Mpenda Haki? Mpenda Amani? Jumapili Tukutane Kwa Gwajima!"

Ian Ndlovu alisema Kuna makosa mawili atakayofanya kabla ya uchaguzi mkuu yatakayo mlazimisha kuachia kiti.

Nasubiri kwa hamu nione kabla ya Septemba nini kitatokea.
Mkuu 'Gagnija', mbona hadi wakati huu amekwisha fanya makosa mengi tu zaidi ya hayo mawili unayoyasubiri?
Au unasubiri damu itirilike kwa wingi mitaani, kuliko inavyo fanyika sasa hivi kwa watu ku otezwa?
 
Yani mkuuu hunizidi mimi

Me nakwambia inaniumiza kuliko unavyoweza kufikiria,......sielewi wabongo tuna uzuzu wa kutoka wapi kwa kweli

Nimesoma humu leo,kuna mtu kapigwa mpaka mauti na watendaji wa kijiji eti kwa tuhuma za wizi

Sasa habari kama hizo zinanipasua sana moyo wangu mpaka nakuwa nashindwa kuendelea kuzisoma au nazokwepa kabisaa

Maana huwa zinanifanya nafikiria mambo mengi sana, najiuliza maswali mengi sana ,mwishowe najikuta najuta tu kwa kukosa namna.......,
 
Ndio, wanatumia nguvu sana… lakini nguvu za haki na sauti ya wananchi huwa hazizimwi kwa virungu. Twende tukaabudu kwa pamoja kwa Mungu wa roho na kweli.
Sasa sijui nilisemeje hili, kwa sababu ni jambo la kusikitisha sana.
Kuna historia ndani ya nchi yetu; pamoja na kwamba hakuna mfanano wa moja kwa moja, lakini ni tukio lililo karibu na hili linalotafutwa sasa hivi. Hili likitokea itakuwa ni kama kulipiza kisasi (bahati mbaya sana).

Nalikumbushia tukio la Mwembechai. Samia na GENGE lake bila shaka yoyote wanalikumbuka vizuri tukio hilo; kwa hiyo mategemeo yao ni kwamba, litafanyika, na mambo yataendelea vile vile ilivyokuwa wakati ule; ila sasa litawapa ujasiri zaidi wa matumizi ya nguvu kubaki madarakani.
Akina Jumanne Murilo na akina Awadh bila shaka watakuwa mstari wa mbele kabisa kulipiza hicho kisasi.
Mimi napendekeza tusiwape fursa hiyo sasa hivi. Tutumie njia nyinginne za kuwavurumisha mashetani hawa.
 
Usikate tamaa.
Huwezi kuikatia tamaa Tanzania; never!
Kidogo unachoweza kuchangia, changia ili mwishowe tuondoe dhulma hii nchini mwetu.
 
Kama maagizo yametolewa na mahakama, polisi wanapaswa kuyatekeleza bila masharti, hiyo ndiyo misingi ya utawala wa sheria. Kutotekeleza ni kuvunja mfumo wenyewe.
Kwa maana hiyo basi, inawezekana kwenda mahakamani tena kuanzisha kesi dhidi ya wanaozuia watu kuabudu?
Hili ni swali ninaloomba ulitafakari vizuri kabla hujanijibu lolote.
 
Tuja

Tunaanzia wapi Kaka?tunaanzia wapi?
Kwenye jamii kama hii?
Samahani sana, sina maana ya kukuzungusha kuhusu hili jambo.
Jibu langu ni hilo hilo. Kama wewe unajihisi hatuna pa kuanzia, ndivyo hivyo hivyo na mamilioni ya waTanzania wengine wanavyo jiuliza hivyo hivyo!
Kwa hiyo, tatizo linaanzia kwetu sisi wenyewe kwa kujiona hatuna tunacho weza kufanya. Laiti kama tungefanya hata hicho kidogo kabisa, badala ya kukata tamaa moja kwa moja!
Kuazimia kutoshiriki katika jambo lolote linalowapa kisingizio cha kubaki madarakani, ni hatua moja muhimu; kama kutoshiriki kwenye kupiga kura.

Hakuna atakaye kuja nyumbani kwako kukupiga risasi kwa vile hukwenda kupiga kura; au hukujitokeza kwenye mikutano yao ya hadhara; n.k., n.k..
Ni kuwanyima ushirikiano katika jambo lolote lile wanalofanya.
 
Mkuu 'Gagnija', mbona hadi wakati huu amekwisha fanya makosa mengi tu zaidi ya hayo mawili unayoyasubiri?
Au unasubiri damu itirilike kwa wingi mitaani, kuliko inavyo fanyika sasa hivi kwa watu ku otezwa?
Alipokufa Magufuli, tuliambiwa nchi imerudishiwa tabasamu. Tunachokiona kwa sasa ni udhalimu kuliko wakati wa Magufuli.

Still, I'm hopeful that as a nation, we'll laugh again before October.
 
Alipokufa Magufuli, tuliambiwa nchi imerudishiwa tabasamu. Tunachokiona kwa sasa ni udhalimu kuliko wakati wa Magufuli.

Still, I'm hopeful that as a nation, we'll laugh again before October.
Binafsi sijawahi kuwa na matumaini makubwa juu ya nchi yetu kuondokana na balaa hili kama niliyo nayo safari hii.
Itakuwa ni laana ya kipekee sana kama fursa hii itawapita pembeni waTanzania.
 
Mnapigana na nani na kwa faida ya nini? Mnapigana dhidi ya nini?

KUBWA KULIKO YOTE"
"UNAVIJUA VITA AU UNAROPOKA?"
kama hujui kinachopiganiwa nina sababu gani ya kukuambia? ukitaka kujua kama navijua vita au naropoka anzisha uone
 
Kwa maana hiyo basi, inawezekana kwenda mahakamani tena kuanzisha kesi dhidi ya wanaozuia watu kuabudu?
Hili ni swali ninaloomba ulitafakari vizuri kabla hujanijibu lolote.
Kwa sasa, sio kwa Tanzania hii.
 
Tulimtetea alipoletewa figisu.. Mara paap kaenda kuchukua fomuπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† nikajua hii ndio michezo yao...simtetei tenaπŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸ˜‚πŸƒπŸΏπŸƒπŸΏ
 
Tatizo la hilo kanisa ni moja TU, kutojali wengine Kwa kupiga makelele usiku. Ni haki yao kusali usiku ila sio kwa spika zinazosikika 5km Radius. Kwa kweli ni bughudha mno. Serikali iingilie kati haya Maombi ya usiku kwa spika.
 
wewe utakuwa una mapepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…