Kumshindanisha Diamond na mwanamziki yoyote Tanzania ni ujinga, si kwa waliopo au waliokuwepo. Bahati nzuri mi ni mtu wa zamani, najua wale wa zamani na wa sasa.
Ukiweka ushabiki pembeni, kuna wale wasiojua biashara ya muziki(showbiz) wanabaki kusema Diamond alikuwa zamani enzi za "nenda kamwambie" and the likes lakini hawajui dogo amebadilika kulingana na soko, internationally na local(kwa wale wa amsha amsha), muziki wa kuchezeka na ambao unaweza kumfurahisha hata asuyejua Kiswahili.
Kwa sisi tunaoishi na watu wasiojua Kiswahili hauwezi kumshawishi mtu asikilize nyimbo za kina Kiba/Marlaw ambazo wanaimba visauti kama wanaimba taarabu, hakuna mwenye uelewa wa kinachoimbwa na haiwezekani ukamshawishi apende nyimbo za aina hiyo.
Kuwashindasha Kiba na Marlaw inaweza kuwa sawa lakini kumtaja, I mean hata kumtaja tu Diamond katika wanamuziki wa level hizo ni makosa na ni kama kunakuwa na makusudi flani kwani ndiye mtu anayepaisha jina la Tz internationally katika sekta ya burudani.
Angalia fans hata maoni tu popote kwenye social media, angalia impact ya shows zake, angalia endorsements na matangazo na vyote hivi havikuja kwenye silver plate bali ni matunda ya mafanikio katika biashara ya burudani(kuimba vizuri, kujibranda vizuri, kumantain kwenye level ya juu kwa muda mrefu, kufanya kazi kwa bidii, kushikamana na timu yake bila ya majivuno kujiona yeye ndiyo kila kitu).
Hawa nyota wengine wa muziki(Bongo flavour) wangekuwa kiwango cha Diamond hata kufanya nao interview ingekuwa ni shida, kuwa humble pia kunambeba sana, kuushikilia ule Utandale kunamsaidia pia ndiyo diehard fans wake asilimia kubwa ni wale wa uswazi.
Wa kushindanishwa locally waendelee, nyota wanaopaisha jina la nchi kimataifa washindanishwe/walinganishwe na international artists.