Mpoki ni balaa

Mpoki ni balaa

Ukweli unauma eeeeh........
Go on Mpoki......
Though I didnt watch.....but from comments I realize that you "CALLED A SPADE A SPADE"
 
ni kweli nakubali watanzania wengi tuna iq ndogo....tena sana no wonder wanasiasa uchwara wanawatumia wanavyotaka......
 
Kiukweli jokes hizi zinategemea na mazingira uliyopo. Hata maraisi hutaniana wanapokutana wakiongea. Lakini jokes watakazofanya wakia on-air ni tofauti kabisa na zile watakazofanya off-air. Mfano, kitendo cha Mpoki leo kusema familia ya kina Bonny kuwa ni ya wabahili kuliko watu wote sijakifurahia kabisa. Tena bila kutaja ubahili wao ni upi!! Hata Bonny mwenyewe amekwazika sana. Si yeye tu na wengine pia. Ni bora angemtania Bonny pekee yake kuliko kuweka na wadogo zake wote.
Bonny ni miongoni wa ma dj wachache sana hapa Bongo wenye heshima kubwa kutokana na sanaa yake. Hivyo kusema tu ni bahiri mkubwa bila kuelezea walau kidogo ni kwa vipi ni bahiri. Kwa kweli unakuwa hujamtendea haki. Kwa hili la Bonny limenikwaza hata mimi, kwa sababu namjua Bonny in personal.

Hivi 'bahili' ni tusi?mi mwenyewe mbahili
 
Hakika kuwasema watu ktk public kama ile sio kuchekesha bali ni kukosea heshima na usiri wao wa kibinadamu. Halafu sidhani kama wale watu watakua happy tena kwenda kwenye show zijazo za K.T.M.A.
 
Aliboa sana. Niliangalia ili tu nijue yupi ni next kuumbuliwa! Kupanda pale jukwaani hakikuwa kitendo cha kufurahisha tena kama ilivyozoeleka. kila anayepanda alikuwa anafikiria ni negative comment gani itatolewa dhidi yake
 
Ukweli unauma eeeeh........
Go on Mpoki......
Though I didnt watch.....but from comments I realize that you "CALLED A SPADE A SPADE"

Mkuu watu wamevunjiwa heshima hadharani we unashabikia?
 
Mkuu watu wamevunjiwa heshima hadharani we unashabikia?

Ndo hapo sasa. Eti anasema,'Fina Mango ni mwanamke mjanja kuliko wote kwa kuwa ndo mngoni wa kwanza kuzaa na Mzungu.'
Hivi ukizaa na Mzungu ni ujanja?! Mpoki anahitaji mapinduzi ya ki fikra. Kwa sababu kwa maneno mengine anamaanish hata Mama yake alikosea kuzaa na Baba yake ambaye ni Mhaya!
Kwa dunia ya leo unawaambia nini wasichana wa Tanzania ambao wanatafuta wenza kuwa wasikubali kuzaa na wabongo eti kisa ni rangi yao.
Wakati America na Ulaya iko inapinga rascism kwa nguvu zote huku sie tunachekelea!!!
 
Hakika kuwasema watu ktk public kama ile sio kuchekesha bali ni kukosea heshima na usiri wao wa kibinadamu. Halafu sidhani kama wale watu watakua happy tena kwenda kwenye show zijazo za K.T.M.A.

Hata ukiangalia audience ya jana,unaweza kuona ni watu wa aina gani wanaenda huko kwenye tuzo. Kiukweli kila mwaka inazidi kukosa mvuto. TBL nna BASATA wanahitaji kuangalia hilo otherwise tuzo hii haitakuwa na lengo lililokusudiwa.

Ushahidi wa hili wasanii wote wakongwe hawakutokea mfano Hassan Rehani Bitchuka,Lady Jay D, Mtangazaji mahiri Massoud Massoud. Lazima walipewa taarifa kuhusu lakini hawakutokea na wala hawakutuma wawakilishi.

Mimi ningependa Mpoki ajifnze kwa watu kama kina Evans Bukuku ktk hili. Kingine huwezi kutoa jokes ktk lugha ambayo huifahamu eg. Kiingereza. Ni kitu kibaya kwa anayesikiliza unavyo haribu lugha yao.

Theme ya KTM inasema 'KI KWETU KWETU' sasa kung'ang'ania kingereza usichokijua ni nini?
 
Kwa upande wa wachekeshaji wa maneno mpoki hakuna wa shindana nae hapa Bongo ila kwa watu wanavyomponda si shangai mana hata wahenga walishasema nabii hakubaliki nyumbani kwake!!
 
Back
Top Bottom