Mpina ataka kumuumbua Waziri Mwigulu bungeni, apatwa na kigugumizi, Spika ambana "mi sielewi"

Mpina ataka kumuumbua Waziri Mwigulu bungeni, apatwa na kigugumizi, Spika ambana "mi sielewi"

Hawaruhusiwi, wao ni watoa majibu, na kwa sababu watamuulizaje jambo waziri mwenzao Bungeni? Ndio maana watu wanapendekeza mawaziri wasitokane na wabunge. Ukiwa na mbunge akawa waziri basi hawezi tena kuwasemea Bungeni. Kama kuna swali atauliza kwenye vikao vya baraza la mawaziri
Umejibu vizuri, Kuna shida ya uelewa watu wengi humu jf na mtaani. Waziri hawezi kuiwajibisha serikali kwa kuwa yeye ndio serikali.

Waziri ndio anajibu yote yanayoulizwa kuhusu serikali.
 
Waziri anauliza kwa nan? Baraza la mawaziri majibu yote yapo, ndio maana unaona bungeni mbunge yoyote anapouliza swali kuhusu serikali waziri ndio anapaswa kujibu.
Kwa hiyo kwa mfano waziri wa afya akitaka ufafanuzi kutoka wizara nyingine inabidi afuate waziri husika ofisini kwake na sio kuuliza bungeni?
 
Mpina amerusha kombora au ameuliza swali?????

Maana Si Kwa mtetemo na kigugumizi kile...

Apumzishwe mwigu, ana mambo mengi kichwani.
 
Kwa hiyo kwa mfano waziri wa afya akitaka ufafanuzi kutoka wizara nyingine inabidi afuate waziri husika ofisini kwake na sio kuuliza bungeni?
Kuna baraza la mawaziri, hapo ndio majibu yote yapo ndio maana wenyewe wanaita collective responsibility.

Hata waziri fulani akienda sehemu akaulizwa swali na wananchi ambalo halipo kwenye wizara yake Kama hafahamu atawasiliana na waziri husika
 
Back
Top Bottom