Mr Nice afunguka kuhusu utajiri wake

Mr Nice afunguka kuhusu utajiri wake

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mr.Nice akifunguka kuhusu utajiri wake ulivyotoweka ghafla!. Katika hali yakushangaza, Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice, finaly afunguka kuhusu utajiri wake na sababu za kushuka kwake kimuziki, katika moja ya interview.

Mr.Nice alidai kuwa hajui ni nini haswa kilichotokea ila yote hayo ni mipango tu ya Mungu. Mr.nice alizidi kufunguka na kusema kuwa, alikuwa na jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zote zikiwa katika account mbalimbali hapa nchini, na hela zote hizo zimetoweka katika kipindi cha muda mfupi bila yeye kujua zimetumikaje.

"Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu, kwani sikuwahi kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu, pesa yote nilikuwa naipata kwa hali, naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu" alisema Mr.Nice.

"Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama. Marekani,Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, SouthAfrica na kwingineko, na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana"

Alimalizia star huyo kutoka Tzee na mwanzilishi wa staili ya TAKEU.

Lucas-Mkenda-aka-Mr-Nice.jpg


Mbali na kushuka kwake kimuziki Mr.Nice anakiri kuwa ana-miss sana enzi hizo kwenye show zake zisizoweza kusahaulika na machozi huwa yanamtoka kila akumbukapo show aliyopiga nchini Rwanda.

Ambapo hadi waziri wa nchini humo aliweza kumsubiria airport kumpokea tena kwenye red carpet huku akisindikizwa na magari ya polisi, pamoja na mashabiki wake lukuki waliojaza uwanja huo wa ndege kushuhudia ujio wake.
 
Daaad,!!! Anatia huruma sema ndo maisha bwashee hakujipangaaaaa,,,,,
 
Daah ndo ashakuwa Historia hata kabla ya muda wake. Anajipanga kurudi tena au ndo amemshukuru Mungu kwa yote?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Alijiimbia jide hataki kuwa HISTORIA, tutakuja kusikia baadae, ooh nilipigaga picha na akina nelly na chris brown, nilikuwa mtanzania wa kwanza kushiriki BET , tutaona binamu , sisi wachawi aka ma haters tupo apa tunaangalia movie inavyoenda.
 
Kuna mwngine nae atakuja dai hivyo hivyo ngoja aendelee tu kuleta magari ya zamani na kudanganya kanunua kwa bethidei
 
bibie huyo ndo niagieni,hawezi rudi tena levo hizo

AHahaha haha jaman watu wachawi humu, muacheni mwenzenu bhana anajipanga na TAKEU style part 2, mi ananichekesha tu eti akikumbuka analia dah
 
Daah ndo ashakuwa Historia hata kabla ya muda wake. Anajipanga kurudi tena au ndo amemshukuru Mungu kwa yote?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

kurudi kwenye chati ni ndoto atafute tu pa kutokea kwa namna nyingine
 
Tatizo huyu mpare hana kipaji. alizifumania nyimbo za shule ya vidudu akazikopi, akajifanya yeye ndo MC HAmmer na kiburi chake.
 
Back
Top Bottom