Pamoja na jitihada za wahisani kuchangia ustawi wa Jamii zetu, bado siafiki na dhana kwamba Nchi yetu au nyingine za Kiafrika pamoja na Jamii zake, hazina uwezo au nia, au dhamira ya kujinasua. Kukosekana kwa vipaumbele kutoka kwa walio Serikalini, nadhani, ndio iwe motisha ya Wananchi kujenga Vyoo na kuchimba visima vyao wenyewe, kwani hakuna teknolojia yeyote ile mpya ya kufanya hivyo. Vyote hivyo vinahitaji mashimo!
Huyo Bisti apewe maua yake, ila hakuna cha ajabu alichokifanya, zaidi ya kujipendekeza tu kwenye jamii anayotaka kuinyonya. Hayo ni maoni yangu.
Ukizangitia Binadamu anaweza kufa siku tatu iwapo hato kunywa maji, basi utaona kuwa, sio serikali, na V8 zake au Wahisani na bilioni zao ndizo wanaotuweka hai.
Je itakuwa sawa kusema bila ya Serikali au bila ya Wahisani hatupigi hatua, itakuwa sawa? Sidhani!
Naamini Wananchi vijijini au sehemu yeyote ile yenye uhitaji wa maji katika ustawi wao, hawana budi kuwa na Uwezo wa kuchimba Visima au vyoo vyao wenyewe. Wafanye hivyo.
Badilisha fikra