Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Ilipojaribu uliposema bunge ni wawakilishi wa wananchi!Sijui wananchi wepi kwa uchaguzi wa 2020 ambao uligubikwa na mauzauza ya kutisha mpaka mzee Magu aliwaonya wabunge kwamba pasipo yeye hakuna ambaye angeweza kuwa mbunge
Inamaana Jiwe ndiye aliyetuchagulia wabunge!
 
Patamu hapo, sasa tutaangalia je hii serikali iko mfukoni mwa kanisa katoliki au haina dini?
 
Tuambiane ukweli, jiulize, rais angekuwa ni MkatolikinMagufuli ndio ameileta hii DPW, TEC wangetoa waraka huu?.

Mkuu Pascal Mayalla mbona hao maaskofu huwa hawabagui ? Wao nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi soma waraka huu hapo chini wakimkosoa Magufuli Mahakama Bunge na mambo mengine

 
Ndio maana jambo lako la EA lilikwama mkuu
 
Hakuna kingine wanaogopa influence ya mwarabu, wanajua uislam ulifika Tanganyika kupitia mwarabu, bila ujio wa mwarabu pasingekua na uislam, wanajua mwarabu ana pesa, pesa zitaleta miradi Kama shule na hospital ambazo wao wametumia kuvuna waamini
Wanaogopa kurudi Utumwani
 
Huu ndo unafki uliopo katika haya mambo. Taasisi za kidini zibakie na kazi ya dini na mambo ya utawala yabakie katika serikali. Jambo likiwagusa kanisa ndo wanajifanya wana uTanzania lakini lisipo wagusa wanakaa mbali na kujifanya haliwahusu ni jambo la kiutawala.

Kama serikali inauwezo wa kuuza mali za nchi bila ridhaa ya wananchi huoni kama hapa tatizo kubwa ni mifumo ya kiutawala na katiba? wananchi wamelalamika kuhusu katika kwa miaka mingapi sasa? kanisa walitoa waraka? nini kikubwa katika nchi zaidi ya katiba? Huu ni upumbavu wa hali ya juu kwa hili kanisa kuhisi wao ndo watawala wa hii nchi.

Kutumia mwamvuli wa udini kutoa misimamo ya kitaifa ni kuligawa taifa! na hii inaashiria wazi ni kiwango gani taifa hili limejengwa katika misingi ya kuwapendelea wakristo.
 
The claim that God had to take a human form to understand the temptations and human sufferings (May God forgive me for even uttering this words) shows what a narrow understanding of God's power is to the claimers of this concept.

No wonder why they associate their wishes to God's will (eti sauti ya wengi ni sauti ya Mungu). In western countries kule kuna sauti kubwa sana ya kuunga mkono ushoga, je ni sauti ya Mungu hiyo?
 
Tunayo teknolojia inayokua kuweza kulingana na bandari nyingine zinazofanya vizuri?.

Wengi wanaopinga uwekezaji ni kama wanataka tubakie kwenye mkwamo wa uendeshaji tulionao kwa miaka mingi.

Hawatazami namna muwekezaji anavyokwenda kukuza rasilimali watu kwenye sekta nzima ya bandari, hawatazami ule ufanisi mzima wa ufanyaji kazi wa TPA utakavyokuwa.

Afrika inakwama kwa sababu ya kuwaendekeza mno wanasiasa na siasa kwa ujumla, hakuna anayejali wala kuheshimu mchango wa elimu.
 
Naomba nipate ufafanuzi wa hapa tuu mwana "Yohana Mtembezi" mwenzangu.
...pamoja na mema yote DPW waliokutendea during Expo Dubai, and after...
Mema yapi hayo!!??
 
Iwe kuchanganya au isiwe kuchanganya ,
mambo ya siasa hayapaswi kuwekwa kanisani ,kama wanaweza kufanya siasa waamue kujiunga na chama kimojawapo ,ndani ya makanisa mahekalu misikiti wapo wanavyama mbali mbali.
mambo ya bandali ni mzigo wa CCM .
Ingieni kwenye vyama sio mnataka kuwagawanya makanisa na kutuharibia vyama. Mkikamatwa mnasingizia dola inawabana kwa sababu Raisi ni Muislamu,

Vyombo vitawafuata huko huko madhabahuni.

Eti kanisa Katoliki ,njooni TEXAS USA muone wakatoliki wanavyolikimbia Kanisa na kuhamia ,nyie mpo mkidaiwa sadaka na mkidanganywa kusifu mungu mtu.

Mijicho yote hio mikubwa mnashindwa kuuona ukweli ,ila sema ndio hivyo mtakosa sadaka ya bwana.
 
Tunayo teknolojia inayokua kuweza kulingana na bandari nyingine zinazofanya vizuri?.
Hakuna teknologia mpya iliyoko kwenye bandari yoyote kubwa Duniani ambayo nchi hili ikiamua kusomesha watu wake, na kuwekeza kwa kununua mitambo ya kupakua na kupakia mizigo kama hiyo ya DPW, kwa ajili ya bandari ya Dar es salaam itashindwa kuwa na ufanisi.

Umesema mwenyewe kuwa siasa na wanasiasa ndio tatizo, ni kweli lakini zaidi ni wanasiasa wabadhirifu ngazi za juu ndio wenye maslahi kwenye bandari hasa hii ya Dar es salaam na ndio hao wanaotengeneza mgogoro kwa awamu zote nne kasoro awamu ya kwanza....

Grand corruption ndio tatizo kuu la bandari ya Dar es salaam.
 
Kuongea ni rahisi sana, miaka yote tumeshindwa wapi kusomesha wataalam wa sekta husika?, kumbuka kuwa maana ya bandari huenda ikibadilika kila kukicha. Sio upakuaji na upakiaji melini wa makontena ni zaidi ya hapo, hao DP World wanafanya shughuli za bandari kwenye mabara yote na wanao uzoefu mkubwa sana wa sekta husika, usidanganywe na hizi hoja za uzalendo na utaifa yapo mambo ni makubwa kuliko huo uzalendo wetu wa mdomoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…