo hayo ya Urusi ila huyapitishia India
 
Kwa hiyo mwarabu ndiyo mwarobaini wa wizi na ubadhirifu jipange upya huko ni mchepuko hauna tija

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
Mwarabu ana teknolojia ambayo sisi hatuna. Kumbuka bandari sita za China zimemkodisha.

Siasa nyingi za kijinga ndio sifa ya utanzania wa leo hii, hakuna mantiki zaidi ya kudharau ambacho mtu hana uelewa nacho.
 
Back
Top Bottom