Uchaguzi 2020 Mpwapwa tumekuchoka Mbunge wetu Lubeleje

Uchaguzi 2020 Mpwapwa tumekuchoka Mbunge wetu Lubeleje

Dah! Mpwapwa ……. imehujumiwa sana. Mpwapwa ilikuwa ni kituo kikubwa sana cha ufugaji wa ng'ombe wa maziwa wa kisasa ambacho kilijengwa na wakoloni, kilihamishwa kinyemela kwenda kuwekwa kama sikosei Kilimanjaro. Kulikuwa na chuo cha walimu cha uhakika, Kambi ya JKT nafikiri bado ipo nk. Ilivyo Mpwapwa hivi sasa kimaendeleo nafikiri sio haki kwa wakazi wa Mpwapwa. Sio Mpwapwa tu ambayo wakati ule ilikuwa ni wilaya ambapo Kongwa ilikuwa wilaya ndogo. Wabunge wa hizi wilaya mbili hivi sasa wote hawafai kushika nyazifa zao, nitashangaa CCM ikiwapitisha wagombee tena ingawaje moja wao ndio Spika. Inakuwaje Spika anamiliki Petrol Station zote za wilaya ya Kongwa? Wengine wote wanapigwa vita?
 
Sisi wapiga kura wako tumechoshwa na kuwa na Mbunge bubu bungeni. Tulikuchagua ukawasilishe mahitaji yetu bungeni na siyo kwenda kugonga meza.

Mpwapwa miundo mbinu ya barabara ni mibovu na shida ya maji ipo palepale na wewe unaendelea kugonga meza tu.

Jiandae kabisa maana uchaguzi wa mwaka huu hapati kura zetu maana tumekuchoka.

In God we Trust
Kweli anataka afie bungeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkipitishiwa magari ya muziki na kanga mnawapa tena madaraka
 
Back
Top Bottom