Mpina ataka kumuumbua Waziri Mwigulu bungeni, apatwa na kigugumizi, Spika ambana "mi sielewi"

Mpina ataka kumuumbua Waziri Mwigulu bungeni, apatwa na kigugumizi, Spika ambana "mi sielewi"

Lakini ni kawaida Duniani hapa, watu aina ya LUHAGA MPINA kudidimizwa sana !.

Watanzania na Binadam waliowengi Wana kasumba ya kuwadown watu wanaonekana Bora.

Ndio sababu Heshima akupayo Mtanzania haitokani na Kile kilichobora ulichonacho, Bali wewe ni nani!!.


MUNGU WA ISRAEL AENDELEE KUMLINDA MH.LUAGA MPINA, AMPE AFYA NJEMA, ILI AENDELEE KUSOMA ,KUDADAVUA NA KUJA NA MAMBO YALIYO CHANYA.

Viva Magufuli Kwa Huyu Mbunge !!

CCM wanacheza sarakasi tu. Hoja hii iliibuliwa kwa kirefu bungeni mwezi Juni 2022

Mbunge Nusrat : Azungumzia shilingi Trilioni 300 tarehe 22 June 2022



Source : Uhondo TV
 
Rais angekuwa anajua watanzania wanataka nini, hivi leo mwigulu asingeendelea kukalia kiti cha waziri wa fedha. Na rais kuendelea kushupaza shingo kwa ajili ya mwigulu anajipunguzia ushawishi kwa watanzania, sema hili la kupungua ushawishi chawa hawata mwambia, maana kazi yao kubwa ni mapambio. Maana hata malkia akiwa utupu wao haiwahusu. Ila kwa nia njema tu, na kwa maslahi mapana ya nchi yetu, haijarishi una chama au hauna chama. Ila mwingilu angemtafutia kazi nyingine ya kufanya. Ili kurudisha imani kwa watanzania, inayozidi kuporomoka siku hadi siku.
Mbona mnakuwa wapumbavu kiasi hiki? Kuondolewa kwa waziri wa Fedha ndo hitaji muhimu la watanzania kwa sasa?
 
Mwigulu kila sehemu ukipita anaongelewa yeye aisee na bado anaenda ofisini kaharibu uchumi Mama anaendelea kumkumbatia tuu..
 
Acha roho mbaya.
Utasema ni roho mbaya napokea, ila ukweli lazima kusemwa, kwenye hicho kiti Hana mvuto , pamoja na Zungu kuingiza watanzania kwenye matatizo ya tozo( Mungu anamuona) ila kwenye hicho kiti kidogo anamvuto, ila uyu hamna ,
Sema ndo hivyo nafasi za kuokota ila hapamtoshi pale, bora Dr Msukuma mzee wa kutema yai
 
Mataga ni mataga tu.
Huyo Mpina anaongea kwa kuwa sio waziri kwa sasa angekuwa waziri asinyanyua mdomo katu angebaki kugonga meza kwa kila neno analosikia.
Watu wake walishaenda na ruler kupima samaki mgahawa wa bunge na alishawahi kutajwa kama waziri kichaa huko Ulyankende Republic!
 
Utasema ni roho mbaya napokea, ila ukweli lazima kusemwa, kwenye hicho kiti Hana mvuto , pamoja na Zungu kuingiza watanzania kwenye matatizo ya tozo( Mungu anamuona) ila kwenye hicho kiti kidogo anamvuto, ila uyu hamna ,
Sema ndo hivyo nafasi za kuokota ila hapamtoshi pale, bora Dr Msukuma mzee wa kutema yai
Nibora Dr Msukuma?🎓 umezidisha utani🤠
 
ile - ya ya ya ya ya ya ya ya ya ya ya ya ya ya ya........

wazee waliminya kitufe kumuumbua maneno yakagoma kutoka mdomoni dadadeq- bado kijana mdogo apunguze majivuno / majigambo... hiyo ni salam tosha ya tozo kwake. 😀😀😀
 
Kwa hiyo kwa mfano waziri wa afya akitaka ufafanuzi kutoka wizara nyingine inabidi afuate waziri husika ofisini kwake na sio kuuliza bungeni?
Elewa ndugu unaelimishwa, Waziri hawezi kuihoji Serikali wakati wa Kikao bungeni. Wana vikao vyao vya Baraza la mawaziri. Wawapo bungeni wao ni wajibu hoja zinazoulizwa/hoji wabunge. Huelewi?
 
jibu pekee nililoskia ni Yaaa yaaa yaaa yaaa yaaa yaaa yaaa yaaa yaaa
 
Back
Top Bottom