Wahenga Siasani wanasema kwa Kawaida Bunge la Chama kimoja ni Bunge la Serikali
Hivyo Mpina Kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge ni Sawa Kabisa na Kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM tofauti yake ni Wajumbe tu
Wahenga wanasema kuna uwezekano Mpina akapewa adhabu kali ikizingatiwa Bunge hili limebakiza mwaka mmoja tu
Ngoja tuone
Mlale Unono 😃🐼
Kwenye hili, Luhaga Mpina amewabananisha wenzake kwenye Kona mbaya na ya hatari sana.
Na huyu bwana Luhaga Mpina ile kupeleka ushahidi wake kwa Spika na hapohapo kufanya Press Conference kuelezea hatua kwa hatua kila alichokiwasilisha kwa Spika na kuumwaga ushahidi huo hadharani, si kwamba alikuwa hajui kinachokuja. Na sio kwamba alikuwa hajui consequences zake. Si kwamba alikuwa hajui kanuni za Bunge zinasemaje.
Generally speaking, ni kuwa huyu bwana si mjinga. He knows exactly what he's doing. Hopefully kuwa amejiandaa kwa lolote.
Kikubwa ni kuwa ameiweka CCM na serikali ya CCM kwa ujumla ktk njiapanda. Wamakonde husema, UKIKIMBIA NCHALE, UKISIMAMA NCHALE na UKIKAA NCHALE. Kwa maana kwamba uamuzi wowote watakaochukua dhidi yake kwenye hili, hautawapa nafuu yoyote. Kilichopo mbele yao ni kupima tu uamuzi gani una madhara nafuu kuliko mwingine.
Wakumbuke tu kuwa hizo nyaraka za ufisadi huo wa CCM (Rais Samia kupitia kwa waziri wake Bashe na Mwigulu), tayari ziko mikononi mwa wapinzani wao wa jadi Tundu Lissu na CHADEMA kwa ujumla. Wakijichanganya tu watapigwa spana mpaka wataanza kutafuta SMG zilipo!!
Mimi naona hili, kuwa, Kuna baadhi ya vigogo wa serikali wakitolewa sadaka. Bashe atapona. Mtandao wa mafisadi utamlinda maana Rais Samia Suluhu Hassan mwenyewe kupitia kwa mwanae ndiye mhandisi wa ufisadi huu.
Huu ni ushahidi wa waziwazi kuwa ndani ya serikali na CCM Kuna mgawanyiko mkubwa kuhusu u - Rais wa huyu mama.
Nimejaribu kufikiria hata namna Luhaga Mpina alovyopata nyaraka za kuthibitisha tuhuma zake.
Ni kwamba amezipata kwa haraka sana, kwa urahisi sana tena zingine zikiwa nyeti sana toka ktk taasisi nyeti za serikali ili kuishikisha adabu serikali hiyohiyo. Hii ni kuonesha kuwa Kuna watu ndani ya serikali na taasisi zake hawaridhishwi na namna huyu mama anavyoenda pamoja na baadhi ya wateule wake maalumu.
Hili kundi jingine ndani ya serikali hiyo hiyo lililoachwa solemba, lisiliopata mgawo wa rushwa za uuzaji rasrimali za Tanganyika kwa waarabu wa mashariki lenyewe liko tayari kumwaga mboga. Kina Luhaga Mpina ni wapambe tu!!