Majuto ni mjukuu lakini hujachelewa kaka,
jamaa alikuwa na matumizi mabaya sana pia alikuwa mgomvi mno . nakumbuka siku moja tukiwa pale uwanja wa ndege wa JK Nyerere Mr nice alikuwa amerejea toka comoro akiwa na wacheza show wake alikuwa anakuja bear kwa fujo mno na kucheza hovyo alikuwa kero kwa kila mtu. lkn katika hari ya kushangaza Mr nice alichukua pombe yake ambayo ilikuwa kwenye kopo na kumwagia mzungu aliyekuwa amekaa pasipo hili wala lile.
na kisha akawa anamtolea maneno ya kijeri akisema mimi natembea dunia nzima na pesa ninayo hata huko kwenu wazungu wenzako wananitetemekea.
sawa polisi wetu wakamwita chemba na kuongea naye baada ya muda mfupi akaondoka, sasa hilo ni tukio moja la muda usiozidi dakika thelathini sasa vp kwa masaa 24, nani anajua wale polisi uliwapa bei gani?
pia kuna jamaa alitoka malawi akawa analalamika juu yako anasema kwa jinsi alivyokuwa nakupenda akaona ni bora akupe zawadi ya gari , jamaa anasema alikupa gari ambayo ilikuwa mark 11 old model nawe hukuonesha kuifurahia japo ulipokea , lakini cha kushangaza ukiwa unaimba kwenye onesho lako na huyu jamaa alikuwa mmoja wa wahudhuliaji na mulionana ukamtambua cha kushangaza ukaita pale kijana atakayeweza kuimba moja ya mashairi ya nyimbo zako na uliahidi kutoa zawadi ambayo hukuitaja , kuna kijana akajitahidi kuimba moja ya nyimbo zako na ukampa ufunguo wa ile gari aliyokupa mshaji , jamaa anasema alijisikia vibaya na kuamua kutoka nje na moyo unamuuma mpk leo kwa kitendo hicho.
inawezekana kabisa ukapata mafanikio makubwa kuliko haya ya mwanzo lkn badili tabia kaka