Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Ili kuuita ni utapeli, njoo na takwimu halisi.

1. Watanzania wangapi wameweka pesa zao kufuga kuku na baada ya kufikisha miezi sita hawakulipwa?

2. Wangapi wamelalamika kudhurumiwa?
Utapeli sio mpakaa utokeee na watu walie ndo ujuee huu ni utapelii...!! Hata Ontario hadi leo huwezi jua ni Watanzania wangapi aliwatapeli so huo upuuzi wa kuhitaji statistics unaweza mtafuta mtuhumiwa
 
Mfanyabiashara, Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara ya haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za Umma zaidi ya Tsh. 17 bilioni.

Machibya ambaye ni mkazi wa Oysterbay amesomewa mashtaka yake leo 10/08/2020 na Wakili wa Serikali muandamizi mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya. Akisomewa mashitaka yake, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na 60/2020, kati ya mashitaka hayo 7 yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha za umma bila ya kuwa na leseni na kutakatisha fedha.

Mfahamu zaidi Mr. Kuku:
Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?
Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku
[emoji3516]
ALL IN ALL,
NDUGU_JOTI ANASEMAJE KATIKA HILI?
 
Ashakum si matusi. Tuwiane radhi, kawadhulumu wenye akili za kikuku.
Baada ya DECI, D9 na upumba.vu mwingi wa aina hiyo, watu bado hawakushituka ??

Kesho mwingine atakuja kwa staili nyingine na Ponzi scheme mpya na watu wataingia mkenge.

Hakuna hela ya short cut. Labda uibe, udhulumu nk.
Unatakiwa kufahamu kuwa kipindi cha DESI kuna wana jf wengi na wengine walikuwa hawajazaliwa, hawaelewi hayo mambo
 
Huyo nae mshamba tu si angejisepea kwenda duniani huko sasa imekula kwake.
 
Watanzania hatutatoboa kwa majungu. Mtu ameanza kidogo kodogo, sasa ametoboa na anasaidia wengi, badala umfanyie promo watu wainuke, unamwekea vikwazo.

Ameajiri wangapi?
Kodi kiasi gani kinalipwa?
Maisha ya wangapi yamenyooka kwa juhudi zake?

Kama halipi kodi ipasavyo, aelimishwe alipe kodi hizo siyo kumfunga.

Ujinga na kukomoana. Halafu sisi watumishi wa serikali tunaotegemea mishahara na rushwa za wananchi hatuwawazii mema wahangaikaji. Wakitoboa tunanuna.

Tuanzishe kazi za mikataba tu, nadhani tutaheshimiana
Jama hakukamatwa from no where ndugu yangu lazima kuwa mashahidi ambao ni walalamikaji kuwa malipo yao hawajapewa na hizo kelele ndo zimepelekea huko.
 
Mnaosema kakusanya 17 bilion na kwanini amebaki bongo inabidi mjue hizi hela hajazipata kwa mkupuo mmoja yaan amehesabiwa hela alizokuwa anakusanya kidogo kidogo tokea 2017 huko mpaka leo

Ooh kumbe.
 
Haya makampun ya kitapeli yamejaa,kuna moja inaitawa VKP INVESTMEST wauza viwanja kwa mkopo,watu tuliwaamini sababu ni registerd tumemaliza mikopo hakuna cha viwanja,mashamba wala kurudishiwa hela mwaka wa tatu kesi ipo mahakamani zaidi ya bilioni moja watz tumepigwa watu zaidi ya 300.Mmiliki wa kampuni hana pesa wala kiwanja cha kumpa mtu.
Sasa viwanja hamkupewa au mliambiwa mlipe kwanza then mkaonyeshwe viwanja.....
 
  • Thanks
Reactions: amu
Jamaa nilishangaa anauza 2018 Jaguar F-Pace kwa 250M! Nikajiuliza kulikoni. Kumbe mambo yalishaiva
Hapo no alichemsha,kumbe pesa alikuwa ananunulia mpaka Jaguar. Ila angekuwa anafuata aliyoyasema. Jamaa angekuwa millionea. Sema watu aliowadhulumu ndo walianza peleka malalamiko serikalini.
 
Kijana amebuni njia yake yakujipatia cake ya Taifa, jamaa wa Taifa wameona amezikusanya wameamua kufanya yao.Kwanini wasingemzingua kabla hazijafika kiasi hicho?
Huyu mtu anawekeza, haibi cha mtu. Ukifika shambani kwake unaona kabisa mabanda na kuku zaidi ya laki mbili. Ana masoko ya uhakika, anakusudia kujenga kiwanda cha kusindika nyama, kiwanda cha kutengeneza vyakula vya mifugo, zote hizo ni ajira kwa watanzania.

Pesa yote haiendi nje inabaki humuhumu. Sasa nyie mnaosema ni tapel, mmeifanyia nini nchi hii? Wazo gani la kuinua jamii mmeanzisha na likakubaliwa? Kumlinga mr Kuku na Ontario siyo sawa. Hata Ontario, unapoteza pesa kwa kukiuka misingi na tamaa
 
Daah sasa kuku wake now nani atawasimamia atakuta wahuni wameuza wamegawana chao...!! Sema jamaa atafute mwanasheria hata Peter Kibatala atachomoaa
Huyu mtu anawekeza, haibi cha mtu. Ukifika shambani kwake unaona kabisa mabanda na kuku zaidi ya laki mbili. Ana masoko ya uhakika, anakusudia kujenga kiwanda cha kusindika nyama, kiwanda cha kutengeneza vyakula vya mifugo, zote hizo ni ajira kwa watanzania.

Pesa yote haiendi nje inabaki humuhumu. Sasa nyie mnaosema ni tapel, mmeifanyia nini nchi hii? Wazo gani la kuinua jamii mmeanzisha na likakubaliwa? Kumlinga mr Kuku na Ontario siyo sawa. Hata Ontario, unapoteza pesa kwa kukiuka misingi na tamaa
 
Watanzania hatutatoboa kwa majungu. Mtu ameanza kidogo kodogo, sasa ametoboa na anasaidia wengi, badala umfanyie promo watu wainuke, unamwekea vikwazo.

Ameajiri wangapi?
Kodi kiasi gani kinalipwa?
Maisha ya wangapi yamenyooka kwa juhudi zake?

Kama halipi kodi ipasavyo, aelimishwe alipe kodi hizo siyo kumfunga.

Ujinga na kukomoana. Halafu sisi watumishi wa serikali tunaotegemea mishahara na rushwa za wananchi hatuwawazii mema wahangaikaji. Wakitoboa tunanuna.

Tuanzishe kazi za mikataba tu, nadhani tutaheshimiana
Kama kuna malalamiko mi nawaunga mkono kua ni tapeli . Lakini kama hamna malalamiko na analipa kodi ilibidi serikali wamuunge mkono . Ikiwekana wamsaidie kwenye ushauri na usimamizi . Wenzetu huko duniani wanaheshimu mawazo ya watu na kuwasaidia kuboresha. Angekua mtu wa nje tungemuona genius . Lakini tunapiga kila bila fact
 
Halafu ndo nimeanza kuelewa, nimeiona kwa Bon Jacob video lkn hata sikumtambua ni nani. Ndio maana tutaendelea kuwa maskini.

Wamgemsaidia kutatua chamgamoto hizo ndogo ili aendeleze mradi wake huo ambao unakomboa wengi
 
Back
Top Bottom