Dah! Mpwapwa ……. imehujumiwa sana. Mpwapwa ilikuwa ni kituo kikubwa sana cha ufugaji wa ng'ombe wa maziwa wa kisasa ambacho kilijengwa na wakoloni, kilihamishwa kinyemela kwenda kuwekwa kama sikosei Kilimanjaro. Kulikuwa na chuo cha walimu cha uhakika, Kambi ya JKT nafikiri bado ipo nk. Ilivyo Mpwapwa hivi sasa kimaendeleo nafikiri sio haki kwa wakazi wa Mpwapwa. Sio Mpwapwa tu ambayo wakati ule ilikuwa ni wilaya ambapo Kongwa ilikuwa wilaya ndogo. Wabunge wa hizi wilaya mbili hivi sasa wote hawafai kushika nyazifa zao, nitashangaa CCM ikiwapitisha wagombee tena ingawaje moja wao ndio Spika. Inakuwaje Spika anamiliki Petrol Station zote za wilaya ya Kongwa? Wengine wote wanapigwa vita?