Mpenzi aliyenisaliti amerudi, nawaza nimfanye nini?

Mpenzi aliyenisaliti amerudi, nawaza nimfanye nini?

Unapotembea na mawazo ya kumfanyia mtu ubaya unajipotezea muda tu, umekiri moyo wako uliumia, jiulize kama bado unauma au umepoa, kama umepoa mwambie huyo mtoto huna muda wa kuonana nae.

Kama bado unampenda nenda mkayaweke sawa mambo yenu inawezekana aliteleza tu hakuna asiekosea, lakini kujidanganya umfanyie ubaya huku bado unampenda unajiumiza mwenyewe bila kujua na utachukua muda mrefu kumsahau kwa mawazo ya revenge uliyonayo.
 
Nchi hii ina ziada ya wanawake 5,000,000 na zaidi hivyo nikimuona dume analia lia kuhusu mademu huwa namshangaa sana na wala sina muda wa kumshauri chochote.
 
Wewe bado unampenda na unasikilizia tu. Katika hii dunia msamaha ni kitu muhimu sana. Sikiliza moyo wako na utende kwa kadili ya maelekezo yake
 
Habari wana bodi,
Niende moja kwa moja kwenye maada tajwa hapo juu, ni miezi takribani 3 tangu aliyekuwa mpenzi wangu (x-girlfriend) aliponiacha kwa kunitamka kuwa "kuanzia leo mimi na wewe basi" alipo nitamkia sentence iyo tu tangu siku iyo hakuwai kuona sms wala calling yangu, nilifuta taarifa zake zote kwenye kitarakilishi changu (computer na simu) sikutaka kabisa kumsikia ila moyoni nilikuwa na maumivu yaliokuwa ykiwaka moto mzito,

atimaye amemtafuta mtu wangu wa karibu na kuomba kuonana na mimi ili tuongee, lakini main pont yake kuu ni kutafuta suruhu kwa kilicho tokea katikati yetu (usaliti alio nifanyia), uyu binti aliniachia maumivu makali sana wana JF, nilimpenda na kumthamini sana kwa kila kitu ila aliamua kwenda.

wakuu, uyu binti napanga siku ya kuonana nae nifanye nini (niongee nae nini, nimpangeje ili baadae nije kumpiga tukio zito), maana nahisi moyo wangu una hasira na chuki juu yake kama mbogo, ila sizionyeshi kwake waziwazi, nataka nimpitishe kwenye ziwa la miiba ili atakae kuja kumuoa uyu binti basi binti awe na adabu na heshima.

NINI NATAKA KUTOKA KWENU:

uyu binti nataka nimuweke kwenye mazingira ambayo afurahi kuwa na mimi uku nikimuandalia tukio lake la surprise.

natamani nipate experince kwenye issue ya X wako kurudi ulimpa adhabu gani kuu, ambayo atokuja kuisahau (sio kumdhuru kimwili noo).

Najua watakakuja watu hapa na kusema samehe na sahau, No ilo nalijua
Safi kabisa ubaya unalipwa kwa ubaya. Msubirie kwenye anga zako alafu mfanyie kitu hatasahau.
 
Wewe ndo utaamua kama kurudiana naye au kuacha, hayo mengine sijui ya kumfanyia kisasi hayana maana yoyote kwako.
 
Habari wana bodi,
Niende moja kwa moja kwenye maada tajwa hapo juu, ni miezi takribani 3 tangu aliyekuwa mpenzi wangu (x-girlfriend) aliponiacha kwa kunitamka kuwa "kuanzia leo mimi na wewe basi" alipo nitamkia sentence iyo tu tangu siku iyo hakuwai kuona sms wala calling yangu, nilifuta taarifa zake zote kwenye kitarakilishi changu (computer na simu) sikutaka kabisa kumsikia ila moyoni nilikuwa na maumivu yaliokuwa ykiwaka moto mzito,

atimaye amemtafuta mtu wangu wa karibu na kuomba kuonana na mimi ili tuongee, lakini main pont yake kuu ni kutafuta suruhu kwa kilicho tokea katikati yetu (usaliti alio nifanyia), uyu binti aliniachia maumivu makali sana wana JF, nilimpenda na kumthamini sana kwa kila kitu ila aliamua kwenda.

wakuu, uyu binti napanga siku ya kuonana nae nifanye nini (niongee nae nini, nimpangeje ili baadae nije kumpiga tukio zito), maana nahisi moyo wangu una hasira na chuki juu yake kama mbogo, ila sizionyeshi kwake waziwazi, nataka nimpitishe kwenye ziwa la miiba ili atakae kuja kumuoa uyu binti basi binti awe na adabu na heshima.

NINI NATAKA KUTOKA KWENU:

uyu binti nataka nimuweke kwenye mazingira ambayo afurahi kuwa na mimi uku nikimuandalia tukio lake la surprise.

natamani nipate experince kwenye issue ya X wako kurudi ulimpa adhabu gani kuu, ambayo atokuja kuisahau (sio kumdhuru kimwili noo).

Najua watakakuja watu hapa na kusema samehe na sahau, No ilo nalijua
28 October:

Tayari umeshafanya maamuzi. Ila kisasi ni cha Mungu. Hilo tatizo unaloliongeza ni kubwa kuliko la mwanzo. Lazima tujifunze kuwa wavumilivu katika kila hali kuliko kuiangalia hali yenyewe kuwa ni tatizo.

Kumbuka hata wewe watu wanakuvumilia na hawajawahi kukuchoka.

Kila la kheri mkuu🙏
 
Mtu unafikiria kufanya kisasi kwa mwanamke ili iweje sasa!, akiumia wewe pesa zinaongezeka?. Endelea mbele hakuna kurudi nyuma. Kama mlimalizana imekwisha hio,just move on. Unaweza kumfanyia halafu hata asiumie ukaona anaendelea na maisha fresh tu, utaumia mara sita. Kisasi kikubwa kwake ni wewe kumove on,ukiwa na furaha bila yeye.
 
MADHARA YA KULIPA KISASI

"Wapenzi, msijilipizie kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu Mimi, Mimi nitalipa, anena Bwana" (Warumi 12:19)

Kuna hasara zinazoweza kukupata ukiamua kulipa kisasi kwa mambo uliyofanyiwa ambayo hayakupendezi. Ikiwa ni masuala ya kikabila, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kidini, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kifamilia, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kikazi, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya uhusiano wako na majirani zako, usilipe kisasi.Ndiyo! Usilipe kisasi! Kwa nini? Kwa sababu "imeandikwa kisasi ni juu yangu Mimi; Mimi nitalipa, anena Bwana".

Lakini ikiwa utaona ya kuwa Mungu hawezi kukusaidia na ukaamua kujichukulia madaraka ya kujilipiza kisasi hasara zifuatazo hakika zitakupata!

Hasara ya Kwanza "UTASHINDWA!"
Katika jambo lolote lile lililokukasirisha - liwe la kidini, au kikabila, au kifamilia, au kikazi, na kadhalika ukiamua kulipa kisasi utashindwa wewe kwa sababu vita hivyo si vya mwili na wala silaha ambazo Mungu amekupa si za mwili! Tunasema hivi kwa sababu katika 2 Wakorintho 10:3- 5 imeandikwa hivi:"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi yamwili; maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo".
Tena katika kitabu cha Waefeso 6:12 imeandikwa hivi: "Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho".

Uwanja wa mapambano uliyonayo ni "katika ulimwengu wa roho" na mapambano uliyo nayo "si juu ya damu na nyama" - ingawa unaona ya kuwa ni watu na ni binadamu kama wewe wanaokusonga - lakini fahamu hili ya kuwa wanatumiwa tu na ibilisi!

Mbinu mojawapo ya shetani anayotumia akitaka kukuangamiza ni kukufanyia kitu kitakachokukasirisha ili uamue kujibu au kushindana kimwili kwa sababu anajua ukishindana "kimwili" au katika mwili utashindwa hakika, maana vita hivyo si vya mwili wala silaha ambazo Mungu amekupa si
za mwili!

Hasara ya Pili "MATATIZO HAYATAKWISHA!"
Kumbuka imeandikwa hivi katika kitabu cha Wagalatia 6:7; "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote ampandacho mtu. Ndicho atakachovuna".

Ikiwa umeamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule aliyekufanyia - ubaya hautakwisha, kwa sababu utavuna ulichopanda.Ndiyo maana imeandikwa hivi:"Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, mabaya hayataondoka nyumbani mwake" (Mithali 17:13)

Ukiamua kulipiza kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nyumbani mwako - Biblia inasema "mabaya hayataondoka nyumbani mwako" Hii ndiyo maana matatizo mengi katika ndoa na katika jamii hayaishi - kwa sababu mtu akifanyiwa ubaya naye analipa kisasi.Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nchini mwako ujue hakika mabaya hayataondoka nchini mwako. Hili ndilo lililowapata wenzetu wa nchi za Burundi na Rwanda - kulipizana kisasi - matokeo ni uhasama usiotaka kupotea - pamoja na juhudi zote za kimataifa kutafuta suluhisho.

Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa kazini kwako - fahamu mabaya hayataondoka kazini kwako. Ikiwa ni shuleni - mabaya hayataondoka hapo shuleni.

Tena hali ya mwisho inakuwa mbaya zaidi,kila wakati kisasi kinapoendelea kupandwa. Kwa sababu ukiwapa watu ubaya - nawe utapewa ubaya kwa; "kipimo cha kujaa na kushidiliwa, na kusukwa sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile upimacho ndicho mtakachopimiwa" (Luka 6:38)
Kumbuka ubaya haushindwi na ubaya mwingine, bali unashindwa na wema kama vile dawa ya chuki si chuki bali upendo! Ndiyo maana Warumi 12:21 inasema; "Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema".

MUNGU NA AKUBARIKI SANA.....
 
Habari wana bodi,

Niende moja kwa moja kwenye maada tajwa hapo juu, ni miezi takribani 3 tangu aliyekuwa mpenzi wangu (x-girlfriend) aliponiacha kwa kunitamka kuwa "kuanzia leo mimi na wewe basi" alipo nitamkia sentence iyo tu tangu siku iyo hakuwai kuona sms wala calling yangu, nilifuta taarifa zake zote kwenye kitarakilishi changu (computer na simu) sikutaka kabisa kumsikia ila moyoni nilikuwa na maumivu yaliokuwa ykiwaka moto mzito,

Hatimaye amemtafuta mtu wangu wa karibu na kuomba kuonana na mimi ili tuongee, lakini main pont yake kuu ni kutafuta suluhu kwa kilicho tokea katikati yetu (usaliti alionifanyia), uyu binti aliniachia maumivu makali sana wana JF, nilimpenda na kumthamini sana kwa kila kitu ila aliamua kwenda.

Wakuu, huyu binti napanga siku ya kuonana nae nifanye nini (niongee nae nini, nimpangeje ili baadae nije kumpiga tukio zito), maana nahisi moyo wangu una hasira na chuki juu yake kama mbogo, ila sizionyeshi kwake waziwazi, nataka nimpitishe kwenye ziwa la miiba ili atakae kuja kumuoa uyu binti basi binti awe na adabu na heshima.

NINI NATAKA KUTOKA KWENU:

Hyu binti nataka nimuweke kwenye mazingira ambayo afurahi kuwa na mimi uku nikimuandalia tukio lake la surprise.

Natamani nipate experince kwenye issue ya X wako kurudi ulimpa adhabu gani kuu, ambayo atokuja kuisahau (sio kumdhuru kimwili noo).

Najua watakakuja watu hapa na kusema samehe na sahau, No ilo nalijua
Kula nyuma
 
Namuonea huruma huyo binti.

Wanawake wanatakiwa kujua kua wanaume ni watu wa visasi, ukimuacha mwanaume usirudi tena.

Sasa binti wa watu amejileta kwenye maumivu mwenyewe halafu atakuja kulaumu wanaume wote baadae kua hawafai.
 
Mkuu hao viunge wanajua kupindua shilingi muda wowote,, usiweke dhamana sana, Wewe shukuru umeachwa na hujafa..

Hicho unachoenda kufanya sasa hivi ndio unaenda kujichimbia kaburi, atakufanya kitu hujawai fanywa..

Utanishukuru baadae
 
Back
Top Bottom