Kuna msichana nimekuwa nae kwenye mahusiano kwa muda wa miezi 7 sasa na siku kadhaa.
Na tulipanga hapo baadae tuje tuwe na mwisho mzuri (ndoa)
Katika kipindi chote hicho ambacho tulikua pamoja tuliweza kuwa na furaha japo pia kukwazana kupo kama binadamu, lakini tulikua tunaongea yanaisha na kurudisha uelewa kati yetu.
Pia tangu nimekua nae, baada ya muda nilianza kukagua simu yake, ili kuangalia je? Kama mwenzangu kweli ana nia na mimi au yeye ana mambo yake mengine anayowaza na watu wengine.
Katika hatua hiyo ya ukaguzi wa simu yake nilishawahi kukuta baadhi ya sms za mapenzi, ikiwa ni namba ngeni kabisa ndio iliyoingia zinaongoza kutuma kutuma sms hizo kwenye simu yake, na nilipojaribu kumuuliza mwenzangu yeye alijaribu kujitetea kwa kusema hizo namba hazifahamu na kudai tu ni watu ambao wanataka kumuharibia mahusiano.
Pia kuna uzi ambao nishawahi kuleta hapa kuhusu kutoelewana mimi na yeye, kutokana na simu ambayo nilipokea wakati wa usiku na huyo mtu alidai kwamba anamfahamu huyu msichana kuliko hata mimi ninavyomfahamu, na pale nilipomuasha usiku kujibu madai ya huyo mtu alianza kulia usiku hadi mida ya saa tisa(9) usiku akidai ya kuwa namuonea tu, lakini yeye hamfahamu.
Baada ya hapo hivi, juzi wakati naangalia whatsapp yake nilikuta chat ambazo ameweka password, lakini nilianza kuhisi pia kuna kitu hakipo sawa.. Baada ya hapo nilimuuliza kuhusu chat hizo lakini yeye alidai ya kuwa nisiwe na wasi wasi kwani hakuna baya linaloendelea.
Na ndipo siku ya jana nilimsihi sana atowe password hizo ili niangalie vitu hivyo ambavyo anachati na wao watu.
Sasa katika kubishana nilifanikiwa kuchukua simu ile ili aniambie password za kwenye zile chat, lakini aligoma.
Hivyo niliamua kuondoka na ile simu mpaka pale ninapokaa, na yeye kunifuata baadae... Pia hapo nyumbani tulibishana kwa muda sana, lakini aligoma kutoa password.... Ndipo aliponiambia nimpe simu ili atoe Mwenyewe hizo password... Kwa kuwa nilishahisi kuna vitu ambavyo anaficha na lazima vitakuwa ni viovu, niliamua kumpa simu yake.
Baada ya kuchukua simu, hakutoa zile password, ila badala yake aliamua kufuta zile chat zote... Hivyo kwa kuwa alifanya vile kwa makusudi, nilimuamuru aondoke zake. Lakini pia aligoma kuondoka... Hivyo nilitumia nguvu kumuondoa apo nyumbani kwa kuwa nilishahisi tu mambo yanayoendelea sio mema hata kidogo.
Hivyo leo alinisihi sana tuongee yaishe... Lakini kabla ya hapo kuna maswali nilitaka kumuuliza na katika kumbana sana niligundua mmoja kati ya wale watu aliokuwa akiwasiliana nao ni bwana wake wa kwanza kama alivyodai(ex boyfriend) na hawa wengine alidai tu, ni watu ambao wanamtongoza tu lakini hawajui...
Na kwa kuwa nilishaanza kumchunguza muda sana alisema ukweli wote
Sasa mimi binafsi nilimuambia ya kuwa sina tena imani na wewe, akaanza kama kawaida kulia usiku kucha, anadai nimsamehe...
Je wakuu hapo ingekua imetokea kwa upande wako ungefanyaje?