The end doesn't justify the means. Nchi inaendeshwa kwa sheria na taratibu; so hakutakiwi kuwa na excuse yoyote ya kufanya uhalifu; kosa liitwe kosa - kusiwe na lakini.... otherwise kila mtu atakuwa anavunja sheria akijua kuwa kuna mahali atasamehewa makosa yake ikiwa ataleta matokeo mazuri. Vipi kama akisababisha madhara kwa hicho anachofanya? Utasikia kila mtu anailalamikia serikali kuwa ilikuwa wapi kumchukulia hatua huyo mtu. Kwahiyo kwamba ameajiri watu, amelipa kodi, amenyoosha maisha ya watu bado haiondoi ukweli kuwa amefanya uhalifu. Hata wauza madawa ya kulevya wanaajiri watu, wanalipa kodi na wanawafanya watu watoboe... lakini madhara yake ni makubwa kuzidi faida.
Kwa mfano huyu bwana angeamua kusepa na mipunga ya watu... mngesemaje? Well, tuseme jamaa ni mwaminifu hawezi kusepa na mipunga ya watu; vipi kama akiamka siku moja akakuta kuku wote wamekufa, atawalipa nini wawekezaji wake? Is he insured? Kama unafikiri napiga porojo kamuulize Ontario atakusimulia kilichowakuta na TMT yao. Mpaka leo kuna watu wanatamani wamrarue Ontario - lakini na yeye aliajiri watu, alilipa kodi na aliwafanya baadhi ya watu watusue.
Na vipi kama watu wanamtumia yeye kutakatisha pesa = yaani wanafanya mishe haramu (Mfano kuuza madawa ya kulevya) halafu mapato wanayopata wanaenda kuwekeza kwa jamaa. How does he screen them? Hapo ndipo serikali inaposisitiza kuwa lazima uwe na leseni, kwasababu leseni hupewi kizembe - lazima wawe na uhakika kuwa hakuna janja janja utafanya kwenye pesa za watu, wala hutapokea pesa zilizotokana na mishe za kijanja janja.
Jamani, mnataka watapeliwe angalau watu wangapi ndo hili somo liwaingie? Tujifunze kutokana na makosa, lakini hayo makosa sio lazima tuyafanye sisi.