Wakuu salama? Leo naona hali ya hewa kama imechafuka ghafla baada ya huyu dada kunambia habari za pisi yangu aka mchepuko.
Leo tulikua wote akaniuliza kwa utani “sarah” ni nan kwako nikamwambia simjui nilishtuka kidgo akanionesha na picha zake alizopost jana status akanambia sindo hyu ? Nikaangalia nikamwambia simjui.
Raha ya mwanamke akiwa na kitu ili akitoe unatakiwa ujibu shit ili apte hasira sasa hapo ndo akaanza funguka kwanza mtu mwenyew unambadilisha badilisha majina mara sarah, mara umsave ya kiume unaficha nini? Na kilichonishtua jana nimechange jina nikaandika “mbeba taka” akanambia sahivi umemsave mbeba taka hapa ndo nikahisi huyu bibie kanihack kajuaje? Na simu yangu ina password na face ID juu na kwa sasa niko nae anaweek 2 hapa kwangu.
Chats nazochat nae mpaka majina ya utani nayomwita mchepuko wangu ananambia yote nayomwita na tulikua na ratiba ya kwenda Zanzibar kanambia yote sasa najiuliza kajuaje hapa ndo sielewi na yeye kasema atadeel na huyu mchepuko papendicular hii vita siwez ingilia mimi ila nimekataa katukatu kwamba sijui anavyoongea.
Ndugu wanaume nisaidieni dada anapataje taarifa na sim yangu hashiki kabisa. Nimejiuliza sana au anavizia nikilala anascan face ID? Lakin face ID ukifumba macho haisense natumia iphone.
Haya yote yameanza baada ya kuja kwangu toka chuo kifungue na alisema kama namwanamke mwingine atajuaa tu hizi kauli zake ndo nmezikumbuka leo[emoji28][emoji119][emoji119]. Sijui dada anatumia mbinu gani nisaidiein. Huu mchepuko unanipa mapenzi motomoto nyie[emoji119]