Mpenzi wangu alinifumania, ananichanganya!

Mpenzi wangu alinifumania, ananichanganya!

alinifumania lile fumanizi ambalo halina kupinga! yani fumanizi la 100 percentage..
zikapita siku mbili hanitafuti nami nikawa kimya namawazo sijui naanzia wapi kujitetea,nikaona isiwe tabu nikaenda kulanduka na Serengeti lager kama 5 hivi kisha nikampigia simu!.

Nikajua hata atakuja juu lkn mtoto wa watu ndo kwanza akawa mpole kama maji ya kwenye mtungi!.. baada ya salamu nikamuuliza "umenisamehe..?" akacheka kidogo halafu akakaa kimya.
nikamuuliza tena "au ndo umeniacha tayari..??"
akavuta pumzi akajibu
"nimekuacha na sijakuacha pia!" hapohapo akakata simu!
nikapiga tena akaniuliza nini..? nikamuambia "Nakupenda"
akajibu "Nakupenda na sikupendi pia".

nipo matatani ananichanganya sana sielewi hapa majibu yake mawili mawili yaninitia sonona na mtanziko wa mawazo! kwa ambae amekutana na swahibu kama hili ulifanyaje kuyaweka mambo sawa ,kijana wenu penzi bado nalitaka maana mtoto miuno kama feni bovu!.
Wacha UFALA endelea kula pombe Mzee wangu akili itakaa Sawa.
 
Back
Top Bottom