Mpina: Nchi yetu imefilisika hadi inapangisha Bandari? Tusikubali hili

Mpina: Nchi yetu imefilisika hadi inapangisha Bandari? Tusikubali hili

Je terms and condition alizoingia DP world na inchi zingine ni zile zile tulizopewa cc hapa ?

Nyie mnajivunia Huyu bwana kufanya kazi na Inchi zingine kama USA ndio maana mnamkingia kifua , mngeleta mikataba ya huko tuka compare clauses za artcles kwenye mkataba pengine tungeongea lugha sawa.

Kubinafsisha hiyo Bandari sio tatizo , tatizo ni hizo clauses , zinatubinya Mbupu hujapata kuona.

Muda utatukosoa ngoja tuone.
Haziwezi kufanana .kwa kuwa saa100 ndo alyeenda dubai kuomba omba kwa hiyo mshart laizma tukubaliane yae
 
Zipo bandari Marekani zinaendeshwa na Dubai ports...je wamarekani wamefilisika?

Kwa nini huu uongo umekazana nao? Marekani ipi unaongelea hapa. Utetezi wako kwa huu ujinga unanishangaza sana halafu wajinga wenzio wanakupa like.

The Boss, kumbe wewe ni mpuuzi kiasi hiki. Kamati ya bunge ya Marekani iliikataa DP World kwa kura 62-2 walipoomba kuendesha Bandari kadhaa nchini humo.

Lazima utakuwa na ubia na Waarabu hao au ni wajomba zako na wewe pia.
 
Zipo bandari Marekani zinaendeshwa na Dubai ports...je wamarekani wamefilisika?
Terms na conditions za mikataba ya Marekani na hii wanayotaka kuingia na Tanzania zinafanana? Kama umeiona mikataba ya Marekani tuwekee hapa ili tuwe na uelewa mpana wa namna wanawekeza, lakini ukikomaa tu kwamba wamewekeza huku na kule bila kujua conditions za mikataba yao, unakuwa ni uvivu wa kufikiri!
 
Mpina kalipwa na Karamagi...
Ilikuja taarifa hapa Karamagi kawapanga wabunge machachari.
M
Karamagi alikuwa mwana hisa Ticts ambao wameondolewa..dili wamepewa Wengine
Si bora wanahisa wawe hao kina karamagi pesa zao zitazurura humu humu nchini, kuliko kuwapa waarabu ambao watapelwka pesa kwao na kutuachia ukata tu
 
Terms na conditions za mikataba ya Marekani na hii wanayotaka kuingia na Tanzania zinafanana? Kama umeiona mikataba ya Marekani tuwekee hapa ili tuwe na uelewa mpana wa namna wanawekeza, lakini ukikomaa tu kwamba wamewekeza huku na kule bila kujua conditions za mikataba yao, unakuwa ni uvivu wa kufikiri!

Achana na huyo mpuuzi, hakuna bandari hata moja nchini Marekani inaendeshwa na hao Waarabu. Walijaribu kujipenyeza huko wakatupwa mbali. Mikataba ya kipuuzi kama huu mwisho wake Chalinze.
 
Nyie wafanyakazi wa bandari mtamtimia kila mtu lakini hamtafanikiwa. Mmemtumi slaa imeshindikana. Naskia amegawa pesa kwa kila mwandishi wa habari ila wapi swala liko pale. Mnamtumia mpina lakini wapi. Kubalini ulaji wenu umefika mwisho tunataka uwazi sana katika uendeshwaji wa bandari. Zile rushwa zenu nzito nzito zimefika tamati. Tafuteni kazi nyingine. Mbona sisi walimu tunaishi? Hatuna rushwa lakiniaisha yanaendelea tu. Njooni tuungane

MPINA AILIPUA VIKALI SERIKALI, "NI HATARI SANA KWA TAIFA, NAWASHINIKIZA TUSIKUBALI HII"​



Nchi yetu imefilisika kipesa inapangisha aka kuwekeza mpaka Bandari?

Ninamuunga Mkono Mpina maneno yake anayo zungumza yana point kubwa.

Uwekezaji wa bandari ni mbovu sana Serikali iangalie sana kukodisha bandari za nchi yetu miaka 10 ijayo Serikali yetu tutakuwa kama Zimbambwe tutafilisika kwa kila kitu na umasikini utazidi kiasi ambacho. Tutakuwa tunaomba omba misaada kwa wafidhili wetu kila siku Mungu asijaalie tusifike huko amin.
 
Nchi ina majanga hii.
Wanasiasa kuweni na huruma basi.
Mkielewa pia kufa kupo, na kila mtu atatoa hesabu yake namna alivyowatendea wenzake mbele za Mungu. Hakuna kitu kinauma jamani kama urithi wetu kutolewa kwa wageni.
 
Nchi ina majanga hii.
Wanasiasa kuweni na huruma basi.
Mkielewa pia kufa kupo, na kila mtu atatoa hesabu yake namna alivyowatendea wenzake mbele za Mungu. Hakuna kitu kinauma jamani kama urithi wetu kutolewa kwa wageni.
Wanaweza kuwadhibiti wapinzani lakini siyo wezi wa bandarini, wala hawezi kuboresha huduma bandarini zikawa shindani kimataifa
 
Wabinafsishe na tanesco, Kama watampata mwekezaji ambaye atatuhakikishia umeme hautakatika milele, atauza unit moja kwa 150 tu, ataunganisha umeme nyumba zote za nchi hii, ataanzisha vyanzo vingi vya umeme na ataripa Kodi yakutosha kwa serikali. Wakimpata wampe tu maana sisi hatuna akili za kuendesha vitu hivyo
 
Back
Top Bottom