Mpenzi wangu ana mahusiano na kaka yangu wa damu

Mpenzi wangu ana mahusiano na kaka yangu wa damu

Pole mkuu. Tafuta ushahidi kama wana mahusiano kisha wapoteze.
 
Nilianza mahusiano na huyu binti mwaka juzi mwezi wa kumi na mbili. Mwaka 2019 Nikiwa semester ya mwisho kabla ya kumaliza chuo nilipata supplementary ambayo mwalimu alichelewa kutoa matokeo, akaja kutoa siku moja kabla ya graduation hivyo jina langu halikuwepo kwenye list ya graduates iliyopitishwa na senate. Nikaambiwa niandike barua then nitaingizwa kwenye list mwaka unaofuata.

Ulipita mwaka mzima, siku chache kabla ya graduation ya mwaka uliofuata ambao ndio nilipaswa sasa nigraduate ilitoka list ya mwaka huo lakini jina langu halikuwepo. Ikanibidi niende chuoni kufuatilia.

Nilipofika chuoni na kuanza kufuatilia ndipo nilipokutana na binti huyu. Kiufupi yeye na mimi tulikuwa kwenye the same scenario na yeye hakuwemo kwenye list pia. Tulikutana kama bahati tu nikiwa kwenye kundi la watu nje ya ofisi ya head of department ambaye hakuwemo ofisini, nilishangaa binti mmoja mchangamfu ananifata moja kwa moja akiwa amenyoosha simu yake akanipatia na kuniambia

"Ongea na head of department mwambie tunamsubiri huku ofisini mimi naogopa"

Niliipokea ile simu na huo ndio ukawa mwanzo wa kujuana. Tulibadilishana mawasiliano na baadaye mahusiano yakazaliwa. Nilimpenda sana yule binti ukizingatia sikuwahi pata binti mzuri na smart kama yule maishani mwangu. Kwa bahati nzuri alipata kazi mkoa wa nyumbani kwetu ambako mimi pia ndio ninaishi. Ila yeye akawa anakaa wilayani mimi nakaa mjini. Kuna siku nikiwa kaka yangu yangu ambaye yuko likizo home huyu binti alinipigia na katika maongezi akaniuliza uko na nani nikamjibu niko na kaka yangu akasema hebu mpe simu nimsalimie sikuona shida nikampa wakaongea ila maongezi yalikuwa ya kawaida tu. Niwe muwazi hapa huyu kaka yangu huwa simpendi kihivyo kwa sababu ana tabia ya kuniongelea vibaya hivyo namheshimu tu kwa sababu ni ndugu.

Sasa juzi kuna shosti yake na huyu binti wanafanya kazi sehemu moja alinitumia picha whatsapp ambayo ni ya kaka yangu na kuniuliza kama ninamfahamu, nikamwambia huyo ni kaka yangu je picha yake umeitoa wapi? akajibu amenionyesha Frida (sio jina halisi) ambaye ndio huyo mpenzi wangu. Nilipata mashaka yeye na kaka yangu wamefahamiana vipi wakati wameongea kwa simu tu. Kiukweli mimi huwa sina tabia ya kumuamini mtu yeyote mpaka hapo nikahisi kuchapiwa. Nikawa namfatilia bro kimachale. Kuna siku bro alikuwa anaongea nje ya nyumba na simu nikamfatilia lakini katika maongezi nikabaini anaongea na huyu huyu binti. Usiku wa jana mida ya saa mbili ndio nimeona txt kwenye simu ya bro simu ikiwa lock ila ikaingia txt ya namba ya huyu binti. Txt inasema nanukuu

" Kweli bora niachane nae tu"

Nimemuuliza rafiki yake aliyenitumia picha hajafunguka ila kaniambia tu

" hayo ndio maisha Pacbig"

Nimeumia sana sijajua hata cha kufanya ila I think this is going to be the end of our brotherhood between me and my brother, I hate him more than I hate a devil.
Mbususu kitu kingine jamani. Dah! Wee huyo demu wala usiumize kichwa..wee piga na bro nae apige basi maisha yanaendelea
 
Cha kufanya wewe ndo uanze kumpiga chini na usimpe sababu. Ukipigwa chini wewe utaumia zaidi
Mweee hapa dawa nijamaa aombe game alafu katikati ya game ajidahi amekosea tobo
 
Usikubali mwanamke avunje undugu wenu,
Tambua mwanamke Ni wakupita,undugu wenu wakudumu
 
Achana na huyo Mwanamke siyo mwaminifu songa mbele maisha yaendelee.
 
Muache uyo dem kabla aja kuacha utani kumbuka, maumivu ya kuachwa ni tofauti na ya kuacha.na maumivu ya kuachwa ni makubwa ata kama alie kuacha ulkua na mpango wa kumuacha [emoji81][emoji81]
 
Pole mkuu, huyu mwanamke asiharibu undugu au heshima kati yako wewe na brother wako. Piga chini kwa hekima, kaa na bro kiutu uzima. Undugu na heshima ni muhimu zaidi kuliko huyo mwanamke. Sio mwaminifu huyo mwanamke...
Jinamizi hilo linawatia majaribuni kaka bora uachane nae kuliko kuvunja udugu, "ndugu atabaki kua ndugu ht km ni mwanga"
 
aliyemkuta mwenzake kwanza ndio akae pembeni!

mtihani: jaribu kufuatilia nani kati yenu alikuwa wa kwanza.

kaa karibu shosti ake na Frida, anajua zaidi! ila kama unakifua na muda wa kupoteza!

msichukiane, you are badboys for life! 👊
 
Piga chini huyo kicheche,usivunje undugu Ila huyo kaka yako mwambie kuwa alichokufanyia siyo fresh na mwambie kuwa umeamua kumuachia hilo bomu ahangaike nalo kwani na yeye atakuja kulizwa tu
 

Huwa nashangaa sana mtu akisimulia kisa kama hiki na akimalizia kwa kusema hajui cha kufanya, hujui ufanye nini?
 
Back
Top Bottom