Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Mr. Kuku ahukumiwa kulipa fidia TSh. Bilioni 5.4, faini Tsh. Milioni 5 au jela miaka 5

Hiyo B5 ikishawekwa kwenye accnt ya DPP inamaana wale walio tapeliwa ndo hawapat hata 100 mbovu ? Mbna kma serikali inashiriki utapeli sasa hiyo hela warudishe kwa walio tapeliwa na waache kujimilikisha
Sheria inasemaje??? Halafu AiSiiSii mnapeleka hili jalada nalo lini??
 
Waatharika ni wawekezaji wananchi wa kawaida wengi waliopoteza pesa, iliyokuwa mwenyewe account ya Tariq.
Fedha zao ndizo zilizochukuliwa na Ofisi ya serikali.

5 tena yaani!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hizi kesi sa kukubali mashitaka na kulipa fine ni mbinu za kuibia watu pesa.

Binafsi mpaka leo sijaelewa kosa la mr kuku. Maana kama mradi ulikuwa active na watu wanawekeza kwa free consent sasa kosa lipo wapi?
Ni Kweli kabisa, sio kama Qnet, labda leseni kukosekana, ubunifu wa namna hii, serikali ingemchukua na kumsaidia au kuchukua mawazo yake ili iweze kutengeneza ajira kwa watanzania.Hali ni ngumu mno kwa watanzania ndio maana watu wanatapeliwa na hizi network marketing.
 
Duuh noma kweli rafiki angu!!! Wangemuacha tu uyu chalii maana iyo m5 ni kama wemkomoa tu cuz wanajua kabisa hana kibunda chote wamelamba dadeki
Hahahahahah yani hii ni sawa na mtu kakufunga mikono halafu anakuzaba kofi kwa dharau...huku akisema "nipige basi nawewe"
 
Yani Bongo roho mbaya tu... Kwani Kampuni ngapi Zinaendesha Upatu bongo???? Sema watu wa rohoo za kwa nini wameona jamaa amepigaa mpunga mrefuu sanaa kiutani utani tu wakaamua Kublack mail wakombe pesaa.. Kama kweli sirikali ipo serious na kukataza maswala ya upatu why Qnet viongozi wake hawashikwii na ndio wanaaongoza kuibiaa watu hela tena mamilion kabisaa hasa wastaafu kila siku wanalia. Kuna wanafunzi wenzetu wamepoteza Dira kabisa kisa Qnet ilaa hapa Mr. Kuku baada ya kupiga parefu wakaona hapanaa lazima figisu ifanyweee.

Jamaa kapigwa faini mil 5 lakini too bad na pesa zote wamekombaa eti zinapelekwa serikalini kama ni Pesa haramu why ziwe halali kwa serikali bhasi WARUDISHIWE HAO WALIOZITOA HIZO HELA maana na document wanazo kwa kufanya hivyo sirikali itakuwa imewasaidia Waliokuwa wametapeliwa lakini kuzichukua ni kutapeli hao waliozichanga tena afadhali Mr Kuku angerudisha japo kidogo lakini Sirikali duu imekomba zote

Kampuni za upatu zinazoanzishwa hapa nchini toka nje ya nchi na Mabeberu kina Forever Living..Qnet..D9 na nyingine nyingi haziguswi kabisa zipo zinatapelii tu watuu. Ila mwafrika anzisha kampuni alafu kuwe na upatu ndani yake hakika Cha motoo utakiona hasa kama Ukifanikiwaa. Deci na Mr.Kuku uafrika ndio uliowaponza laiti kama wangekuwa wazungu hadi Waziri angeenda piga nao picha kuvutia wengine.

Mwisho kabisa tunajua upatu ni kosa kisheria lakini HII ISIWE KWA KAMPUNI ZINAZOANZISHWA NA WABONGO TU hata zinazoletwa na Wazungu nazo zifungiwe na kuburuzwa mahakamani wahusika tuache Kubaguana wenyewe kwa wenyewe na kuwatukuza wazungu. Kama ni kosa kwa Mwafrika zidhani kama ni sawa kwa Mzungu serikali iliangalie Hili.

HAKIKA ADUI WA MWAFRIKA NI MWAFRIKA MWENZIE MZUNGU ANASINGIZIWA TU.
 
Sasa huu ni utapeli wa serikali why wasirudishiwe waliozichanga na doc wanazo???
Unapigwa shtaka kisha zinakwapuliwa then shughuli inakuwa imeisha, sahivi sila nyepesi "Uhujumu uchumi" utatafutwa angle zote uingizwe kweny hio vanga.
 
Kwa mpunga huo mi naenda jela
Kama intention ni kukwapuliwa kiswaufu hata ukienda jela haisaidii kwa sababu hela washachukua. Bora kupunguziwa adhabu tu halafu inaonekana dogo ana asili ya dharau toka alipotoka kimaisha huko uraiani. Sidhani kama kwa business cycle aliokuwa nayo anakosa mtu wa kumpa 5M asiende jela.
 
Kumekucha Sasa Hivi
Kuna Jamaa Yangu Aliweka Cash Nyingi Sana
Muda Wote Alikuwa Anangoja Hatma Yaani Waonewe Huruma Sasa Hivi Ndiyo Jahazi Limezama!!!
Cash Imerudi Serikalini, Mr Kuku Hoi
 
Utakuwa una undugu au maslahi na Mr Bata
Nitapambana Na Rushwa Bila Kigugumizi Chochote Na Dawa Ya Jipu Ni Kulitumbua.
Nimejipa Kazi Ya Mtumbua Jipu
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Wakuu inakuaje serikali inachukua fedha kutoka kwenye account ya mtu bila ridhaa yake. Sheria za bank zimekaaje?
Yani unasemaje serikali inachukua bila ridhaa wakati wamekaa mezani jamaa akaridhia kumpa mitonyo DPP? Isitoshe jamaa yuko hatiani na keshakiri kwamba alifeli. Serikali ina mkono mrefu na inaweza kufanya hivyo kwa kufile order kwa banks tu ili walete taarifa zako za mipunga.
 
Back
Top Bottom