TANZIA Mpelelezi Mkuu wa PCCB ndugu John Minyenya afariki dunia

TANZIA Mpelelezi Mkuu wa PCCB ndugu John Minyenya afariki dunia

Wakuu, Mpelelezi Mkuu wa PCCB ndugu John Minyenya afariki dunia usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Hindu Mandal baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Bwana Minyenya alikuwa miongoni mwa viongozi wa juu waliopeleka taarifa ya pelelezi mbalimbali za tuhuma wakati wa kukabidhi ripoti kuu ya PCCB ya mwaka 2019/2020.

Aliyezungushiwa alama ni yeye akiwa pamoja na waziri mkuu wakati huu wa mapambano ya COVID 19.

Alale salama
View attachment 1442868
Ndio maana namuona Mkulu, hatoki chato,
Na hii covid ikifika october Haki ya nane!
Sijuhi kama atafanya kampeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ndiye aliyepokea barua za misamaha ya wafungwa kisha akaruka barua ya Kabendera ili aendelee kuteseka lupango!Aende tu!
Sio yeye ni ile remote control iliyojificha kule mafichoni chattle ndiyo inawaburuza hawa watendaji . Si unaona yanayoendelea huko Bungeni. Spika ananata na beat ya mpiga ngoma wa chattle.
 
Mkuu Nina hakika taarifa ulizo nazo kuhusu huyo Minyenya sio sahihi! Nina fahamu kituo chake cha kazi kabla ya kupelekwa makao makuu na ninajua alihamishiwa makao makuu lini ndio maana nakwambia taarifa ulizo nazo sio sahihi kafuatilie vizuri kumuhusu huyo kiongozi!

Sent using kidole gumba
Nadhani kweli amemchanganya huyu Minyenya. Kama ametokea mikoani na hapo makao makuu ana muda mfupi sasa anahusikaje na kesi ya Kabendera?
 
Apumzike Kwa amani,
Hakika kila nafsi itaonja mauti, kila mmoja ataondoka Kwa wakati aliopangiwa na kwa sababu anayoijua Mungu pekee.
Hakuna anaye ijua kesho yake!
 
Hawa ndo wanakaaga na majalada ya watuhumiwa kwa miaka hata 10 ama sio? Wakiisaidia serikali kutesa watu wakibaki mahabusu kwa muda mrefu
 
Back
Top Bottom