Mpesa MasterCard Tanzania: Kama unapenda uhakika wa malipo yako mtandaoni USIITUMIE

Na wewe nani aliyekwambia mpesa master card si salama??? Siku zote mtu anapokosa maarifa na discipline hufanya makosa na huanza kulalamika kwamba kaonewa, Mtu kaona mtu anatangaza facebook dawa ya utajiri na akalipia ila hajapokea dawa, hapo kweli kuna haja ya kuanza kulalamikia voda???? Wengine hizi mpesa card tunatumia bila matatizo yoyote na hadi sasa nimefanya na kuwafanyia watu miamala isiyopungua mia na yote ilitiki
 
Ishu kwenye makato yao unakuta viwango vya kimataifa $ ipo kwenye 2230 huku unakatwa 2500 yan hapo ndio unajuta.
 
Kinacho leta utata ni kwamba muanzisha post haweki hio softwarw aliyonunua na website yake, Yawezekana kabisa aliaminisbwa na matapeli kuna software ya internet ya bure, kubashiri michezo na kushinda unapobeti au kufukua namba ya firlfriend au mke usome chats 😁😁. matapeli wajanja sana.

Na nimuhakikishie tu hio pesa haigandi hewani kusema ni pending, ishachomolewa na kwa vile hakutumia paypal inakua vigumu kabisa kurudishiwa pesa
 
Ishu kwenye makato yao unakuta viwango vya kimataifa $ ipo kwenye 2230 huku unakatwa 2500 yan hapo ndio unajuta.
Wana mambo mengi hao.

Nenda hata banc abc upewe kadi ndani ya dakika kumi ushamalizana nao unaanza kufanya miamala yako.

Hakikisha unalink kadi yako n amtandao wa paypal na kila muamala fanya kwa paypal kwa usalama zaidi hata ukipigwa unarudishiwa mzigo.

Binafsi nawatumia hawa mpesa kwa muda mrefu bila shida yoyote kwasababu miamala yangu mingi natumia ngao ya paypal, ila nisingetumua paypal huenda yangenikuta haya ya alieanzisha thread, Paypal ni kama condom.
 
Ulishawahi kung'amua hao banc gharama zao zikoje yan kitu che thamani ya 1$ kwenye account wanakata pesa ngapi ya tsh mana hapo ndio tamuchungu ilipo
 
Pesa kukaa hewani huwa maana yake imeshikiliwa na card networks (Visa, MasterCard au American Express).

Hizo situation zinafahamika kama holds/blocks

Hutokea pale kunapokua na tatizo kwenye mihamala.

Kila card network ana policy yake linapokuja suala la 'holds'

Visa kwa mfano, anaweza hold hadi siku 30, American Express yeye hatazidi 15 days.

Hapa ndipo pale pesa inakua imetoka kwa card issuer wako ila haijafika kwa merchant
 
Ulishawahi kung'amua hao banc gharama zao zikoje yan kitu che thamani ya 1$ kwenye account wanakata pesa ngapi ya tsh mana hapo ndio tamuchungu ilipo
Hao wako poa tu mkuu, Sifatiliagi sana maana naonaga rate nayochajiwa na rate iliyopo sokoni hazitofautiani, kiufupi hawajawahi kunichaji kwa rate ambayo ilinifanya nianze kuchunguza rate halisi
 
acha kumtisha mtu na kutetea wezi...ama vodacom wamekutuma....uje uwatetee...yani mtu adai haki yake zaidi ya mwezi tatizo lake lisitatuliwe leo...tena uje umtishe adai haki yake kinyonge...ndio maana tunabaki masiki milele
 
Acha kumtisha mleta mada
Tanzania tuna uhuru wa ku express chochote tunachojiskia na kuweka icing kwa cake JF wanakibia #where we dare talk openly.
So ni haki yake.
 
Acha uwongo natumia mastercard hadi nimewahama ni mwez sasa nafanya mialama na benki
 
Pole mkuu kwa changamoto zilizokupata. Mimi huwa naitumia kwa transactions ndogo ndogo ambapo transaction moja haizidi Tsh 50,000 na so far transaction zote zimeenda vizuri. Na vile vile nimetumia kwa site iliyo trustred (aliexpress.com). Siku nyingine kama unataka kununua kwenye website kwa hela kubwa kama hiyo ni vizuri ukatumia intermediary kama paypal. Kwa maana hiyo kwenye akaunti ya paypal ndo unaweka hiyo virtual card halafu kule ka supplier ndo unaweka account ya paypal. Hii itakulinda sana. Kama kwa paypal transaction ingegoma kukamilika hela isingetoka kwenye akaunti yako ya virtual card. Paypal pia inakulinda dhidi ya kuibiwa na wanaijeria.
 
Pia mtoa mada toa taarifa TCRA pia. Vodacom Wana mauzi Sana na wale customer care staff wao hua wanakera Sana. Ni kweli Kuna tatizo kwenye mpesa na pia kwenye MasterCard yao
 
Huwezi amini kilichomponza ni kuuliza "Ukisema kwenye mitandao swala lako ndiyo litakua limetatuliwa?" Angeweza ongea vizuri mpaka mleta uzi angeridhia
Waafrika hasa wabongo ni jeuri na hawawezi biashara sababu hawajui kujali wateja, poor customer care.
Wanasahau wapo kibiashara na wanapata hicho wanacholipwa sababu ya fedha za wateja walizo zitafuta kwa jasho lao.
 

Nimecheka asee! Pole mkuu.
 
Ushauri mzuri sana hapo kwenye kutumia Paypal. Kuweka details za kadi yako moja kwa moja kwenye site za wauzaji unaweza kuja kusafishiwa account yako siku moja.
Ila wizi wa kuuziwa bidhaa bandia hata ukitumia Paypal unaibiwa tu.
Kuna mzee wangu flani nilimsaidia kununua kitu kwa Card yake kutumia Paypal hakupata mzigo wake huu mwaka wa pili.
Wakati mimi nanunua vitu miaka yote bila shida, yeye aliona tangazo Facebookya offer flani kumbe kule FB wamejaa scammer wa kinaijeria na Ulaya Mashariki.
 

You are too quick to jump into conclusion, issue ya pesa kuwa pending ni jambo la kawaida kila mtu anaelewa, kisichokuwa cha kawaida hapa ni kwanini Vodacom wanachukua muda mrefu kumtatulia shida yake, kumbuka vodacom hawajasema kuwa pesa imeshakafika kwa merchant husika. Sidhani kama humuelewi mtoa mada.

Kama ameibiwa pia vodacom kwa kumuwakilisha mastercard walipaswa wamjibu mlalamikaji kuwa pesa imeshafika ulikokuwa unafanya malipo sisi hatuna chakukusaidia. Suala la yeye alikuwa analipia nini sio la kwetu. Hapa ni kwamba pesa imeshakatwa kwenye account yake lakini haijafika kwa merchant, hivyo majibu ya hili yanatakiwa kutoka kwa Mpesa-mastercard (vodacom)
 
Reactions: Pep
Swala a yeye alikuwa analipia nini ni muhimu kujua wapi tumsaidie, Kuna matapeli wanadanganya wanauza software za kucheki meseji za mpenzi wako, Kutengeneza pesa bia jasho, kutumia internet bure, n.k usipojiongeza ukaamini hivyo vituv vipo ndo ushapigwa
 
mkuu kwanza shida naona iko kwa mtandao ambao umelipa , mimi nimetumia master card yabmpesa mara kadhaa bila shida hata pale malipo yalipofeli nilipata kurudishiea hela huwa nanunua site za kueleweka kama aliexpress alibaba amazon na ebay nahisi hai 2checkout wamekupiga pesa na voda kwao wanaona malipo halali yamefanyika.

Sent from my SM-A507FN using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…