Mpina: Kifungu kilichotumiwa na Spika Tulia kunituhumu na kunihukumu hakipo!

Technically ilipaswa Spika amuachie naibu wake alisimamie lile swala, maana yeye tayari alikuwa ni mlalamikaji. Sasa mlalamikaji kapeleka malalamiko yake kwenye kamati na akaielekeza kamati cha kufanya, akapokea taarifa ya kamati na kuendesha kikao cha kutoa hukumu ya dhidi ya mtuhumiwa huku yeye akiwa ni mlalamikaji.
 
Sikiliza dakika 59 na sekunde 39 utaelewa nani anahitaji kupgwa spana.
usijaribu kuleta uongo, Bashe kashindwa hata kujitetea kwa zile hoja zilizotolewa, na hapa tena anaenda kuwavua nguo. Bunge zima Hakuna mtu aliyesimama kujibu zile hoja zaidi ya kuongea upumbavu, spika Tulia ndio kabisa ni kama Likwidi tu wa pale kurasini.
Wewe unaweza kujibu hoja za mpina?
 
Mheshimiwaspika waBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Tulia Amemuonea Msheshimiwa mpina kwa maelezo aliyoyatowa Mpina ana ahaki ya kusema ukweli ingawa ukisema ukweli ndio unapigwa vita Mheshimiwa Bache amefanya makosa kama anavyosema Mheshimiwa mpina na kusababisha bei ya sukari kuwa juu. Hakutendewa Haki Mheshimiwa mpina Ameonewa na Spika pamoja na kamati ya maadili ya bunge na wabunge wote waliounga mkono. Mheshimiwa Mpina ni mtetezi wa Wanyonge wananchi walala hoi hongera zake tuko pamoja nae siku zote asivunjike moyo awe mstari wa mbele kutetea maslahi ya Wananchi.
 
Umeangalia Kikao Kizima???
Uliona alipotoa Taarifa akasema kama kazuiwa Kwnda bungeni wala kusogea Karibu na Bunge "aliuliza atawezaje kupeleka Ushahidi wake na utetezi wake?"
 
Umeangalia Kikao Kizima???
Uliona alipotoa Taarifa akasema kama kazuiwa Kwnda bungeni wala kusogea Karibu na Bunge "aliuliza atawezaje kupeleka Ushahidi wake na utetezi wake?"
kazuiliwa baadaya kupeleka kitu chake cha ushahidi na baada ya kusikilizwa kwa siku kadhaa na kamati.

Hukumu ya kuondoilewa bungeni imetolewa na bunge lote. Kila mtu kashuhudia.

zingine zote ni porojo zake tu.
 
Viva Luhaga Mpina ; uishi maisha marefu .
 
Huyo mpina anafikiri kamati iliwekwa ya nini? Kuchunguza na kupitia yasiyokuwepo?

Anacheza na akili za wajinga tu.
 
Katika maisha kila mwanadamu ni chawa kwa yule anaye mshabikia. Nawe ERoni ni chawa wa Luhaga Mpina


Wewe kwa akili yako tu hata kama ni cha wa mama na mama yake na mama yake mzaa mama yake unaona kuwa ni kweli sukari iliingizwa tani Elfu 60 isiyo na kodi tena imeagizwa kwa dharura halafu imeingia mtaani iuzwe zaidi ya sh. 2000/- Sukari kutoka Brazil haiwezi kuuzwa zaidi ya sh. 1800 iliwa na kodi . Sasa iweje sukari iliyofutiwa kodi iendelee kuuzwa sh . 3500/ - mpaka 5000/ - Ni wazi kuwa sukari haikuingizwa nchini bali walidanganya kama kawaida . Na mchezo huo unafanywa sana na hizo bodi zikishirikiana na Mawaziri na watendaji wengine kwenye wizara . Meli ilifika bandarini na kuegesha pale documents zikatolewa meli aikasepa na sukari yake . Ni meli tu iliokotezwa njiani na kuambiwa hebu njoo simama hapa kidogo halafu chukua mpunga wako kidogo sepa .

Kama kweli walikua wana nia ya kuondoa adha ya sukari nchini hawa wageni na sukari yao ya kigeni kwa Watangayika basi wangeruhusu Sukari toka Zanzibar ambayo ni washirika wa Muungano iingie kwa dharura.
Zanzibar ambayo mpaka mwaka jana sukari ilikua haijawahi kuvuka sh. 2000/- Kwanza wangeinua sasa Soko la Sukari Zanzibar na kuongeza kipato cha wananchi wa Zanzibar na kiwanda chao na wakulima wao.
Hili ina maana hawakuliona hao wazamagendo na sio Wazalendo wenu ?

Kenya kwa miaka yote wananunua mahindi Tanganyika kama ujirani mwema ! Lakini kama kweli palikua na nia ya dhati ya kuingiza sukari kwa nini tusiingize sukari toka Malawi?
Kama ni dharura kwa nini wasiruhusu wafanyabiashara wa Mbeya na Tunduma kuvuka Boda na kununua sukari ya Malawi kwa dha9iii0rura na kuwanufaisha watanzania wenye mitaji ya kawaida kama yule mfanyabishara wa makava ya Simu?

Kwa nini iwe ni dharura halafu iletwa na muuza Makava ya Simu asiyejua hara ubora wa sukari na hana hata Magodown ya kuhifadhi ani Elf 30 za Sukari?
Je , anaweza kutuonyesha walipohifadhi hiyo Sukari na aliisafirisha kwa fuso au IST au Boda boda au Kirikuu kwenda kwenye magodaoni ya mengine?

Ni wazi mchezo huu ndio uliomwondoa Kangi Lugola enzi za JPM japo Kangi hakuhusika na hakujua kua kuna mchezo kama huo wa kuagiza vitu hewa na pesa inapigwa na wajanja.

Serikali imeshajitoa kwenye uzalishaji wa sukari na haina kiwanda sasa haya mabodi bodi ya nini kama sio kufuja fedha za umma na kufanya michongo ya kishetani kwenye fedha za umma!!

Eti bodi ya Korosho inaundwa na Rais wakati serikali haina hata eka moja ya Shamba la korosho .
Bodi ya Kahawa wakati hakuna mashamba ya Umma. Ni wizi mtupu .

Basi wateue vijana wasio na ajira kwenye hizo bodi la hasha wanateua watu walioshindwa na kufilisi makampuni mengine.

Enyi CCM na watawala wake Msipotubu na kubadilika yanayotokea Huko kwingine huko yatawafikia na mali mnazizozivuna bila jasho zitachukuliwa bila jasho.

Mungu amechoka kusikia vilio vya watu wa nyonge kwenye nchi aliyoiumba na kuipa utajiri mkubwa ambao sio mali yenu wenyewe na familia zenu bali ni mali ya Watanzania mil. 65 pasiwe na anayekosa chakula wala dawa wala maji wala choo shuleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…