Tetesi: Mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM

Aendelee tu kulalamika, lakini CCM haimtambui tena maskini.
 
JPM ataendelea kuwa Rais 2020 - 2025.

Hizi nyingine ni porojo tu za mitandaoni.
 
Sasa watafanyaje mkuu wakati akili zao walisha zikabidhi kwa chakubanga?
Na usiwaone wanajikakamua humu, wakiwa Lumumba kwenye mgao wanakuwa wapole sana,wanafokewa sana
 
Membe ndiye mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM mwaka huu ni suala la muda tu
 
Sio wote wanaofaulu kwenda A level wamescore Division one ya 7A's..labda alikua operative wa kawaida tuu hapo TISS..Ubobezi unategemea Sana missions alizo accomplish.
 
Kama hawakutaki hawakutaki tuu hata aende vikao gani ashapigwa chini na hatarudi tena, na anajua uraisi hawezi kushinda yaani na hashimu rungwe hawana tofauti wanahangaikia matumbo yao. Kama anawafadhali aendelee kuwapiga tuu.
 
Membe hana lolote. Alishindwa Lowasa itakuwa Membe. Membe hana tofauti marehemu Mnasa Sabi Mnasa aliyegombea awamu ya pili na Mkapa

QUOTE="Mystery, post: 35783641, member: 73370"]
Kwa namna huyu "Jasusi mbobezi" Bernard Kamilius Membe, anavyoendelea kushika "chart" humu kwenye mitandao ya kijamii, ni dhahiri kuwa huko kwenye hicho chama, wanachodai wenyewe kuwa ni chama kikubwa, hivi sasa kunatokota na sisi wananchi tusubiri, kwa kuwa yajayo yanafurahisha au kukarahaisha...

Membe ametoa madai mazito sana kuwa Katiba ya CCM haikufuatwa katika kufukuzwa kwake ndani ya Chama

Kwani amedai kuwa ni takwa la kikatiba, anapofukuzwa kiongozi yeyote wa ngazi za juu katika chama hicho ni LAZIMA jambo lake lingejadiliwa ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, ndipo uamuzi ufikiwe.

Jambo ambalo halikufanyika katika kufikia uamuzi wa kufukuzwa kwake. Kwani mwenyewe anadai kuwa "process" ilikuwa haijakamilika, kwa kuwa kikao kilichomjadili kilikuwa ni kikao cha Kamati Kuu pekee, wakati mchakato ulikuwa haujakamilika, kwa kuwa kikao chenye uamuzi wa mwisho, ambacho ni kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilikuwa hakijakaa.

Jambo linaloshangaza ni kuwa tokea madai hayo yatolewe na Membe, hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya juu wa CCM, aliyejitokeza kujibu tuhuma hizo

Kwa madai mazito kama hayo, ni kwanini hadi sasa chama cha CCM, kimeamua kukaa kimya, kisitoe majibu yoyote, kwa madai hayo ya Membe?

Inaelekea kuna mfukuto mkubwa sana huko kwa majirani zetu wa CCM

Ni dhahiri sasa kama alichoongea mwenyewe Membe, kuwa tufanye subira kati ya mwezi huu wa June hadi October ya mwaka huu, lolote lisilotegemewa na wananchi wengi litatokea katika nchi hii na litaleta kishindo kikubwa sana!

Subira yavuta kheri, ngoja tusubiri ili tuyashuhudie yatakayojiri
[/QUOTE]
 
Kwa kuwa unaamini mwisho ni ushindi unao_matter bila kujali umepatikanaje, hao wapinzani wa JPM nao wanaweza kupita njia hiyo hiyo na JPM asirudi ofisini.

Hiyo itakuwa poa sana
 
Jasusi mbombezi ana rekodiwa akiwa anaongea na simu. Emu acha kumpa sifa ambazo hazimfai huyo mzee, sijui kashamaliza pensheni yake.
 
unaeweza kusumbua ni wewe tu
 
Umemaliza kila kitu mkuu,huu mjadala ufungwe sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…