Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Mfanyabiashara, Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara ya haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za Umma zaidi ya Tsh. 17 bilioni.

Machibya ambaye ni mkazi wa Oysterbay amesomewa mashtaka yake leo 10/08/2020 na Wakili wa Serikali muandamizi mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya. Akisomewa mashitaka yake, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na 60/2020, kati ya mashitaka hayo 7 yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha za umma bila ya kuwa na leseni na kutakatisha fedha.

Mfahamu zaidi Mr. Kuku:
Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?
Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku
Wacheza upatu wako wa kila aina huyu alikuwa na wazo zuri ni kijana kajiajiri na kuajiri serikali inapaswa kumsaidia ..inaweza kupata suluhisho kubwa la ajira

Jr[emoji769]
 
Wajinga
Wapumbavu
Wahitaji
Wapo kila siku ...Mr Kuku katumia fursa vizuri ...hajaiba wametoa wenyewe na kuna waliopata kuna waliokosa...haya ni maisha usipothubutu utaishia kutumwa Maji misibani na kwenye vikao vya ndugu
Hata akina gwajima ni mr kokoriko wengine kwa gia ya dini

Jr[emoji769]
 
Kuna jinsi hela inakuwa chungu halafu unasikia kuwa hazirudi huku ukiwa na tumaini kuu kuwa hela utazivuna.

Sikuwahi kuelewa jinsi ya kuvuna wale kuku..nilieleweshwa sana siku hiyo nyumbani lakini wapi.

Kweli maisha ni akili..raha alizokula bro huyo toka 2017.Sasa kwa mfano tu hapo wakatia tia maneno akatoa za uchaguzi kama b10.
B7 akaachiwa then sisi tuliowekeza kuku wetu wa Kidigital tukatangaziwa jamaa amefilisiwa nani atajua?

Kwa sababu huyo jamaa unajua anaweza kuchangia kujengwa kwa Steigler Gorgee kule..au hata akachangia kujenga SGR kipande kidogo tu.
Nchii hii hela zipo na kuna namna tu

Wazee wenzangu wa Mzigo wa kubet twendeni zetu..Kuna Man U leo...kule Inter..
 
Afadhali swali nililo uliza kwenye moja ya uzi hapa limepata majibu..

Joti sijui naye atakamatwa kwa kutangaza biashara haramu.

Mfanyabiashara, Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara ya haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za Umma zaidi ya Tsh. 17 bilioni.

Machibya ambaye ni mkazi wa Oysterbay amesomewa mashtaka yake leo 10/08/2020 na Wakili wa Serikali muandamizi mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya. Akisomewa mashitaka yake, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na 60/2020, kati ya mashitaka hayo 7 yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha za umma bila ya kuwa na leseni na kutakatisha fedha.

Mfahamu zaidi Mr. Kuku:
Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?
Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku
 
Hela za deci mpk Leo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Serikali imejimilikisha uwezo wote wa kufanya dhambi "kihalali"!

-Kubeba silaha na kuua
-Haki ya kuvamia nchi yeyote na kuua raia wake
-Haki ya kufanya fujo
-Haki ya kudhulumu pesa za wananchi na kuwapa wengine
-Haki ya kusema uongo kwa "maslahi" ya taifa
-Haki ya kuchukua private property na kufanyia watakacho
-Haki ya kumiliki jeshi na silaha..mwananchi huruhusiwi
-Haki ya kuwapangia wanadamu wa hiyo nchi kipi cha kufanya na kipi sio cha kufanya kiwe kwenye sheria au kisiwepo
 
Hakuna pesa ya mtindo huo Mkuu, kila siku wanalizwa lakin hayakomi tu tangu lini pesa inatafutwa kwa kutumia vikundi, eti mtu ufanye nae share, vicoba, na sijui jumuiya hapa wajanja ndio watakao kula. Baadae inaanza migogoro na maujinga kibao hata kampuni tu zinaleta shida sembuse hayo ya kumwamini mtu.
Pesa hutafutwa na mtu binafsi na si vinginevyo.
Mwanangu kanipigia simu mda si mrefu. Nilimrushia hio clip! Ameshusha pumzi ya nguvu maana aliweka 3.5M...Nilichomjibu ni kuwa hio hela itafanyia shughuli za kizalendo kujengea barabara na mashule so asiwe na wasiwasi! Iko katika mikono salama.

Amejifariji kwa kusema in business kuna ku win na kujifunza.
 
Back
Top Bottom