Mr Beast ajenga visima 100 vya maji barani Afrika

Mr Beast ajenga visima 100 vya maji barani Afrika

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Kwa project hii ataweza kunywesha maji watu takribani laki tano.

Nchi alizozigusa ni Kenya, Zimbabwe, Uganda, Somalia na Cameroon

Kwa msiemjua Mr beast, ni youtuber ambae kipato chake huki wekeza katika michezo ya kusaidia watu kifedha na projects za kusaidia jamii.

Hongera kwake.

View: https://youtu.be/mwKJfNYwvm8?si=U9kKln-zqQfJBVN0
 
Mungu ambariki the Beast kwa kazi kubwa anayoifanya kuwasaidia wenye mahitaji mbalimbali kwenye bara letu la Afrika.

Kwa kweli ni aibu kusaidiwa kisima cha maji ambacho pamoja na gharama kubwa za sasa za mafuta, haiwezi kugharimu zaidi ya shilingi 25,000,000 kukichimba.

Ni kama vile Afrika tumekosa Viongozi wa kuguswa na matatizo yetu, badala yake tumekuwa na Viongozi wanaoendekeza matumbo yao.

Poor us 😢
 
Kunywesha maji watu takribani laki tano !!!; Kudos kwa jamaa kujitahidi kufanya the right thing ila sustainability inabidi watu waanze kutunza mazingira na kuvuna ya mvua; Dunia ina matatizo ya Fresh water kuna only 2% na Afrika tungetumia maji kwa kufuja kama huko Ughaibuni yasingetosha kamwe.....

Mababu zetu knew how to use water efficiently na recently Kagame emefanya makubwa sana hata kufufua mito na chemichemi zilizokuwa zimekufa...; Its about time tuwe serious kuhusu long term water usage na hio ni kujikita kwenye water recycling pia...;

Lakini kwa Tanzania yenye maziwa makuu matatu Africa kulia kuhusu maji ni Upunguani....; Ila tukiendelea hivi huenda vita vitakavyokuja vitakuwa ni vya maji huko Egypt hawawezi wakafa kwa kukosa maji wakati wewe huko una Victoria yako na kujisifia kwamba ni yako....; As Human Beings we need to work together na ku-conquer mazingira..., We either survive together as a unit or die individually one at a time....
 
Mark of the beast 666 , wa kwenye kitabu Cha ufunuo 🤔
 
Nchi zetu bado zinapewa misaada ya visima na vyoo toka kwa wahisani. Hivyo visima vyote bei yake ni viete moja tu. Smh
Pamoja na jitihada za wahisani kuchangia ustawi wa Jamii zetu, bado siafiki na dhana kwamba Nchi yetu au nyingine za Kiafrika pamoja na Jamii zake, hazina uwezo au nia, au dhamira ya kujinasua. Kukosekana kwa vipaumbele kutoka kwa walio Serikalini, nadhani, ndio iwe motisha ya Wananchi kujenga Vyoo na kuchimba visima vyao wenyewe, kwani hakuna teknolojia yeyote ile mpya ya kufanya hivyo. Vyote hivyo vinahitaji mashimo!

Huyo Bisti apewe maua yake, ila hakuna cha ajabu alichokifanya, zaidi ya kujipendekeza tu kwenye jamii anayotaka kuinyonya. Hayo ni maoni yangu.

Ukizangitia Binadamu anaweza kufa siku tatu iwapo hato kunywa maji, basi utaona kuwa, sio serikali, na V8 zake au Wahisani na bilioni zao ndizo wanaotuweka hai.

Je itakuwa sawa kusema bila ya Serikali au bila ya Wahisani hatupigi hatua, itakuwa sawa? Sidhani!

Naamini Wananchi vijijini au sehemu yeyote ile yenye uhitaji wa maji katika ustawi wao, hawana budi kuwa na Uwezo wa kuchimba Visima au vyoo vyao wenyewe. Wafanye hivyo.

Badilisha fikra
 
Kodi wanachukua, huduma wajiletee wananchi yenyewe sio
 
1699471703687.png

Kama humfahamu Mr. Beast basi ingia YouTube kwa muda wako na umtazame. Ni kijana mdogo (25) anayefanya mambo makubwa kwa kutumia pesa nyingi. Hivi karibuni ametembelea Africa akiwa na lengo la kujenga visima vya maji safi 100.

Hakika lengo lake lilitimia. Alianza nchini Kenya ambapo alijenga visima zaidi ya 40+ kwenye vijiji tofauti ambavyo vilikua na shida ya maji. Hata hivyo hakuishia hapo. Katika ziara yake hiyo, kuna muda alikua anaelekea kijiji jirani na akakutana na daraja fupi la miti linalokatisha katikati ya mto. Wenyeji walimpa historia za hatari na kusikikitisha zilizowahi kutokea kwenye daraja hilo, hususani mto unapojaa maji. Mr. Beast aliwajengea daraja jipya la kisasa ambalo lina uwezo wa kudumu zaidi ya miaka 100+

Halikadhalika, Mr. Beast alifanikiwa kupita katika shule mbalimbali na kujionea miundombinu mibovu. Alihakikisha kila kitu kinaboreshwa. Kwa mfano, alijenga maktaba za kisasa na kujaza vitabu vipya. Pia alinunua madawati na kuboresha miundombinu ya darasa. Lakini pia alinunua kompyuta mpya kabisa.

Ziara yake iliendelea nchini Zimbabwe, Uganda, Somalia na Cameroon ambapo aliongeza visima katika kila nchi na kutimiza jumla ya visima 100. Akiwa Zimbambwe katika shule moja, aliwanunulia wanafunzi wote baiskeli mpya ili wasipate adha ya kufika shuleni.

Dunia ni sehemu salama tukiwa na watu kama hawa.
 
Back
Top Bottom