Bilioni 350 bila kutoza kodi, huku mimi nikituma 30,000/= kijijini kwetu nakatwa tozo.
Haya mambo kama Samia hayajui, au anayajua na kuamua kuyafumbia macho makusudi ndio yanamfanya aonekane alivyo Rais dhaifu.
Kwasababu hata kama kweli hayajui, anapopata taarifa kama hii toka kwa Mpina hakuna anachofanya zaidi ya kukaa kimya na kulea huu wizi, huku wao wakiwaza jinsi ya kumshughulikia mtoa taarifa za wizi.
Mpina kwa sasa ndie mbunge anayejitambua kule bungeni, nampongeza kwa kuamua kwake kujitofautisha na walamba asali wengine bila kuhofia nafasi yake kwenye bunge lijalo, inshort, Mpina ameushinda utumwa wa tumbo unaosababisha kujipendekeza.