Mpenzi wangu hataki kunielewa juu ya kosa langu

Mpenzi wangu hataki kunielewa juu ya kosa langu

Ndugu zangu humu wa zima? Natanguliza samahani. But nachohitaji ni ushauri.

Mimi ni kijana napitia changamoto katika mahusiano yangu kama mnavyojua mapenzi yanavyoumiza hasa pale mtu unayempenda akichokwa na tabia zako na akafanya maamuzi ya kuvunja uhusiano, na wakati bado unamuhitaji, naandika haya kwa uchungu😭😭😭

Mahusiano yetu yalianza vizuri tu na tukaenda vizuri ila shida ilianzia kwangu, nilikuwa napenda sana nimtengenezee mwenzangu wivu ili asijeniacha na kitu nilichokuwa nafanya ni kupost picha za msichana mwingine na hii nilikuwa naifanya pindi mwenzangu akinikosea ila hii tabia mwenzangu ilimkera sana but sikuweza kushtuka nikajiona niko sahihi na nimefanya hiyo tabia ya kumpost huyo msichana mwingine kwa nyakati 3 tofauti

Sasa hii ya tatu mwenzangu ameona imezidi ameamua kuniacha karibu mwezi, sasa mawasiliano yetu sio mazuri baina yangu na yeye, kinachoniuma zaidi huyo dada niliyekuwa nampost siko nae kwenye mahusiano.

Mpenzi wangu hataki kunisikia hataki kuiniona ananiona mimi muongo muongo ila baada ya mambo kuwa magumu nimeamua nimueleze ukweli wa juu ya hicho ninachokifanya cha kupost huyo dada ila mwenzangu ndio hivyo hataki kunielewa

Sababu zilizonifanya niwe nampost huyo dada ni

1. Kumtengenezea mwenzangu wivu ili asije niacha

2. Akinikosea nilikuwa nampost ili walau aniulize huyo nani ili nipate chance ya kuchat nae

Maamuzi niliyochukua ni

1. Kuomba msamaha

2. Kuonesha ushahidi kuwa huyo msichana siko nae kwenye mahusiano

3. Kukutana na mchumba wangu ambae nimemkosea ili nimuelezea A-Z kipi hasa kinanifanya nafanya hivi
ila ndo hivo mwenzangu asilimia za kuniamini zimepungua amepunguza uaminifu juu yangu

4. Nimepanga safari ya kusafiri kutoka mkoa wa Katavi hadi Dodoma ili niweze kukutana nae tuzungumze hili suala japo % za kuweza kukuta ni mdogo maana bado mwenzangu ana wasiwasi na mimi ila mimi nimeamua niende hivyo hivyo japo sijui itakuaje

Nimeamua kuondoka na kumtafuta ili nifanye suluhu japo kipato changu kidogo ila nitajibana mpaka nifike huko tujadili haya mambo

Nisaidieni mawazo na namna sahihi ya kuweza kulimaliza hili suala langu

Mwenzangu mpenzi wangu yuko humu ni member sitapenda nitaje jina lake.

Kama atasoma haya maelezo nataka ajue nampenda sana na sipendi nimpoteze❤️❤️

Napitia kipindi kigumu cha mateso makali😭😭😭😭😭 mawazo , mambo yangu hayaendi muda mwingi natumia kuwaza haya tu😭😭 kazi zimesimama nakonda na ulaji wangu umekuwa sio mzuri kabisa😭
Umri wenu ni gani?!
 
Duh!!! Tena angekunyoosha uliporusha picha mara ya kwanza.. Ila huyo uliyemposti nani wako? Alikupa ruksa ya kutumia picha yake? Hana bwana?..
Usiumie, wewe beba tu machungu ya makosa yako. Hivi huyo uliyekuwa unimportant yeye hujamsababishia shida.!? Halafu wivu haujengwi hivyo..!! Na wivu ni natural siyo wa kupanga..!

MTAFUTE ULIYEKUWA UNAMPOSTI AKAKUSAIDIE KUOMBA MSAMAHA..!!! Lakini na yeye umuandalie maelezo yenye mashiko
 
nimemsababishia matatizo maana mchumba wake alinitafuta nikamuelewesha akanielewa na sasa ivi wako vizuri tu

hapo kwenye kumtafuta huyo mtu natamani nifanye hivo ila bado huyu mpenzi wangu haniamin anaona nitaishia kumdabgaya
 
Lady Jaydee was right aliposema kuna wanaume kama mabinti.. at more than 25yrs bado unatengeneza wivu through posting? Total childish behaviour. Na sijui nan alikufundisha mahusiano.

My take is, hata akikusamehe, tayri ashakuona mtoto na hujakomaa kiakili so automatically heshima itashuka kwa kiwango cha 5G. Na kwa mwanaume, mwanamke wako akishakukosea heshima, unapoteza muda wako tu. Kinachofuata ni nyundo nzito.

Alaf pia, kama yuko humu, bado umejianika uchi sokoni, maana ataona pia hili lipost lako na ushauri unaopewa, so watever u do, ataona pia umeshindwa kuamua kama mwanaume but unaendeshwa na mawazo ya jamii.
My nigga, stand on ur stance kama mwanaume, go there, mchane live kuhusu ujinga wako na uskie atachoamua. Akileta usoro, vaa viatu pita hivi. Heri kufa ukiwa umesimama wima rather than kuishi on your knees kama kondoo.

Know your worth and take responsibility for your actions.
Wahed mkubwa!🤬
 
Mbadala wako ukisha Anza kutafutwa tangu ulipo post Mara ya pili na amepata .... Kikubwa kwa Sasa unategemea huyo Alie mpata anamalengo gani nae yakinoga huko mzee ndio Basi tenaa. Yakiharibika huko labda anaweza kurudi.

Bro na ulipo muambia ukweli ndio umeharibu kabisa yaani ndio amekudharau vilivyo na ukienda huko Dom ndio atakutapika kabisa.

Mwanamke ni Kama mbwa wa ndani siku akitoka nje ya gate ukianza kumfukuzia kumrudisha ndio atakimbia mbali zaidi akijua mnacheza. Ila ukamuigno na kurudi ndani nae atarudi ....Sasa wewe unacho kifanya ni kumkimbiza hapo tegemea atakimbia mbali zaidi na nadhani dalili za kukimbilia mbali zaidi umeanza kuziona.

Shortly bro ndio umesha achwa kubali tu Wala usiendelee kutumia pesa na Mali kuharibu.

Hutaki jifanye mjuaji
 
Sijui kwanini nacheka ila ngoja nicheke kwanza[emoji38]
Anyway pole sana natumaini mwnye mpenzi wake ataona hii…
Dahhh!!mi mwenyewe apa imenibidi nicheke kiukweli daaah!yote mema mpenzi wake kama yupo humu chonde chonde naomba karibu kumuelewa mwenzio Ili mambo yaende jaman...
 
Punguani

Unacheza kombolela na mtu mzima.
Acha utoto mkuu.

Michezo ya kitoto ni ya watoto, watu wazima wanamichezo yao kuimarisha ndoa zao. Kama huijui ni pm.
 
We ni mshamba wa Mapenzi sema hilo ni funzo. Siku ingine uache tabia za kitoto hizo maswala ya kuvimba vimba kisa unaona demu anakuelewa sana uachege.
Demu mkipishana kidogo unampost demu mwengine kumkomesha. Huo ushamba, achia watoto wa la 7
 
Kama ni Mwezi.. na upo katavi yeye yupo dodoma..
kwa utoto ulioufanya kwa mwanamke huyu.
Na nature ya watoto wa kike. Mzee umeachwa miezi miwili iliyopita kabla wewe hujajua. Usiende huko utateseka zaidi.
 
Ndugu zangu humu wazima? Natanguliza samahani. But nachohitaji ni ushauri.

Mimi ni kijana napitia changamoto katika mahusiano yangu kama mnavyojua mapenzi yanavyoumiza hasa pale mtu unayempenda akichokwa na tabia zako na akafanya maamuzi ya kuvunja uhusiano, na wakati bado unamuhitaji, naandika haya kwa uchungu😭😭😭

Mahusiano yetu yalianza vizuri tu na tukaenda vizuri ila shida ilianzia kwangu, nilikuwa napenda sana nimtengenezee mwenzangu wivu ili asijeniacha na kitu nilichokuwa nafanya ni kupost picha za msichana mwingine na hii nilikuwa naifanya pindi mwenzangu akinikosea ila hii tabia mwenzangu ilimkera sana but sikuweza kushtuka nikajiona niko sahihi na nimefanya hiyo tabia ya kumpost huyo msichana mwingine kwa nyakati 3 tofauti

Sasa hii ya tatu mwenzangu ameona imezidi ameamua kuniacha karibu mwezi, sasa mawasiliano yetu sio mazuri baina yangu na yeye, kinachoniuma zaidi huyo dada niliyekuwa nampost siko nae kwenye mahusiano.

Mpenzi wangu hataki kunisikia hataki kuiniona ananiona mimi muongo muongo ila baada ya mambo kuwa magumu nimeamua nimueleze ukweli wa juu ya hicho ninachokifanya cha kupost huyo dada ila mwenzangu ndio hivyo hataki kunielewa

Sababu zilizonifanya niwe nampost huyo dada ni

1. Kumtengenezea mwenzangu wivu ili asije niacha

2. Akinikosea nilikuwa nampost ili walau aniulize huyo nani ili nipate chance ya kuchat nae

Maamuzi niliyochukua ni

1. Kuomba msamaha

2. Kuonesha ushahidi kuwa huyo msichana siko nae kwenye mahusiano

3. Kukutana na mchumba wangu ambae nimemkosea ili nimuelezea A-Z kipi hasa kinanifanya nafanya hivi
ila ndo hivo mwenzangu asilimia za kuniamini zimepungua amepunguza uaminifu juu yangu

4. Nimepanga safari ya kusafiri kutoka mkoa wa Katavi hadi Dodoma ili niweze kukutana nae tuzungumze hili suala japo % za kuweza kukuta ni mdogo maana bado mwenzangu ana wasiwasi na mimi ila mimi nimeamua niende hivyo hivyo japo sijui itakuaje

Nimeamua kuondoka na kumtafuta ili nifanye suluhu japo kipato changu kidogo ila nitajibana mpaka nifike huko tujadili haya mambo

Nisaidieni mawazo na namna sahihi ya kuweza kulimaliza hili suala langu

Mwenzangu mpenzi wangu yuko humu ni member sitapenda nitaje jina lake.

Kama atasoma haya maelezo nataka ajue nampenda sana na sipendi nimpoteze❤️❤️

Napitia kipindi kigumu cha mateso makali😭😭😭😭😭 mawazo , mambo yangu hayaendi muda mwingi natumia kuwaza haya tu😭😭 kazi zimesimama nakonda na ulaji wangu umekuwa sio mzuri kabisa😭
Aliyekuambia wivu unatengenezwa nani? Wivu huja automatically pale palipo na mapenzi ya kwelii? Halafu uko Kwenye mahusiano badala ya kufanya bidii katika kuimarisha mahusiano yako wewe umekomaa kuwaza usiachwe, hujui kuachwa kunatokana na uzembe, uvivu na ulegevu katika mahusiano yako. Halafu kabisa unapost picha ya msichana mwingine huo ujasiri uliutoa wapi? Unapaswa ufungwe jiwe shingoni utupwe baharini
 
Back
Top Bottom