Mpina: 05/2021 Symbion ililipwa bilioni 350 bila kutozwa kodi

Mpina: 05/2021 Symbion ililipwa bilioni 350 bila kutozwa kodi

Nchi ina matatizo hii...! Hapana aisee!

Ni lini viongozi wetu wataumizwa na hali mbaya za watu wanaowaongoza

Wananchi wanakufa kisa wamekosa huduma bora hospitalini, Majii safi, njaa, ajali zinazosababishwa na miundombinu mibovu

Ni lini hawa viongozi wataanza kuthamini maisha ya wengine na kwamba pazia linalotuzinga Ni zile nafasi tu, lakini sote Ni binadamu na tuko sawa!!.

Ni Kwa nini tunapomkumbuka JPM kunakuwepo mashambulizi makali saana???

Ni lipi sasa kwenu mmefanya ili basi tumsahau mnayedhani hakufanya kitu?

Ndo kutuongezea mzigo wa kodi?

Ndo kutunyima maji na umeme?

Ndo kutuongezea malipo ya kuingiza umeme majumbani?

Aaaah! Semeni, ni lipi sasa?

Tulizoea kuona kila aliyehusishwa na wizi, alitumbuliwa na wengine kufikishwa mahakamani, Kwa sasa kinafanyika nini sasa.?

Magufuli hakugusa mwizi hata mmoja wa maana, alikua anadeal na vidagaa kwa kelele nyingi, lakini hakuna fisadi hata mmoja alimgusa. Kamkamata Singa na Rugemalira, lakini kawaacha wanasiasa wenzake ambao ndio walikuwa watoa maamuzi. Inshort alikuwa ni mpenda sifa za bei rahisi.
 
Alilipwa lini
Wakt mwingine simuamini mpina Yuko na kasazi fln HV azibitishe hilo
 
Mbunge Luhaga Mpina amehoji ni kwa nini kampuni ya Symbion ililipwa pesa zaidi ya bilioni Mia tatu bila kutozwa kodi ya Serikali?!

Amehoji pia ni kwa nini mkataba wa symbion uliokuwa unakoma 2015 ulihuishwa September 2015 bila kufuatwa taratibu na ajabu Serikali kwa uharaka ilikubali kuilipa Symbion Mei 2021 na bila kutozwa kodi?

Amehoji inakuwaje C.A.G ameshasema mkataba ule uliingiwa kimakosa na kwa nini aliyeuingia kimakosa hawajibishwi na matokeo yake Symbion amelipwa pesa za Watanzania maskini pasipo kufuatwa utaratibu?
Tanzania ina watu wanyama sana....
 
Jana namuona Hamphrey Polepole akiangalia golf huko Malawi, kalambishwa asali katulia.
Saa nyingine sisi wananchi inatubidi tuwaunge mkono hawa watu vinginevyo watapewa asali kama Mbowe, nk watusaliti.

Kwanini tusiingie barabarani kuwaunga mkono watu wanjitoa kwa ajili ya nchi yetu?
 
Bilioni 350 bila kutoza kodi, huku mimi nikituma 30,000/= kijijini kwetu nakatwa tozo.

Haya mambo kama Samia hayajui, au anayajua na kuamua kuyafumbia macho makusudi ndio yanamfanya aonekane alivyo Rais dhaifu.

Kwasababu hata kama kweli hayajui, anapopata taarifa kama hii toka kwa Mpina hakuna anachofanya zaidi ya kukaa kimya na kulea huu wizi, huku wao wakiwaza jinsi ya kumshughulikia mtoa taarifa za wizi.

Mpina kwa sasa ndie mbunge anayejitambua kule bungeni, nampongeza kwa kuamua kwake kujitofautisha na walamba asali wengine bila kuhofia nafasi yake kwenye bunge lijalo, inshort, Mpina ameushinda utumwa wa tumbo unaosababisha kujipendeza.
Kuna chawa wanamsifu huyu mama kila siku sisi kila siku tunakatwa kodi kwa miamala mbali mbali , 300b without consideration of tax
 
Mbunge Luhaga Mpina amehoji ni kwa nini kampuni ya Symbion ililipwa pesa zaidi ya bilioni Mia tatu bila kutozwa kodi ya Serikali?!

Amehoji pia ni kwa nini mkataba wa symbion uliokuwa unakoma 2015 ulihuishwa September 2015 bila kufuatwa taratibu na ajabu Serikali kwa uharaka ilikubali kuilipa Symbion Mei 2021 na bila kutozwa kodi?

Amehoji inakuwaje C.A.G ameshasema mkataba ule uliingiwa kimakosa na kwa nini aliyeuingia kimakosa hawajibishwi na matokeo yake Symbion amelipwa pesa za Watanzania maskini pasipo kufuatwa utaratibu?
Kumbe ndio maana vituo vya mafuta vya lake oil vimeota kama uyoga
 
Back
Top Bottom