Mpina: 05/2021 Symbion ililipwa bilioni 350 bila kutozwa kodi

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Mbunge Luhaga Mpina amehoji ni kwa nini kampuni ya Symbion ililipwa pesa zaidi ya bilioni Mia tatu bila kutozwa kodi ya Serikali?

Amehoji pia ni kwa nini mkataba wa symbion uliokuwa unakoma 2015 ulihuishwa September 2015 bila kufuatwa taratibu na ajabu Serikali kwa uharaka ilikubali kuilipa Symbion Mei 2021 na bila kutozwa kodi?

Amehoji inakuwaje C.A.G ameshasema mkataba ule uliingiwa kimakosa na kwa nini aliyeuingia kimakosa hawajibishwi na matokeo yake Symbion amelipwa pesa za Watanzania maskini pasipo kufuatwa utaratibu?
 
Bilioni 350 bila kutoza kodi, huku mimi nikituma 30,000/= kijijini kwetu nakatwa tozo.

Haya mambo kama Samia hayajui, au anayajua na kuamua kuyafumbia macho makusudi ndio yanamfanya aonekane alivyo Rais dhaifu.

Kwasababu hata kama kweli hayajui, anapopata taarifa kama hii toka kwa Mpina hakuna anachofanya zaidi ya kukaa kimya na kulea huu wizi, huku wao wakiwaza jinsi ya kumshughulikia mtoa taarifa za wizi.

Mpina kwa sasa ndie mbunge anayejitambua kule bungeni, nampongeza kwa kuamua kwake kujitofautisha na walamba asali wengine bila kuhofia nafasi yake kwenye bunge lijalo, inshort, Mpina ameushinda utumwa wa tumbo unaosababisha kujipendekeza.
 
Mbunge Luhaga Mpina amehoji ni kwa nini kampuni ya Symbion ililipwa pesa zaidi ya bilioni Mia tatu bila kutozwa kodi ya Serikali...
Familia ya Panya hiyo kuanzia babu baba mama watoto mashemeji makaka na madada wote ni imagine unanunua umeme unakatawa makodi yote yale na tozo juu halafu kuna miamba inalipwa bilioni 350 bila tone la makato,,,, na hawaoni aibu wapo tu wanakomaa na skafu zao na wanajiita wazalendo.
 
Nchi ina matatizo hii...! Hapana aisee!

Ni lini viongozi wetu wataumizwa na hali mbaya za watu wanaowaongoza

Wananchi wanakufa kisa wamekosa huduma bora hospitalini, Majii safi, njaa, ajali zinazosababishwa na miundombinu mibovu

Ni lini hawa viongozi wataanza kuthamini maisha ya wengine na kwamba pazia linalotuzinga Ni zile nafasi tu, lakini sote Ni binadamu na tuko sawa!!.

Ni Kwa nini tunapomkumbuka JPM kunakuwepo mashambulizi makali saana???

Ni lipi sasa kwenu mmefanya ili basi tumsahau mnayedhani hakufanya kitu?

Ndo kutuongezea mzigo wa kodi?

Ndo kutunyima maji na umeme?

Ndo kutuongezea malipo ya kuingiza umeme majumbani?

Aaaah! Semeni, ni lipi sasa?

Tulizoea kuona kila aliyehusishwa na wizi, alitumbuliwa na wengine kufikishwa mahakamani, Kwa sasa kinafanyika nini sasa.?
 
Alafu tunamlaumu TANESCO wakati ni kama mwanariadha amefungwa matofari alafu tunategemea ashinde mashindano.....

Tatizo ni kutokuwa na Transparency madudu kama haya watu wangeona aibu kuyafanya...., We need more transparency na Sio sisi tulipe bali waliofanya / ingia kwenye hii mikataba ndio walipe...

By the way makubaliano ya huko China yakija gundulika kwamba hayafai nani atalipa ? Sisi au hao walioingia hayo makubaliano na Wabunge waliokaa kimya bila kuomba kuiangalia...

Ama kweli Tulichezewa, Tukachezewa na Tunaendelea Kuchezewa Sana....
 
Namkumbuka Rais Obama pale ubungo kwenye hiyo mitambo akiuchezea mpira kwa kichwa na Jk akiwa karibu yake akifurahia kweri kweri. !! Halafu hapa hizi juzi nikamuona tena Obama yupo White House alipopewa nafasi ya kuongea akamtaja Biden - vice president Biden - audience waliokuwepo wakacheka sana naye akasema oh huo ni utani tu tulikuwa tumeupanga 😂😂😂 ! Dunia hii ina mambo mengi ya ajabu ajabu ! Mengine huwa yanatokea kama coincidence tu !!
 
CAG kaandika tuu ishu ya Kodi lakini swala ni kwamba je hayo malipo ya deni yalikuwepo kwenye bajeti ya 2020/21?

Na kama yalikuwepo basi ndio swala la Kodi linafuata,kusema nani aliidhinisha kama yalikuwepo hapo Awali sio hoja.
 
Ww mapesa unae anzisha uzi wa Vitenge kila siku. Tuna omba umwambie Mama na Kipara kuwa huu Wizi haukubaliki. Hivi TISS kazi yao ni ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…