Mpasuko mkubwa wa Ardhi watokea Mbagala Saku. Baadhi ya nyumba za watu zaripotiwa kubomoka

Serikali na idara zake za ardhi na hali ya hewa hawajulikani walipo, madiwani , wabunge au madiwani wao hawana number zao? mbunge anaweza kumpigia waziri Moja Kwa Moja wakapata usaidizi wa haraka
 
Watu wamejega juu ya madampo juu ya makaburi juu ya mito kwenye mashimo ya michanga ili mradi vurugu hiyo mimomonyoko lazima itokee kipindi flani!
 
Tanzania hatuna wataalamu wanaoweza kupima chini ya ardhi, tukumbuke tukio la tope Kunduchi mpaka leo hakuna jibu mpaka leo, wataalamu wa Chuo Kikuu cha Ardhi waliingia mitini.
 
Watu waache kuchimba visima vya maji, kwa kutoa maji ardhini wanafanya ardhi kuwa dhaifu
 
Nadhani mvua iliyonyesha imesavabisha udongo kubeba maji mengi. Hiyo ilitokea pia maeneo ya Tabata Bonyokwa, maji yalikuwa yanatokea mlimani kama chemchem, na ukikanyaga hiyo sehemu unatitia. Maji yalikauka wiki 2 baada ya mvua kukatika. Uzuri eneo hilo lina miti na majani. Kuna ukuta wa nyumba moja ulishuka sababu ya hiyo chemchem.
 
Hapa kwa hesab za haraka haraka ni kwamba hifadhi ya maji ardhini imekua disturbed na unstable, pengine kutokana na kuzidisha uvunaji wa maji-ardhi, uchimbaji madini au vifusi nk. cha msingi serikali iingilie kati wataalam husika wafanye mapping ili kuwaelekeza wananchi waondoke kwenye maeneo yote hatarishi. ni vyema pia ikawapa nyumba au viwanja maeneo mbadala.
 
Uko saku kuna bonded limemegukameguka vibaya sana mvua hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…