Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimejaa Afrika na hatufanyi maajabu?

Kwa hiyo hao wachache wa huko ESPN ndio unachukulia kuwa wamarekani wote hawapendi soccer?
Fatilia page yoyote ya michezo ya Marekani utakuja kuungana na mimi, mimi huwa nafatilia zaidi page mbili, espn na Bleacher Report
 
Kumbe wewe ni mzaliwa wa Marekani? Hongera kwa kujua kiswahili!
 
Ni kweli wako katika dunia yao, yasiyoihusu dunia yao hawayajui.
 
Mpira ni kuupa kipaumbele....halafu pesa inafuatia...baada ya kuupenda lazima uwekezaji ufanyike...kuhusu vipaji siamini sana kwenye hilo...Timu yenye msingi mzuri ni rahisi kufanya vizuri kuliko timu yenye vipaji vikubwa ikiwa na msingi mbovu.

Marekani wana pesa lakini Football si kipaumbele chao ila Basketball na American football.

Tanzania mpira ni kipaumbele chetu...tatizo pesa..maana tunahitaji academies kwa ajili ya kuwaandaa vijana wadogo ili wapate misingi ya football waweze ku compete dunia nzima...siyo kama ilivyo sasa tukicheza na timu nyingine wachezaji wetu wanaonekana kabisa ni wazito wa miili na maamuzi.
Tunahitaji viwanja vizuri nk. hivyo vyote vinahitaji dough ambayo hatuna.
 
Mpira ni kuupa kipaumbele....halafu pesa inafuatia...baada ya kuupenda lazima uwekezaji ufanyike...kuhusu vipaji siamini sana kwenye hilo...Timu yenye msingi mzuri ni rahisi kufanya vizuri kuliko timu yenye vipaji vikubwa ikiwa na msingi mbovu.
Sawa boss...
 
Mpira ni kitu Fulani chenye umbo la duara hutumika Katika mchezo ambao hufanyika kwnye uwanja mkubwa na kuwa na watu 11 kwa kila pande mbili ambapo lengo ni kuukokota huo mpira uingie kwnye nyavu iliofungwa katika nguzo nne kwa kuzunguza hizo nguzo.

....atakae ingiza mpira humo kwnye nyavu Basi timu take inakua imeshinda..
 
Mkuu, nimehoji kuhusiana na soka kwa sababu ndio mchezo number moja duniani. Kwa hiyo hata kama Marekani hawaupendi hiyo haiondoi ukweli kwa kandanda ndio mchezo wenye mashabiki wote kuzidi hizo baseball na american football...
Ni mchezo namba Moja duniani na hata Tanzania na Uingereza, lakini sio mchezo namba Moja US. Yaani hata namba mbili na tatu huo mchezo haupo sasa watashindanaje na nchi ambazo huo mchezo kwa ni kipaumbele namba 1.
 
Ni mchezo namba Moja duniani na hata Tanzania na Uingereza, lakini sio mchezo namba Moja US.
Mkuu, soccer liliwashindwa wanaume wa Marekani ndio maana wakaamua kuanzisha michezo yao wenyewe?...
 
Mleta mada analazimisha Mambo ukichagiza na mahaba yake kwenye soccer .

Kila watu Wana utamaduni huwezi lazima hio kitu

Na pia sijui Kama unaelewa Mambo ya TASTE & PREFERENCE
 
Mleta mada analazimisha Mambo ukichagiza na mahaba yake kwenye soccer .
Kama unaniona ninalazimisha mambo, it's okay wewe na mawazo yako.

Siwezi kuhoji American Football kwa maana sio mchezo wa dunia. Hao wamarekani waliamua kuunda michezo yao kwa maana mchezo wa dunia uliwashinda licha ya kuwa na pesa nyingi...
 
USA mpira ni mchezo wa wanawake ndo maana USWNT inashinda kombe la dunia la wanawake kila michuano.

Michezo mingine ambayo USA wanaipenda basi wanashinda.

Afrika kuna vipaji ila haviwi groomed kumbuka hard work beats talent.
 
Mkuu, soccer liliwashindwa wanaume wa Marekani ndio maana wakaamua kuanzisha michezo yao wenyewe?...
Sio liliwashinda bali hawalipendi, Ni kama vile watu wa Mwanza na Arusha tusivyopenda taarab lakini tunapenda hip hop, kwa hiyo ni vigumu kupata wasanii wazuri wa taarab na singeli kutoka Mwanza sababu Wana Mwanza hatupendi mziki huo, lakini kwa dar ni rahisi.
 
USA mpira ni mchezo wa wanawake ndo maana USWNT inashinda kombe la dunia la wanawake kila michuano.

Michezo mingine ambayo USA wanaipenda basi wanashinda.
Kama hawapendi soccer mbona bado wanachama wa FIFA mkuu? Burundi hawakuipenda ICC wakajitoa. Wao USA bado wanafanya nini FIFA?...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…