Mr Blue ndio Nyani Mzee kwenye tsnia ya muziki bongo

Toka Nikujue Leo umeongea bonge moja la point mshkaji wangu.

Agiza chochote hapo bili juu yangu.
 
Ikiwa Hip Hop itaenda kama inavyotakiwa iwe Young Killer anaweza akamzidi jamaa.

Mc Hammer alikua ndiyo msanii bora kwa kipindi kirefu lakini anguko lake lililetwa na gangster rappers mfano NWA, Ol Dirty Bastard, Naughty by Nature n.k. na kwa sasa naona gangster rap inashika kasi huku Bill Nas akiwa ameishikia bango.

Blue gangster rap hawezi sikiliza mistari yake kwenye ngoma ya Kesho, mule ndani aliyeonesha ana mwanga na aina hii ya rap alikua ni Young Dee pekee.

Young Killer kwenye baadhi ya ngoma ameonesha ana idea na hiyo style nina hakika akikazana na kujua upepo wa soko atatoboa zaidi ya Blue.
 
Mkuu Bill Nas anafanya Gangsta Rap?!

Hapo kwa Young Killer nakuelewa ila ninachosema akiweza kuwa kwenye kiwango iki kwa muda mrefu zaidi.

Maana kinachoonekana sasa Young Killer hayupo kwenye ubora ule aliokuwa nao Miaka miwili mitatu iliyopita.

Ametoa ngoma 3 mfululizo na zote hazijafikia ubora wa Dear Game,13 au Jana na leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…