Kumbe vodacom Tanzania wezi kiasi hicho,nilipanga kufanya manunuzi mtandaoni kwa kutumia mpesa,loo! sasa wamenikosa acha wakae na wizi wao.Ngoja nijaribu Airtel.
Pole sana Mkuu,
Ila mimi nimefanya transactions mingi tu kwa M-pesa MasterCard na sijakutana na shida yoyote.
Mara nyingi nimekuwa nikilipia manunuzi haswa AliExpress.
Tano ndogo sana..... Hapo akicalculate damages kwa jumla anaweza ondoka na milioni 20. Ila apate wakili mzuri.Mzee tafuta wakili nenda mahakamani iyo ishu kuna dalili ya kupata milion 5 hapo
Safari tunayo ndefu mnoMimi sina hamu naooooh wameniharibia hadi mahusiano yangu na seller jamaa kaona nazingua na kumpotezea muda tu na akaamua kuniblock!!!Sina hamu na hawa voda kbs!View attachment 1523276
Sio kweli hao uzoefu hawana .Pesa ikiondoka haiwezi elea angani.Ukiona salio limepungua hiyo ilishatoka na kutua ardhini inatakiwa uidai toka ilikotua Sio Vodacom
Halafu Vodacom haiwahusu wenye mtandao wa Master card Ndio waweza just what happened
Mleta mada wasiliana na Master card wenyewe
Usiwe na maneno mengi andika tarehe hii hapa nilifanya malipo kwa kampuni hi hapa kwa kutumia master card yenu namba hii.Hela wanasema hazikufika wakati kwenye card yangu namba hii hii hell kwangu ziliondoka .Watakusaidia chap chap.Nenda website ya master card.Ila andika kifupi Sio Hadith ndefu go direct to the point.Sababu hizo customer care zao huwa busy kuliko kawaida be short and clear usiandike hotuba
Kuhusu kuandika kwa hicho Cha kuchafua Vodacom kila eneo kwa kitu usichpjua kwa uhakika waweza ishia jela na kudaiwa mabilioni kwa kuchafua kampuni
Dai Hali yako kwa adabu na heshima na usijifanye una uhakika Sana kuwa tatizo liko Vodacom!! Pesa uruhusu wewe ziondoke Halafu. Uwakomalie Vodacom
Sema wao Wana huruma ningekuwa Mimi ndio MD saa hii ungekuwa unakiona Cha mtema kuni mahakamani
Mnachoshindwa kuelewa ni kuwa Vodacom wanawajibika kwa kukubali kwao kuwa hela ipo pending na itarudi baada ya siku kadhaa, mpaka sasa hawajakataa kuwa hela haipo kwao.Mkuu nadhani tatizo ni kwamba umepigwa na sehemu uliyonunua hio website na pesa imewafikia ila wamekutandika. Sidhani kama vodacom wana tatizo lolote.
Siku nyingine Tumia paypal kulipia vitu online kwa kutumia kadi hii itakuwa ni kama ngao,
Hapo hakuna msaada, Ni vyema tu labda ungeweka wazi ni softwarw gani ulitaka kununua katika website ipi maana kuna wevsites kibao ambazo ni feki.
Binafsi natumia hii huduma kwa muda mrefu tu nmeagiza vitu, Kulipia software, kulipia services kama website na vitu kibao bila tatizo lolote.
Sio kila mtandao wa kulipia kwa kadi bila paypal, Hakikisha unajiunga na paypal kulipia vitu, Ukilipia kwa kadi directly ukipata hasara hio ni juu yako wewe,
Ulinunua softwarw gani kwa hio lako 4 na website ni ipi???
Waambie voda ili wampe jamaa hilo jibuAcha kulalamikia vodacom wakati tatizo ni wewe uliyetuma pesa kwa mtandao ambao sio genuine.
Vodacom wapo vizur mno kwenye hio huduma yao ya mpesa mastercard.
Nishawahi nunua kitabu ciscopress ikabaki kama laki moja hivi kwenye account ya mastercard nikawa nimeiacha hio pesa tu.
Juzi account yangu ime expire nikarudishiwa pesa yangu kwenye mpesa.
Aliyekupiga ni yule uliyemtumia pesa sio vodacom
Card zangu zote za crdb MasterCard na VisaCard zinagoma zinataka nijaze securecard nazo crdb huduma kwa wateja hawaelewi naambiwaga utapokea sms yenye code ndio hakuna lazaidi....Yan ile kwenda kwenye tawi pia kwangu ni changamoto.Tumieni benki kufanya malipo ya mitandaoni, huko kwenye makampuni ya simu siku ukipatwa na tatizo lolote hutamuona wa kukupatia msaada wa haraka.
Hakunaga hela inayoganda hewani kweny hio miamala, Imepewa tu jina la mpesa master card lakini mwenye nayo ni benki inaitwa banc abc. Kwa ambao tuna uzoefu na hizi ishu kwa miaka mingi tunajua tatizo lipo kwa alienunua hivyo vitu.Mnachoshindwa kuelewa ni kuwa Vodacom wanawajibika kwa kukubali kwao kuwa hela ipo pending na itarudi baada ya siku kadhaa, mpaka sasa hawajakataa kuwa hela haipo kwao.
Wangekataa mapema, mlalamikaji angetafuta namna nyingine ya kupata fedha yake.
Kwa hiyo awe ameibiwa na wanaijeria, wachina nk bado Voda wanawajibika kumlipa kwa kuwa wamekubali na kumuaminisha mlalamikaji kuwa kosa lipo kwao na fedha yake watamrejeshea.
Kwa hilo hawachomoki
Hao crdb wana mlolongo mrefu sana, kuna kipindi mwaka 2014 nilizungushwa miezi mingi sana mpaka mwaka 2015 hamna kitu zaidi ya kwenda tu ofisini kwao na kusainishwa fomu kila nikienda.Card zangu zote za crdb MasterCard na VisaCard zinagoma zinataka nijaze securecard nazo crdb huduma kwa wateja hawaelewi naambiwaga utapokea sms yenye code ndio hakuna lazaidi....Yan ile kwenda kwenye tawi pia kwangu ni changamoto.View attachment 1523423View attachment 1523422
Tofauti ya bank na mitandao ya simu ni aina ya kadi na matumizi yake tu.Bank inatoa Solid Card ambayo unaweza kuitumia mtandaoni, ATM na kwenye mashine zingine zakuchanja card.Mitandao ya simu inatoa virtual card ambayo huegemea matumizi ya mtandaoni tu online.Upatapo tatizo utaenda kwenye ofisi zao kumbuka hata kuhamisha miamala ilikuwa ni dhughuli za bank tu now simu ndio njia mbadala...Tatizo la hawa mitandao ya simu Huduma kwa wateja hawajawaweka watu wa Kibank wanaojua mambo hayo ya MasterCard VisaCard.Mtu aliyesomea mambo ya telecommunication ndio huyo anatakiwa atatue mambo za Bank hili ni tatizo....Pia hii mambo ya online Shopping/payment hata hao Bank hawana wataalamu wa kutosha yan mhudumu anakuuliza PayPal ni nini.Hili suala la ni geni kwa watoa huduma taasisi na kampuni zote tz pia ni geni kwa wateja wao ambalo ndio huishia kwa mteja kuwa MHANGA.Hivi who told you Mpesa Mastercard ni salama? Nyie watu, hivi ukipata tatizo unajua bank ya Mpesa Mastercard iko wapi? Sbb tatizo la fedha ukipata unaenda bank na unapata utatuzi, sasa kuwa na Mastercard wakati hujui bank iko wapi ni kosa sana, au wengi mlijua Mastercard ni kama Mpesa au tigopesa ya kawaida tu? Muwe na Mastercard za bank plz.. Mtalizwa sana msipokuwa makini.