Mpunga chotara wa China wasaidia nchi za Afrika kuhakikisha usalama wa chakula

Mpunga chotara wa China wasaidia nchi za Afrika kuhakikisha usalama wa chakula

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
mmexport1750299552006.jpg


Bw. Moussa Dabo kutoka Gambia alikuwa mwanafunzi wa Yuan Longping ambaye ni Mwanasayansi maarufu wa mpunga chotara nchini China, hivi karibuni alifika kwenye kaburi la Yuan kutoa heshima zake. Alipiga magoti na kuweka mfuko wa mpunga chotara kutoka nyumbani kwake mbele ya kaburi na kusema, Mwalimu, mbegu zako za mpunga chotara zimeota nchini Gambia.

Mwezi Desemba mwaka 2019, katika Mkutano wa kwanza wa Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Afrika uliofanyika Sanya, China, Yuan alisema anatamani mpunga chotara utaweza kukua katika nchi za Afrika, ili kutatua tatizo la usalama wa chakula barani humo. Sasa, matumaini yake yanatimia hatua kwa hatua.

Kutokana na juhudi za taasisi za utafiti wa kilimo na makampuni ya kilimo ya China, zaidi ya nchi 20 za Afrika zimepanda mpunga chotara wa China, na kuongeza mavuno ya mpunga katika nchi hizo kutoka wastani wa tani 2 kwa hekta hadi tani 7.5.

Nchini Madagaska, hadi mwaka 2025, eneo la kupanda mpunga chotara limefikia zaidi ya hekta 90,000, na mavuno ya wastani kwa hekta yalifikia tani 7.5, ambayo ni mara 2 hadi 3 ya wastani wa mavuno ya mpunga wa kienyeji. Madagaska imekuwa nchi ya Afrika yenye eneo kubwa zaidi la upandaji wa mpunga chotara na mavuno mengi zaidi ya nafaka hiyo. Hata serikali ya nchi hiyo imeweka picha ya mpunga chotara wa China kwenye noti kubwa zaidi ya fedha, na kuuita “Carabe”, maana yake ni zawadi bora. Kulingana na mpango wa Madagaska, katika miaka michache ijayo, nchi hiyo itaeneza upandaji wa mpunga chotara katika mikoa yote 23 ya nchi hiyo.

Nchini Burundi, wataalamu wa kilimo wa China wamesaidia kueneza teknolojia ya mpunga chotara, na kufanikiwa kuongeza mavuno ya mpunga nchini humo kutoka wastani wa tani 3 kwa hekta hadi tani 10, na kutoa mchango mkubwa katika kutatua tatizo la usalama wa chakula nchini Burundi. Methali ya Kichina inasema, ni afadhali kumfundisha mtu kuvua samaki kuliko kumpa samaki. Wataalamu wa China wametoa mafunzo ya upandaji wa mpunga chotara kwa watu wa Burundi, na kunufaisha karibu familia laki moja za wakulima.

Nchini Burkina Faso, mavuno ya mpunga kwa hekta kwa kawaida yalikuwa tani mbili au tatu tu hapo awali. Baada ya kupanda mpunga chotara kutoka China, mavuno kwa hekta yanaweza kufikia zaidi ya tani 10. Ofisa mmoja mwandamizi wa Wizara ya Kilimo, Rasilimali za Wanyama na Uvuvi ya nchi hiyo alisema, zamani nchi hiyo ililazimika kutumia zaidi ya dola milioni 16 za Kimarekani kwa mwaka kuagiza mchele kutoka nje ya nchi, baada ya kupanda mpunga chotara kutoka China, uzalishaji wa nafaka umeongezeka kwa kiasi kikubwa, nchi hiyo haihitaji tena kununua mchele kutoka nchi za nje. Badala yake, fedha hizo zinaweza kutumika katika miradi mingine ya kuboresha maisha, na kuwanufaisha watu wengi.

Nchini Msumbiji, mradi uliosaidiwa na China umepanda hekta 20,000 za mpunga chotara kusini mwa nchi hiyo, na mavuno kwa hekta moja yameongezeka kutoka tani 1.5 za awali hadi tani 8. Wenyeji wanatarajia kuwa miradi zaidi ya kama huu itaweza kutekelezwa nchini humo.

Nchini Kenya, mpunga unaostahimili ukame uliotafitiwa na Kituo cha Jeni cha Kilimo cha Shanghai kwa ajili ya nchi za Afrika umefanyiwa majaribio kwa miaka 7, na kupata mafanikio makubwa. Mradi huo unatarajiwa kuidhinishwa nchini Kenya mwaka huu, na kuleta matumaini mapya ya kujitosheleza kwa chakula kwa nchi hiyo, ambayo zaidi ya asilimia 80 ya mchele huagizwa kutoka nchi za nje.
 
Write your reply...kumbe mpunga wa tanzania umezidi kipato wa china maana kwa mbegu ya saro 5 kwa hekari moja unapata tani nne hadi nne na nusu na wachache hua wanapata hadi tani tano. zidisha mara mbili ili upate kipato cha hekta moja utaona inafika hadi tani tisa kwa hekta moja.hii ni mbarali mbeya
 
Back
Top Bottom