Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Dini zipo kwa ajili ya watu na siasa kwa ajili ya watu ukisema hatupaswi kuchanganya means aliyechagua siasa haendi mbinguni kwa kuchagua upande sio?

Shida hapa siasa zinazofanywa ni za kimagendo ndio tunafika kusema hatupaswi kuchanganya ni kwa sababu hiyo siasa za sasa ni magendo na dini zinajitenga na umagendo
 
Mkuu Paskali umekurupuka kutoa uzi kabla ya kufikiri kwanza. Maaskofu kama raia halali wa nchi hii nao wanayo haki ya kutoa maono yao juu ya mustakabali wa nchi, hasa pale wanapoona rasimilamali za taifa zinatapanywa na CCM. Wewe ulitaka wausifie huu mkataba wa kifisadi kwa manufaa ya nani?
 
According to you halafu ndio ukweli?. Yani wewe ndio unaamua ukweli ni ipi. Waarabu wameanza kuwekeza Leo Tanzania?. Tatizo mnataka muibe bandari Kama mlivyoiba gesi ya mtwara na mwisho mkarudi kwa wananchi kuwatoza tozo, eti serikali haina fedha.
Safari hii Waarabu wameshika pabaya
 
Hakuna kingine wanaogopa influence ya mwarabu,wanajua uislam ulifika Tanganyika kupitia mwarabu,bila ujio wa mwarabu pasingekua na uislam,wanajua mwarabu ana pesa,pesa zitaleta miradi Kama shule na hospital ambazo wao wametumia kuvuna waamini
Hao waarabu kama wana nia ya kusaidia wawajengee misikiti kila kata nchi nzima hakuna shida, sio lazima mpaka waje kutawala bandari zote
 
Wasiolijua kanisa katoliki watabeza,, ila kwa tunaolijua kanisa hili kinagaubaga wacha tunyamaze,,
ombi langu mlioko kwenye "sistim" mshaurini Mama hii game ni ngumu..
 
Unaendelea kulamba miguu kama huna huna tu, una uchawa wa kitoto sana
 
Kwani Kuchanganya Dini na Siasa kuna Kosa shida gani ?
Unataka kusema kuna Kimoja kina ushetani Mwingi sana kustahili Kuchanganywa na chengine ?
 
Udini unawatesa tu wasubiri j2 wakawaibie kondoo wao ili walishe familia zao huku kondoo zikipigwa maombi ya kufa mtu ili awe tajiri


Kumekuchaa kataa kuibiwa kwa mgongo wa dini
 
Hakuna kingine wanaogopa influence ya mwarabu,wanajua uislam ulifika Tanganyika kupitia mwarabu,bila ujio wa mwarabu pasingekua na uislam,wanajua mwarabu ana pesa,pesa zitaleta miradi Kama shule na hospital ambazo wao wametumia kuvuna waamini
Sawa
 
Ngoja tuone na wa upande wa pili watasemaje ??!!
 
Kaka paskali mchakato wa kuwapa dipiwelidi bandari unamkanganyiko na chembe chembe nyingi za sintofahamu.

Viongozi wasiwe na haraka kwenye hilo suala la bandari.

Halafu hao tec hawajakurupuka aiseee wamewahoji wahusika wengi.

Mwambieni Mama awe anasoma vitu na apatapo mashaka awe na vijana watiifu kwa jamhuri na sio chawa wawe wanamwambia ukweli mchungu.

Hatuna rekodi nzuri za kimikataba hasa tunayoenda kusaini tukiwa na njaa

Shida ni kubwa ni kuwa kama taifa hatuna dira rasmi.
Wao wametoa mashauri yao kama baraza naamini wanamaono yenye wema ndani.
 
Tuliosoma digrii ya sayansi ya jamii na hususani mabadiliko ya kijamii katika vipindi tofauti tulifundishwa kuwa dini na siasa vilikuwa pamoja kugandamiza jamii au vilifarakana mno na viongozi wa dini kuuawa. soma Marxist theories,feudalism,capitalism na muundo wa superstructure Roman empire na mapito yake ujio wa ukrisitu na uislam ukoloni, na mwisho wa utumwa,dini ilitumika sana na dola! hivi vitu havitenganishwi kivitendo na kiuhalisia kwa urahisi. they are inseperable kwa uwazi au kificho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…